Hivi ndugu ama mdogo wako huwa unampa shilingi ngapi ya matumizi chuoni?

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,612
4,713
Nimekuja na hii mada hapa kuna watu wana watoto wanasoma vyuoni.

Leo naulizia wale wenye wadogo zao ama ndugu zao wanaosoma vyuoni hivi kwa mwezi huwa unampa shilingi ngapi ya matumizi.

Wale wenye wadogo zenu ama ndugu zenu mnaowasomesha mavyuoni kwa mwezi huwa unampa ndugu yako ama mdogo wako shilingi ngapi ya matumizi?

Ama anatumia shilingi ngapi?
Nimeamua kuanzisha uzi huu maana kuna wengi wana ndugu, watoto, ama wadogo zao mavyuoni ili tuweze kujua na kupeana changamoto.

Karibuni
 
Jinsia ya kike.. 7,000 kwa siku
Nauli za mabasi mkoani kwenda na kurudi juu ya mzazi.
Yan 210,000 kwa mwezi.
 
Maisha yanatofautiana mkoa mmoja hadi mwingine,jinsia moja na nyingine.
Lakini Kwa kawaida fomu za kujiunga huwa zinaonesha makadirio ya pesa ya chakula,malazi,vitabu n.k.
 
Wa kiume namchapa na laki moja.wa kike nampiga na 80.wa kike wana njia nyingi za kuingiza pesa hata ukampa milioni kwa mwezi atapewa tu tena.wa kiume namnunulia tv wa kike simnunulii maana atapewa tu.wa kiume nampiga na Tecno na wa kike nampiga na ka toch maana atapewa Samsung galax A3 hata usipompa. ni hivyo tu ndugu mtoa mada
 
Wa kiume namchapa na laki moja.wa kike nampiga na 80.wa kike wana njia nyingi za kuingiza pesa hata ukampa milioni kwa mwezi atapewa tu tena.wa kiume namnunulia tv wa kike simnunulii maana atapewa tu.wa kiume nampiga na Tecno na wa kike napiga na ka toch maana atapewa Samsung galax A3 hata usipompa. ni hivyo ti ndugu mtoa mada
Huwezi kuwa serious unamleaje mtt wa kiume kilegelege hivyo,bila shaka umechangia kitu kisichokuwa na uhalisia
 
Inategemea kama anaishi chuo au amepanga nje matumizi ni tofauti.

Wanaoishi chuo kama ni msichana kwa mwezi mpe 200000 au na zaidi kulingana na mfuko wako hapa ni pamoja na chakula na matumizi. Sasa kwa chuo inategemea kama ana mkopo au hana kabisa. ila awe anajua kutumia vizuri

mvulana mpe 150000 kama hana mkopo kabisa. Zinatosha.

Kama ana mkopo hapa inabidi ujue ana %ngapi?? Inatosha au haitoshi? Maamuzi ni wewe..

Nb inategemea maeneo chuo kilipo chakula ni sh ngap? Hilo ni muhimu sana.
 
.kujua na kupeana changamoto
karibuni
seriously anataka changamoto kwenye kutoa pesa ya matumizi,? basi sawa lkn na shauri
angalia kwanza kipatochako na akili ya nduguyo ndio umpimie..
[akili kwenye matumizi ya pesa]
 
Hii inategemea na mwanafunz mwenyewe...msome kwanza akili yake kuna mwingine anamatumizi mabaya huyu ata umpe million bado haitatosha
 
Ukiwa umechoka sana 5,000 kwa siku = 150,000 per moon, otherwise kama mambo safi angalau umpe 7,000 na kuendelea per day = 210,000 au maximum 250,000 (isizidi hapo utamharibu maana huku uraiani kuna watu wanalamba kilo 5 na kamaliza chuo wakikata kodi mtu anabaki 400,000 na maisha yanakwenda sembuse mwanafunzi
 
Back
Top Bottom