ziko sababu nyingi za watu kuichukia TRA, nitatoa chache wengine wataongezea, kama ifuatavyo-
1. TRA wanaongoza kula rushwa;hawa ni miongoni mwa mafisadi papa,
2. TRA hawakusanyi kodi kutoka kwa matajiri bali kwa maskini, ndiyo maana utakuta TAJIRI ANATAKIWA ALIPE KODI 3.2 bilioni lakini analipa milioni 200, ushahidi upo. Cha kusikitisha maskini anakamuliwa alipe hadi senti ya mwisho
3. TRA wanawasaidia wafanya biashara wakubwa kukwepa kodi, moja ya mbinu kubwa inayotumiwa ni kuleta bidhaa kama transit kwenda nje ya nchi kama zambia/zimbabwe kupitia bandari yetu, hivyo hawatozwi kodi, lkn zikitolewa zinaingizwa ktk magodown mjini, kufunguliwa na kuingizwa sokoni. hili linafanywa kwa ushirikiano na watu wa TRA,
4. makamishina wa TRA wana ubia na wafanyabiashara wakubwa, ndio maana hata wakikamatwa na maofisa wa TRA, Maofia hupigiwa simu na mabosi wao na kuambiwa waaachie bila masharti yoyote? je baada ya hapo unatarajia nini kinaendelea? rushwa/bahasha???? etc
5.TRA wanatumiwa na chama cha magamba yaani c-c-m kuhujumu uchumi, kila anayechangia chama anapewa msamaha wa kodi ingawa huwa haisemwi bayana humu wamo hata akina home shopping centre;
6.TRA wanatumiwa na chama cha magamba yaani ce-ce-m kuwakandamiza wafanyabiashara wanaowasaidia vyama vya upinzani kwa kuwafilisi kabisa endapo hawatafuata masharti ya chama tawala.
Mifano
(a) kuna mfanyabiashara DODOMA alimpokea Mrema akiwa NCCR -Mageuzi 1995 na kumhudumia kwa kila kila. Ce-ce-m walituma Maofisa/makamishina wa TRA kutoka DSM kwenda kutathmini kodi anayotakiwa kulipa serikalini, hesabu waliompa hata kama angeuza mali zote za dukani asingeweza kumaliza kulipa kodi hiyo. kisha akaambiwa kwani shida yake ni nini, aache kusaidia upinzani mambo yake yatarekebishwa mara moja, alipokubali, kila kitu kikarudishwa katika uhalisia.
(b)Muulizeni Bakhresa(AZAM), upinzani ulipoanza alikuwa anawasaidia CUF/chama cha upinzani fedha za kampeni, Ngano yake aliyokuwa ameagiza kutoka Kilimanjaro iliyopitia bandari ya Tanga kuja bandari ya DSM,ilitangazwa kuwa ni hatari kwa afya ya walaji, walimtumia mkemia mkuu wa serikali, kisha ngano yote ilibebwa na malori ya Jeshi na kwenda kumwagwa Pugu kisha kuchomwa moto. kumbuka ngano hii ilikuwa imetoka kwa wakulima anaonunua miaka yote? Ndio maana unaona Bakhresa mapenzi yake kahamishia kwenye biashara zake, mpira wa Miguu na kaachana na siasa.
7. TRA hawakusanyi kodi na ndio wanaofanya nchi hadi leo haiendelei, nawaambia TRA wangeamua kukusanya kodi tusingehitaji fedha za wafadhili kuendesha nchi. Kenya wana nini cha maana lkn mbona nchi yao inaweza kuendeshwa bila misaada ya wafadhili? matokeo yake kodi zetu zinakusanyiwa mifukoni mwao na ndio maana watumishi wa TRA wana nyumba nyingi na ambazo wanaogopa hata kuishi humo. hebu fikiria unakuta mtumishi wa kawaida tu wa TRA ana nyumba yenye thamani ya milioni 800, je watumishi wa ngazi ya juu pamoja na makamishina wana nyumba za bilioni ngapi?
Ushahidi upo hatakatika mitaa tunayoishi,
Ingekuwa amri yangu, ningeifuta TRA na kuiunda upya ikiwa na sura mpya zisizo na harufu ya chama cha magamba kwani huu ni uhai wa taifa.Nchi ikiendelea kutembeza bakuli ndio imefikia wafadhili wanasema tukitaka misaada yao wanaume tushike ukuta/turuhusu ushoga??? je wanaume mnakubali ushenzi wa washenzi hawa wanaokuja kwa jianla wafadhili wakati wanaturudishia walichotuibia miaka ya ukoloni????
nanga natia naita mjadala upenuni