Hivi ni kwanini Tanzania tusianze kuzalisha umeme kwa kutumia uranium?

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,701
71,035
Najaribu kujiuliza ni kwanini nchi yetu isiangalie uwezekano wa kuzalisha umeme kwa kutumia uranium, maana madini hayo yanapatikana kwa wingi sana sehemu mbalimbali hapa nchini, au hatuna wataalamu wa kutosha wa fani hiyo au tunaogopa vikwazo vya wakubwa wa dunia au tunaogopa madhara yake?. Maana inasemekana kuwa umeme wa uranium una gharama ya chini kabisa na hauna madhara makubwa kimazingira.

Wakuu naomba tuelimishane
 
Kupitia tanesco pale na maumeme yao ya njia za zamani,..watu wanakula pale mkuuuu
af %kubwa ya umeme unauzwa nje
apa kwetu ni only 11% ndo wananchi wanaotumia umemee nchi nzima
 
Gas haitoshi sasa tuhamie kwenye uranium, sawa nako pakishindikana sijui tutahamia wapi!!!?
 
Najaribu kujiuliza ni kwa nini nchi yetu isiangalie uwezekano wa kuzalisha umeme kwa kutumia uranium, maana madini hayo yanapatikana kwa wingi sana sehemu mbalimbali hapa nchini, au hatuna wataalamu wa kutosha wa fani hiyo au tunaogopa vikwazo vya wakubwa wa dunia au tunaogopa madhara yake?. Maana inasemekana kuwa umeme wa uranium una gharama ya chini kabisa na hauna madhara makubwa kimazingira. Wakuu naomba tuelimishane
Kwanza wataalam hatuna, labda tuazime wa nje. Pili urutubishaji wa madini haya si wa siku moja au mwaka mmoja, na ni gharama sana. Sisi bado sana
 
Sasa mkuu si tungeanza kujiandaa wakati huu
 
Sasa kama mchakato ni mrefu kwa nn kusiwe na plan kuanzia sasa ili hiyo baadae watu wafaidike, kila marefu ya mwisho na mwanzo ni sasa!!
 
Mkuu uranium ni radioactive material ambayo inafikia mpaka half life ya 560 million years na pengine zaidi yapo. Hivyo inahitaji technology ya hali ya Juu sana kwenye matumizi otherwise nchi itapotea na viumbe wake wote endapo haitasimamiwa vizuri.

Hivyo nafikiri ni busara kuendelea kuiacha ibaki huko huko ardhini mpaka pale teknolojia yetu itakapokua tenge.

Lakini pia itahitaji mdahalo mpana sana kwa nchi za jirani na Tanzania au AU kuruhusu hili.
 
Kama tunataka kutengeneza Silaha za nyuklia hapo kweli litahitaji mjadala mkubwa, lakini kwa kuzalisha umeme sidhani
 
Gesi inaweza kutumika majumbani na kuokoa misitu yetu mkuu
Gas kutumika majumbani pekee nikuishusha thamani, basi tu kwa tanzania tumekuwa watu tulioshindwa kutumia rasilimali zetu ipasavyo, kwa vyote tulivyopewa bado tunashindwa kuvitumia hata tungepewa gas zote na uranium zote dunian bado tubgekuwa na matatizo ya nishat ye umeme.
 
Kweli mkuu yaani utafikiri tumelogwa
 
Kama tunataka kutengeneza Silaha za nyuklia hapo kweli litahitaji mjadala mkubwa, lakini kwa kuzalisha umeme sidhani

Mkuu nafikiri hukunielewa vizuri.. Maana yangu sio matumizi tu ya hiyo uranium bali mchakato mzima wakuichimba unahitaji teknolojia ya juu na hili linasimamiwa na International Atomic Energy Agency (IAEA) ambao ndio hutoa kibali cha kuridhika na teknolojia ya nchi husika.

Pia ukumbuke radioactive material yenye half life hiyo ni very sensitive. Vile vile kwa Afrika Uranium ipo Nigeria, Ghana, Senegal, Kenya, Uganda, Namibia na hapa nyumbani.
Nigeria na Kenya wamepeleka maombi IAEA muda mrefu kuomba kibali.

Ushauri... ikitokea Kenya wamepewa kibali cha kuchimba uranium kwa teknolojia waliyonayo sasa nakushauri hamia mashariki ya mbali kuepusha shari.
 
Mbona watu waliozunguka nchi zinazotumia nuclear power kama France na Germany hawajahama?
I think una overestimate risks za nuclear power.
Labda useme ikianza huku tuhame manake tunaogopa waendeshaji wa huku watakuwa wazembe na kuongeza risks za accidents.
 
Back
Top Bottom