Ni msemo ambao unanitia mashaka, kwamba eti Watanzania hawapendi kusoma vitabu.
Kwa nionavyo Mimi, kusoma kunaendana na MAHITAJI na HOBBY. Sidhani kama mtu ataokota tu kitabu bora kitabu na halafu akakaa siku nzima anasoma ili aonekane anapenda kusoma.
Nimejiuliza, hivi wale watanzania waliokuwa wakishinda na kukesha wakisoma vitabu vya au hadithi za ABUNUASI na ALFULELA ULELA, au riwaya za NJAMA au hata hadithi za kiingereza za ABDULI, SPEAR, TROUBLES, MY DEAR BOTTLE na nyinginezo nyingi, walizaliwa nje ya nchi?!
Ukweli ni kwamba tunajadili matokeo bila kushighulika na chanzo.
Leo ukienda katika maktaba nyingi vitabu na majarida utakayokutana nayo ni ki-magharibi, tena discard. Kwa mtanzania wa kawaida unadhani ataona uhitaji wake kweli?.
Wako wapi waandishi wetu mahiri wa enzi hizo na hata za sasa? Wameenziwa vipi na taifa hili, wamepata support gani ili kuidumisha tasnia hii adhimu ya uandishi? Maana wao ndio wanaojua mahitaji na kiu watanzania.
Embu jiulize kwa mfano, ni nakala ngapi za magazeti ya udaku yenye hadithi za kina Shingongo yanasomwa kila siku? Ni mengi kwa sababu kuna wenye uhitaji na kiu ya maudhui na ujumbe wake.
Si vema kutoa majibu marahisi kwenye mambo mazito. Tasnia ya uandishi na waandishi wa vitabu Tanzania imesahaulika kama si kutupwa, matokeo yake Wananchi wanapata uvivu wa kusoma mambo yasiyowavutia na au yasiyo na tija kwa mahitaji yao.