JET SALLI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2014
- 2,993
- 2,034
Ndugu zangu, nimekaa na kutafakari, nikaona hebu tujadili pamoja suala hili la uchaguzi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumbukumbu tulizonazo tangu tuanze mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, na uchaguzi wake wa kwanza mwaka 1995 pamoja na mapungufu yake makubwa.
Kuna kitu kinaitwa kanuni ya dhahabu. Tafsiri yake inasema: "Usimtengee mwenzako jambo ambalo hata wewe kwa namna yoyote usingependa utendewe." Vyama vya siasa nchini Tanzania vimeshiriki uchaguzi tangu mwaka 1995, na vingi vimedhulumiwa matokeo ya uchaguzi.
Mimi najiuliza, hivi kama CCM ingekuwa chama pinzani, kingevumilia wizi huu wa kura waziwazi kwa muda gani?
Je, vyama pinzani vinaridhika na tabia hii? Na vitaendelea kuridhika hadi lini, ikiwa wananchi tayari wamechoshwa na mwenendo huo? Kama wizi wa kura ndiyo njia pekee ya kuibakisha CCM madarakani, je, CCM inafikiri wananchi wafanye nini ili wapate viongozi sahihi kwa matakwa ya wananchi wenyewe?
Watanzania wa sasa si wajinga. Labda wajinga ni wale wanaolazimisha kuongoza kwa nguvu za dola. Uchaguzi uliokosa heshima kwa wananchi ulianza rasmi mwaka 2019, ukaendelea mwaka 2020 na hata huu wa mwaka jana 2024 chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. Ndani ya demokrasia, unajichagua mwenyewe bila kuhusisha wananchi, huku sheria zote za uchaguzi zikiibeba CCM.
Mwitikio wa No Reforms, No Election kila Mtanzania ameuona, na zaidi hata CCM wenyewe wameliona hilo. Watanzania wamechoshwa na wizi wa kura katika chaguzi, unaopeleka madarakani viongozi wajinga na wasioelewa majukumu yao. Viongozi wasiotumwa na wananchi bali wanaofanya kazi kwa ajili ya maslahi ya CCM pekee, huku wakiacha matatizo ya wananchi bila suluhisho.
Waswahili wanasema: kufanya kosa si kosa, bali kurudia kosa ndilo kosa. Basi No Reforms, No Election ndiyo dawa pekee ya kurudisha imani ya wananchi katika kuchagua viongozi wenye akili, maadili na uzalendo wa kweli.