Hivi ndivyo Tulivyo Watanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ndivyo Tulivyo Watanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mozze, Feb 9, 2011.

 1. m

  mozze Senior Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi sielewi kabisa mantiki ya watu kukimbilia kusema Chadema wanajimaliza Kisiasa kwa kutoka nje ya bunge..... kwa nini watanzania tunapenda conclusion (mahitimisho) rahisi na yasiyo na ukweli? Kwani hao CDM walipata wapi nguvu na wataipoteza vipi? Mbona pressure yao ya Katiba imeanza kuleta matunda?

  Je mtu kama hukubaliani na kitu, unalazimika vipi kukipokea? kama wao waliamua kutoka kwa sababu hawakubaliani na marekebisho wamefanya kosa gani? Wangebaki na kupitisha, baadae wakalalamika ungeona watu humu wanasema kuwa Chadema walipitisha sasa wanalalama nini.... hii ni tabia ya watanzania wengi kupenda kulaumu tu bila hata kufikiria!

  Kwa nini watu wanafikiria vyama vya upinzani nikitu kimoja? kama ingekuwa hivyo basi tungekuwa na vyama viwili tu, lakini kwa vile tuna vyama mbalimbali basi tuzikubali tofauti zao na kuacha kulazimisha wakubaliane ili tuwe na mantiki ya kweli kuhusu demokrasia..... tuache porojo, tuongee ukweli kwa manufaa ya nchi.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tafuta na tafakari wale wanaosema kwamba wanajimaliza, utagundua ni wale wenye nia ya kupindisha tafakuri makini za cdm
   
Loading...