Hivi ni kweli Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuleta mapinduzi ya viwanda?

ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,651
2,790
Ndugu zangu sihitaji ushabiki na mihemko ya kisiasa, nahitaji mawazo chanya yatakayowastua watawala na kuwaonyesha muda unavyokwenda zaidi ya waliyotuahidi.

Ukimsikiliza Waziri wa Viwanda Bwana Charles Mwijage, utadhani yuko kwenye kampeni hataki kuamini kama yeye ndo Waziri na tayari anapaswa kuwa kwenye utekelezaji. Anaongea maneno mengi kuzidi mipango aliyo nayo.

Ananikumbusha mwanamziki mmoja aitwaye Shabba Ranks. Alikuwa na uwezo mkubwa akiwa stejini lakini aliposhuka tu anasahau yote aliyokuwa anaimba.

Je Waziri huyu anajua wajibu wake? Na kama hajui viwanda vitapatikanaje na muda ndo huo 2020 ishakaribia?

Tujadili.

0L7C1291.jpg
 
Tuendelee kuwakumbusha umebaki muda mchache sana ila sina uhakika kama watajenga kiwanda hata kimoja kikubwa tusubiri tuone
 
Wameshasahau hata hiyo Sera. Kilichobaki ni kukamata kamata watu tu
 
It is a truism and I can assure you that underdeveloped areas suffer from a shortage of capital and, generally, a surplus of labor including skilled one. Domestic capital resources may exist to some degree especially maeneo ya mijini tu, however, and the problem becomes one of tapping unproductive savings, providing means and motives for diversion of capital from traditional to novel investments, or perhaps establishing a system of “forced saving”(ambayo ipo kwa sasa hapa nchini) through the taxation system and fiscal policies of the state. Labor supplies are likely to represent underemployment in agriculture, but the actual diversion of labor to industrial employment is likely to require a reorganization of agriculture. I wonder kulikuwa na ulazima gani kuingia katika sera nyeti kama hii wakati majority wapo kwenye kilimo na jembe la mkono limekuwa likitumia miaka nenda miaka rudi! Perhaps sera ya kilimo ingekuwa na nguvu zaidi kwa kuwa inge-involve watu wengi zaidi! Jamaa zangu tunaolima nao mchicha hapa wana kamsemo eti VI-WONDER :D:D:D:D:D lET JUST WAIT AND WATCH..
 
Jmn, mm nilihudhiria mkutano mahala fulan mwaka jana kulikuwa na wabunge wengi tu wa ccm na walipewa nafac kuongea walialikwa km wageni ili waalikwa wengine wapate dondoo mbili tatu toka kwao.

Ss theme ya mkutano huo ilibeba ujumbe kuhusiana na kauli ya mheshimiwa kuhusu uchumi wa Viwanda. Katika kuchangia kufahamu mawazo ya serikali abt hiyo kauli ndio nkaishiwa pozi... Nanukuu Cz I do remember kuliko vyote vilivyoongolewa siku zote za mkutano

"Rais aliposema nchi ya viwanda hakumaanisha kuwa atajenga viwanda nchi nzima ili na watu wengine mpate ajira, alichokuwa anamaanisha ni juhudi zetu wananchi kila mtu ajitahidi awe na kakiwanda nyumbani kwake ikiwemo cha kukamulia alizeti, kutotoleshea vifaranga, mnajiunga kina mama mnaanzisha kiwanda cha kutengeneza sabuni nk. Hiyo ndio nchi ya viwanda aliyoyokuwa anaizungumzia Rais"

Sasa nyie endeleeni kumnukuu Rais vibaya..tutashaaaa
 
Back
Top Bottom