Hivi ni kwanini Mabalozi wa nchi za Magharibi hawakushiriki mkutano wa CCM?

Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,781
3,209
Nimetafakari sana nikakosa majibu kwani sio jambo la kawaida kwa mkutano mkuu wa CCM kutokuhudhuriwa na Mabalozi wa nchi za Magharibi na hasa ikizingatiwa kuwa mkutano huu ulikuwa ni wa kumkabidhi Mwenyekiti Mpya kiti cha uongozi.

Nimepata taarifa kuwa walialikwa na Wizara ya Mambo ya Nje ,ila kwanini hawakukubaliana na Mwaliko huo sijapata majibu, ila niliposoma juu ya Operation UKUTA ya CHADEMA nilikuta sehemu wanataja kuwa kumbe kuna maagizo wamepewa kuwa hawana haki ya kukutana na vyama vya siasa bila kibali cha serikali.

Hili jambo sio jambo dogo maana inawezekana kabisa kuwa CCM ama imechokwa au kuna jambo linaendelea chini kwa chini kuhusu mahusiano ya Serikali hii na mataifa husika, ukiwaza kwa kutumia ubongo utaona ninachouliza ,lakini ukiamua kutumia zile akili za kushikiwa hutanielewa

Kwa mwenye jibu anaweza kutupia hapa, juu ya ni kwanini Nchi za Magharibi ziliamua kuisusia CCM ?
 
Sio kukutana na vyama vya siasa hawana vibali hata vya kufuatilia miradi ya fedha wanazozitoa sehemu mbalimbali za nchi kwa mashirika ya dini kijamii vyo hata shule ukiambiwa udikteta wa Magufuli umefika pabaya usishangae
 
Kabla huja anzisha mada
Ungeuliza kwanza

Mabalozi walifika au hawakufika.
Ulitaka balozi wanchi gani afike?
Maana wapo walie fika kutoka hukohuko ulipo pataja.
Lakini sio tatizo niyaleyale Ya vibendera
 
Hayo uliyo yaandika unauhakika nayo!!

JF mnapewa Tuzo ya uongo na Unafiki?
 
Sisi tunao tazama mambo kwa macho matatu, tunasemaga......
Heri upuuzi kuliko upuuzi mtupu
 
Kabla huja anzisha mada
Ungeuliza kwanza

Mabalozi walifika au hawakufika.
Ulitaka balozi wanchi gani afike?
Maana wapo walie fika kutoka hukohuko ulipo pataja.
Lakini sio tatizo niyaleyale Ya vibendera

Alikuwepo wa Uchina na baadhi wa nchi za Afrika kama Zimbabwe,n.k Swali langu nchi za Magharibi pamoja na Marekani mbona hawakushiriki?

Kuna mdau kaleta hoja ya msingi hapa kumbe mabalozi hawaruhusiwi hata kwenda kukagua miradi ya maendeleo ambako wametoa fedha zao ......this is serious
 
Ndio maana mnaitwa Vibendera fuata mkumbo

Haya endeleeni kudanganyana
 
Nimepata taarifa kuwa walialikwa na Wizara ya Mambo ya Nje ,ila kwanini hawakukubaliana na Mwaliko huo sijapata majibu, ila niliposoma juu ya Operation UKUTA ya CHADEMA nilikuta sehemu wanataja kuwa kumbe kuna maagizo wamepewa kuwa hawana haki ya kukutana na vyama vya siasa bila kibali cha serikali.
?

Hitaji la kutaka mabalozi kupata ridhaa/kutaarifu serikali ya nchi wanakowalisha kabla ya kukutana na wanasiasa, NGOs au hata kutembelea maeneo mbalimbali si amri ya Tanzania peke yake, bali ndio tararibu za kidiplomasia.

Balozi anapokuwa kwenye nchi fulani serikali husika inawajibu wa kutoa ulinzi na kuhakikisha wanafanya kazi katika hali ya usalama. Sasa kama Balozi mathlani wa wa Netherlands anaamua kwenda kukutana na watu anawajua yeye huko Nachingwea na ikatoea akapigwa na watu, serikali ya Tanzania itatoa majibu gani? Mabalozi wenyewe wanalijua hili lakini Tanzania ilikuwa ni shamba la bibi kila mtu anafanya anavyotaka.

Lakini cha kujiuliza, CHADEMA ndio wasemaji wa Mabalozi wanawakilisha nchi zao hapa Tanzania? Siku hizi hakuna Dean of Diplomatic Corps? Inakuwaje chama cha siasa kinakuwa msemaji wa wawakilishi wa mataifa ya kigeni tena kwa mambo ambayo ni kinyume na taratibu za uwakilishi wao?
 
Ulitaka CHADEMA wakae kimya kwa faida ya nani ?
 
Alikuwepo wa Uchina na baadhi wa nchi za Afrika kama Zimbabwe,n.k Swali langu nchi za Magharibi pamoja na Marekani mbona hawakushiriki?

Kuna mdau kaleta hoja ya msingi hapa kumbe mabalozi hawaruhusiwi hata kwenda kukagua miradi ya maendeleo ambako wametoa fedha zao ......this is serious

Karibu wataanza kufunga balozi zao. Hali hii haiashirii nia yoyote iliyo njema.
 
Walikua na kazi nyingine za kufanya.P
Alikuwepo wa Uchina na baadhi wa nchi za Afrika kama Zimbabwe,n.k Swali langu nchi za Magharibi pamoja na Marekani mbona hawakushiriki?

Kuna mdau kaleta hoja ya msingi hapa kumbe mabalozi hawaruhusiwi hata kwenda kukagua miradi ya maendeleo ambako wametoa fedha zao ......this is serious
 
Nimetafakari sana nikakosa majibu kwani sio jambo la kawaida kwa mkutano mkuu wa CCM kutokuhudhuriwa na Mabalozi wa nchi za Magharibi na hasa ikizingatiwa kuwa mkutano huu ulikuwa ni wa kumkabidhi Mwenyekiti Mpya kiti cha uongozi.

Nimepata taarifa kuwa walialikwa na Wizara ya Mambo ya Nje ,ila kwanini hawakukubaliana na Mwaliko huo sijapata majibu, ila niliposoma juu ya Operation UKUTA ya CHADEMA nilikuta sehemu wanataja kuwa kumbe kuna maagizo wamepewa kuwa hawana haki ya kukutana na vyama vya siasa bila kibali cha serikali.

Hili jambo sio jambo dogo maana inawezekana kabisa kuwa CCM ama imechokwa au kuna jambo linaendelea chini kwa chini kuhusu mahusiano ya Serikali hii na mataifa husika, ukiwaza kwa kutumia ubongo utaona ninachouliza ,lakini ukiamua kutumia zile akili za kushikiwa hutanielewa

Kwa mwenye jibu anaweza kutupia hapa, juu ya ni kwanini Nchi za Magharibi ziliamua kuisusia CCM ?
Soma sheria ya diplomatic utaelewa
 
Back
Top Bottom