Hivi ni kwanini dakika 45 ITV hamkaribishi watu kutoka vyama vya upinzani?

NAFIKIRE

JF-Expert Member
Sep 5, 2014
660
454
Wadau.

Nimemaliza kuangalia kipindi cha dakika 45 tano..Leo mgeni alikuwa Masha Mshomba mkurugezi wa mfuko wa fidia Tanzania akiohojiwa na mtangazaji Sam Mahela.

Mimi ni mpenzi wa kipindi hiki sana ila shauku yangu kubwa ni kuona kipindi kinakuwa cha pande mbili kwasasa kipindi kimekuwa cha upande mmoja sana.Kila siku mtu kutoka serikalini sijui ni nini.

Tunaomba Sam uwakaribishe na wageni kutoka "serikali kivuli". Mara ya mwisho kuhojiwa mtu kutoka upande wa pili ni alipohojiwa mbunge Msigwa kama nitakuwa sijakosea.
 
Yule mwandaaji Sam Mahela anatafuta ukuu wa wilaya...yani is lacking objectivity kabisa. Kazi yake ni kusifia serikali tu. Kwa kawaida mtangazaji au mwandishi hapaswi kuchukua upande wowote kwenye habari au stori yake au kipindi chake. Ila yule jamaa kazi yake ni kusifia tu, utasikia anasema, kwa kweli serikali inafanya kazi, hata sie waandishi wa habari tuona wazi kabisa. Sasa ulimuita wa nini kama unajua anafanya kazi vizuri?
 
Kipindi cha leo kilikuwa na manufaa sana kwa watanzania hususani kwenye suala la fidia kwa wafanyakazi. Ni vizuri tujifunze kutopinga kila kitu. Tuangalie yale ya kujenga kwanza.
 
Kwa sasa mgeni anatakiwa awe Charles Msonde ahojiwe kuhusu vyeti vya Bashite. Hao wengine ni kupotezeana muda tu
 
Yule mwandaaji Sam Mahela anatafuta ukuu wa wilaya...yani is lacking objectivity kabisa. Kazi yake ni kusifia serikali tu. Kwa kawaida mtangazaji au mwandishi hapaswi kuchukua upande wowote kwenye habari au stori yake au kipindi chake. Ila yule jamaa kazi yake ni kusifia tu, utasikia anasema, kwa kweli serikali inafanya kazi, hata sie waandishi wa habari tuona wazi kabisa. Sasa ulimuita wa nini kama unajua anafanya kazi vizuri?
Lisemwalo lipo
 
Muandaaji wa kipindi kaingia na woga kama walivyo watu wengi,hana ujasili wa kuruhusu fikra mbadala maana anawajua wataigaragaza serikali kwa nguvu ya hoja
Afu atakua anataka uongozi kama wenzie kwenye serikal hii
 
Tunataka na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi - (CUF) (Taifa) Professa Ibrahim Haruni Lipumba ahojiwe.
 
Wadau:
Nimemaliza kuangalia kipindi cha dakika 45 tano..Leo mgeni alikuwa Masha Mshomba mkurugezi wa mfuko wa fidia Tanzania akiohojiwa na mtangazaji Sam Mahela..
Mimi ni mpenzi wa kipindi hiki sana ila shauku yangu kubwa ni kuona kipindi kinakuwa cha pande mbili kwasasa kipindi kimekuwa cha upande mmoja sana.Kila siku mtu kutoka serikalini sijui ni nini..
Tunaomba Sam uwakaribishe na wageni kutoka "serikali kivuli". Mara ya mwisho kuhojiwa mtu kutoka upande wa pili ni alipohojiwa mbunge Msigwa kama nitakuwa sijakosea.
Sio serikali tu inayokurupuka hata sie raia pia.. Yaani mdau kaja tu kwa kashfa bila kupima amekuja kuleta pumba kwa Magreat thinker nimegundua some people wanachukulia humu kama sehemu ya soga zisizo na viwango.... Mkuu Nakushauri uende pale ITV ukawaulize nadhani utapata jibu murua maana Mtu kama mimi nilishawahi muona Peter Msigwa alitamka maneno kuhusu Naibu Spika na Serikali ikalima fine ITV kutokana na maneno yaliyotamkwa na Mh. Msingwa sasa na sio siku nyingi tuseme miaka kadhaa ni last year tu so unaonesha hata TV sio mfuatiliaji mzuri hivyo nakushauri acha Kashfa kama Bashite

Mahojiano ya Peter Msigwa ndani ya Dakika 45 ITV

Mkuu kama umesoma bandiko langu sijakataa kwamba wapinzani hawajawahi kuhojiwa..ila nimesema ni mara chache sana wapinzani wanahojiwa kwenye hicho kipindi..na nikasema kama sijakosea mtu wa mwisho kuhojiwa ulikuwa mbunge msigwa..ila kuanzia wakati huo kipindi kimekuwa cha upande mmoja sana mpaka kinatoboa sisi washabiki wake.
 
Mimi namtaka aalijwe mama ndalichako au mgeni kutoka NECTA tuna hitaj sana kusilia hekima zao kwa sasa

Cc Daudi
... Uko sahihi ilitakiwa Sam mahela kila panapotokea controversial issue, kama hii ya vyeti, immediately amualike waziri husika for clarification, pia kipindi kile live kwa watu kuuliza some few questions...
 
Mkuu kama umesoma bandiko langu sijakataa kwamba wapinzani hawajawahi kuhojiwa..ila nimesema ni mara chache sana wapinzani wanahojiwa kwenye hicho kipindi..na nikasema kama sijakosea mtu wa mwisho kuhojiwa ulikuwa mbunge msigwa..ila kuanzia wakati huo kipindi kimekuwa cha upande mmoja sana mpaka kinatoboa sisi washabiki wake.
Kwa mawazo yako kwamba wanaohojiwa wanaonesha kadi za chama husika? Kwani hakuna wapinzani ambao ni watendaji wa serikali wanaoalikwa kuongelea nafasi zao? Au unataka kipindi kigeuzwe cha kisiasa.
 
Kikubwa kumaliza mjadala ningefurahi na wale wanaoitwa watu wa serikali kivuli bungeni na wao wawe wanakaribishwa...
 
Wakaseme nini sasa, wakatukane unafikiri hao wamiliki wa media hawapendi kazi zao, zikifungiwa wapinzani wana nini zaidi ya porojo...Wapinzani wamewaandamanisha watoto wa maskini na sasa wamefungwa na wengine kufa wao wanakula maisha, na wao waanzishe ITV yao
 
Back
Top Bottom