Msitari wa pambizo
JF-Expert Member
- Sep 25, 2014
- 3,085
- 5,417
Naomba swali hili liwe mahususi kwa jeshi la polisi na wapenda usalama wote. Huu mtaa wa keko uko jijini Dar es salaam katika manispaa ya temeke. naweza kusema ni mtaa tata tangu enzi na enzi na mpaka sasa matukiao ya ukabaji na wizi hayajaisha katika mtaa huu. SWALI LANGU NI JE HUU MTAA JESHI LA POLISI LIMESHINDWA KUUDHIBITI??
Siku mbili zilizopita kuna mwanafunzi mwenzangu wa chuo cha DUCE amekatwa mapanga kichwani na kusababisha hitilafu katika kichwa chake alipokuwa anatoka chuoni kusoma usiku wa saa 4 akiwa anaelekea nyumbani, na mpaka sasa amelazwa hospitali ya muhimbili kitengo cha mifupa (MOI) mustakabali wa uhai wake mpaka sasa haujulikani maana aliumia vibaya. HUU MTAA UMESHINDIKANA???
Cha kushangaza mtaa huu uko jirani kabisa na Kituo cha polisi Kilwa Road na kituo cha polisi Chang'ombe, kubwa zaidi upo karibu na kambi ya jeshi ya Mgulani. Hivi ni kweli vyombo vyote hivi vimeshindwa nguvu na hawa vibaka??
KEKO! KEKO! KEKO! KEKO! imekithiri kwa uhalifu nguvu ya ulinzi iongezeke.
Nawasilisha!!!!!!