Kimsingi hakuna tabia ambayo haiwezi kubadilika ikifanyiwa kazi. Ila urahisi au ugumu wa kubadilika tabia inategemea mzizi wa tabia yenyewe ulivyojikita ndani ya nafsi ya mtu. Kwa mfano kuna tabia za kurithi kutoka kwa wazazi, mf. hasira, ukali, nk. Hizi ndo tabia-hulka (nature). Tabia hizi zina mzizi mrefu sana, ili mtu aweze kubadilika anahitaji kusaidiwa sana, kutumia nguvu nyingi na njia nyingi, mazoezi mengi, na pia muda mrefu wa kutosha. Hata hivyo mtu hatabadilika kwa asilimia 100 lakini anaweza ku-improve.
Kuna tabia si za kurithi ila mtu kazipata kwenye mazingira aliyopitia mf. shuleni, vikundi vya marika, nk. Tabia hizi zina mizizi si mirefu sana japo zinaweza zikawa zimemkolea sana mhusika. Hizi zaweza kubadilika kirahisi kidogo ukilinganisha na zile za kwanza kwani hizi ni za kujifunza. Mtu akitumia nguvu, akajitahidi na kusaidiwa na wengine anaweza kubadilika.
Mtu anayekimbilia kusema: "we niache tu ndo tabia yangu" ni mtu aliyekata tamaa kufanya safari ya mabadiliko. Ni mtu anayetafuta udhuru, na asiye tayari kuumia ktk zoezi zima la kujibabadua na tabia yake (au kilema chake). Ni mvivu au mtu mwenye majivuno.