Mleta hoja, mbona una mambo ya ajabu, ati wanapata mateso!! Au nimekusoma vibaya. Unadhani huwa wanang'olewa wakiwa hai??? Tembo hata akilipoteza jino kwa sababu yeyote huwa analizika kabisa huwazi kuliona weye. Ndo maana jangili akilitaka hamwombi au hambembelezi ili ampe bali anamtoa uhai kwanza halafu ang'oe kwa shoka. Hivyo usiseme Tembo anasikia uchungu, maiti hasikii uchungu tena. Hata akimwacha hapo kwa kuwaona maaskari, huyo maiti hana faida na meno yake tena.
Ndo maana twasema, Kukamata meno ya tembo tani elfu si hoja kwani tembo aliuawa ndipo jino likatolewa. Tuzuie ujangili kule mbugani sio kuzuia meno ya tembo yasiuzwe.
AK47 zilizo nunuliwa, hebu ziwafyeke majangili ili tembo wapone. Mbona hatujasikia hata mmoja aliyeionja AK47??? Nyalundu muhishimiwa, upo ofisini au upo Dodoma kwenye mchechetooooo