Hivi ndivyo safari ya Desemba 9 ilivyoanza!

Hivi ndivyo safari ya Desemba 9 ilivyoanza!

gefa

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2014
Posts
425
Reaction score
570
Habari zenu ndugu wana jamiiforums !

Naomba niwapitishe kwenye kumbukumbu za matukio yaliyo pelekea DE9 kuwa siku muhimu kwenye ukombozi wa nchi yetu kwa mara nyingine tena katika mwaka huu wa 2025 baada ya ile ya 1961!
Kwa ufupi kuanzia mwezi January 2025 ilionekana kuwa mwaka wa kihistoria kwenye nchi yetu.

JANUARY 2025 - Vyama vikuu vya kisiasa vilianza kushika uelekeo tofauti kila kimoja hapa nazungumzia CCM na CHADEMA. Kwa mara ya kwanza CHADEMA waliwathibitishia watanzania kweli wao ni walinzi wa demokrasi bila shaka yoyote, kwa kuendesha uchaguzi wa wazi na kidemokrasia uliopelekea kupatikana kwa uongozi mpya wa Mwenyekiti Tundu Lissu na waandamizi wengine! Wakati huohuo CCM wakijikuta wanakumbatia mfumo wa kidikteta bila kujiuliza mara 2, Samia Suluhu anawapiga ngwala na kujipitisha kuwa mgombea urais kupitia CCM kwa namna ambayo wanaccm wanajikuta hawana ujanja kuponyoka katika viganja vya Samia.

IMG_20250505_175153.jpg


FEBRUARY 2025 - CHADEMA wanaanza vuguvugu la kampeni ya NO REFORM NO ELECTION Kwenye vikao vya ndani ya chama na wanaanda rasilimali kuanza kampeni yao kuwafikia watanzania huku CCM wakiwa bado hawana wasiwasi na wakiamini watanzania watawasikiza kwenye maigizo yao.

MARCH 2025 - Kampeni ya NO REFORM NO ELECTION inaanza na kushika kasi haraka sana kiasi watu wanakuwa hawaamini nyomi ambayo chadema wanakusanya kwenye mikutano yao, Wananchi wanaonekana kuwaelewa chadema katika mikutano yao CCM wanashtuka na kunaanza kuibuka mambo mengi ! CCM wanajaribu kutumia vyombo vya dola kuidhoofisha chadema kwa kushirikiana na wanachadema waliokuwa wafuasi wa mbowe, kesi na matamko ya kuiminya chadema yanashika kasi sana.

IMG_20250122_153615.jpg


APRIL 2025 - Mtu muhimu kwenye hii safari ya kuelekea DE9 anakamatwa na kufunguliwa mashitaka ya uhaini!( hapa CCM waliamini kazi imeisha😁😁😁) huyu Tundu Lissu 🙌🙌. Hii ilienda sambamba na kuivunja chadema kwa kila namna, kuhusisha msajili wa vyama, tume ya uchaguzi, kesi mahakamani na ukatili wa polisi kwa kushirikiana na viongozi wateule wa Samia waliishambulia kampeni muhimu sana ya NO REFORM NO ELECTION!

MAY 2025 - Huu mwezi uliwaunganisha mwanaharakati Mange rasmi kuwasapoti chadema kwenye kampeni ya NO REFORM NO ELECTION na hapa ndipo walipoibuka kina Askofu Gwajima, mchungaji Malasusa na kisha kukafutiwa ndugu POLEPOLE!

JUNE 2025 - Chadema wanakimbiza mno kampeni ya NO REFORM NO ELECTION ila chama kinapigwa pini na kesi za jaji Mwanga, HECHE anasimama kama mshmbuliaji kiongozi huku akipewa support na kina Gwajima, Mange na taratibu POLEPOLE anaanza kukoleza moto!

JULY 2025 - Chadema pumzi inakata kabisa wanakuja kwa kujivutavuta kwa nguvu ya ushawishi na umahiri wa the genius Tundu Lissu katika kupangua kesi ya uhaini, kwa nyuma POLEPOLE akiendelea kulibeba vema gurudumu la mabadiliko kwa umahiri mkubwa akiambatana na mange na Gwajima bila kumsahau Rachel dangwa akipiga zile zake " weeeh muriloo"😁😁😁

AUGUST 2025 - POLEPOLE anakua kinara wa mchezo anapeleka mashambulizi hatari sana kwa ccm mtandao! Huku Mange na Rachel wakimpa kampani kila mmoja kwa style yake!

SEPTEMBER 2025 - Chadema wanakua smart wanawaachia gurudumu Mange na POLEPOLE wao wanakua bize na kesi zao! Hapa mwamba anaeibeba Tanzania anabaki ni POLEPOLE ndio top!

OCTOBER 2025 - POLEPOLE Anatekwa anabaki Mange ndio kinara wa vuguvugu la mabadiliko ya kweli ya Tanzania mpaka 29.10 sauti ya mange ndio sauti ya mwisho kuwapa watanzania tumaini la kweli kwa nchi yao! BOOOOM🔥🔥🔥🔥🔥 Mambo yanakua tofauti na matarajio ya wengi! Kila mtu anaelewa nini kilichotokea lakini CCM na Samia wanajifunika shuka usoni na kutangaza kua ni usiku sote tukalele wakati ni saa 7 za mchana mda wa lunch!😁😁😁🙄🙄🤬🤬🤬 KAMPENI YA MO 29 IMEPELEKEA VIFO VINGI INAKADIRIWA ZAIDI YA WATANZANIA 10,000 NA MAJERUHI WENGI SANA! Watanzania hawajakubali UHUNI ulioffanyika wanataka MABADILIKO YA KWELI NA YA UHAKIKA! Hapa ndio inaziliwa upya DECEMBER 09 2025 ya MAANDAMANO YA AMANI NA KIHISTORIA!

NOVEMBER 2025 - Kutokana na rekodi za waliouwawa kinyama kwenye MO29 kuwa ni vijana wengi zaidi wa GEN Z , Gen Z wanarudi na mikakati madhubuti ya kuhakikisha unapatikana ukombozi wa kweli wa kiuchumi na kisiasa kwa kuitisha MAANDAMANO MAKUBWA NA YA KIHISTORIA NCHINI TANZANIA chini ya kijana mzalendo ABIL ambae amesimama mstari wa mbele kuishambulia serikali batili ya Samia Suluhu kupitia mijadala mizito inayoendeshwa kwenye mtandao wa TIKTOK hakika DE9 haitakua ya kinyonge!

ABIL amekua mwiba mchungu kwenye miguu ya CCM kuendelea kuitawala Tanzania kimabavu! Akisimama kama kinara wa vuguvugu la mabadiliko kuanzia NOVEMBER hii na technique zake za mashambuli ni tofauti na waliotangulia Tanzania sasa iko katika kipindi muhimu sana kihistoria kwa yote yaliyotokea na yatayotokea tuwe macho kuelewa sote tunajukumu la kuijenga na kuilinda Tanzania bora kwa vizazi vijavyo!

NB: De9 ni mwanzo mwingine kuitafuta Tanzania yenye usawa, inayoheshimu haki za binadamu, utawala wa sheria ,fursa sawa za kiuchumi kwa wote na kuondoa walaghai ambao wanatumika na kwa maslahi binafsi wanainyonga Tanzania!

Watanzania tutafute maarifa ya kuiponya nchi bila uoga!

IMG_20250730_124333.jpg
 
Back
Top Bottom