Hivi ni kweli Lowassa analipa kisasi?

Hivi ni kweli Lowassa analipa kisasi?

musami

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2011
Posts
1,434
Reaction score
460
Nimetafakari maneno aliyoandika mwandishi wa gazeti la Raia mwema ndugu Johnson Mbwambo, kwenye toleo la wiki hii Na.425. Anasema kitendo cha Lowassa kujiunga na Chadema, chama ambacho kwa miaka mingi kimekuwa kikimtuhumu kwa ufisadi ni kulipa kisasi.

Kwa maana sasa hivi Lowassa amekuwa aki-enjoy kuona jinsi wakina Lissu na Mbowe wanavyohaha majukwaani kumsafisha baada ya wao wenyewe kumchafua, kwake huo ni ushindi mkubwa hata kama atashindwa uchaguzi.

Pia kwa upande mwingine, ni kulipiza kisasi kwa CCM waliomkata, na sasa wanahaha kupambana na Chadema. Hata akishindwa atarudi kijijini kwake kama shujaa aliyewashikisha adabu adui zake.
 
Huyu mtu anayejiita Johnson Mbwambo sijui ana tatizo gani na Lowassa!
 
Ujio wa Lowassa UKAWA bila kujali atashinda/ kushindwa Uchaguzi ni neema kwa UKAWA, maana wingi wa viti vya udiwani na wabunge vitaongezeka sana...!
 
Ha ha ha, hapa Lowassa alicheza kama Maradona, mimi ningefurahi zaidi Dr Slaa nae angekuwa kwenye timu ya kumsafisha....

Sasa hata asiposhinda, nataka akamate uenyekiti wa CDM, Mnyika, Lema, Sugu tupa kule. Tunataka CCM B, kiwe chama chenye nguvu..
 
Naona uko kama unazolewa na upepo kila mahali upo, kumponda Lowassa upo kumhimiza afanye UKAWA iwe ccm B upo.. tulia upone haraka wewe LOWASSA NDIO RAIS WAKO KUPITIA UKAWA!!!
VIVA UKAWA!!
 
Daa! mkuu yawezekana kweli maana hata kauli ya lowasa na mbowe zinapingana, mbowe anasema trh 24 hadi 26 hakuna kulala lowassa anasema laleni usingizi wa pono
 
Daa! mkuu yawezekana kweli maana hata kauli ya lowasa na mbowe zinapingana, mbowe anasema trh 24 hadi 26 hakuna kulala lowassa anasema laleni usingizi wa pono

we subiri,hawa bavicha atakachowafanya lowasa hawawezi kumsahau kamwe...
 
Mbona tunajua kuwa ni weye umeandikayote hayo ila sasa unataka kama kuipasha moto habari kiporo?? Wadhani watu watabadilika tena sasa hivi??
Hapana, weshajiamulia rais wao ni nani. Sasa sana mkipunguza kura za Lowasa hazitazidi 10 Tanzania nzima. Atashindaaa mpaka mnazotaka kuiba ziwasute. MABADILIKO NI LAZIMAAAAA nje ya ccm
 
Ha ha ha, hapa Lowassa alicheza kama Maradona, mimi ningefurahi zaidi Dr Slaa nae angekuwa kwenye timu ya kumsafisha....

Sasa hata asiposhinda, nataka akamate uenyekiti wa CDM, Mnyika, Lema, Sugu tupa kule. Tunataka CCM B, kiwe chama chenye nguvu..
Kweli Dr.Slaa kumsafisha Lowassa kingekuwa kituko cha karne
 
Ujio wa Lowassa UKAWA bila kujali atashinda/ kushindwa Uchaguzi ni neema kwa UKAWA, maana wingi wa viti vya udiwani na wabunge vitaongezeka sana...!

Waambie waelewe hao wachumia tumbo.Hawajuwi kabisa kuwa Chadema hawana cha kupoteza, ni faida tu !
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom