Maisha ni safari ndefu, hili linafanana pia na maisha na safari ya Kitila Mkumbo!
Nakumbuka siku alipomshusha kwenye Gari Prof. Penina Mlama ili aongee na wanafunzi,enzi zile migomo bado ipo ipo UDSM. Hapo ndipo wengi tulipomjua Kitila Mkumbo, wakati huo akiwa ni kiongozi wa Kitivo cha Sayansi (naweza kurekebishwa endapo nimekosea).
Tukio hili kwangu mimi ndio limebeba historia ya Kitila.Wakati huo tofauti na vitivo vingine, Vitivo vya Sayansi na Uhandisi ndivyo vilivyokuwa na nguvu au tuseme vilikuwa active kwenye siasa za chuo.Kwa bahati mbaya au nzuri siasa walizoziamini ni katika kutumia nguvu! Kwa kitendo kile cha kukosa nidhamu kwa mama mtu mzima na kiongozi, Kitila alionekana shujaa, mwanamapinduzi na mtetezi wa wanyonge.
Kitila na mashabiki wake walitumia mwanya huo kujifanyia kampeni na Kitila akawa Rais DARUSO!Waliosoma miaka ile wanajua kikamilifu kama Kitila na Makamu wake Francis Michael Kasavubu walitimiza matarajio ya wapiga kura wao au la!
Kilichotushangaza wachache ambao tulikuwa hatumuungi mkono Kitila ni punde tu baada ya uchaguzi yule kijana mdogo mwenye haiba ya kijijini aligeuka kuwa 'mlokole" ! Hakuwa na meno tena kama ilivyotarajiwa na wengi!
Mshangao wetu ulihitimishwa na hatua ya kuajiriwa kama ADMIN kabla hata matokeo ya mitihani kutoka na kufanya kazi na walewale aliowadhalilisha!
Sikuwahi kumsikia tena hadi alipoanza kuandika makala magazetini na baadaye kuwa tulipomuona kuwa Mshauri wa CHADEMA na leo amekuwa Permanent Secretary ambaye ameahidi kuanza kuyatolea majibu kwa yale aliyokuwa anayafanyia harakati!
Natumaiani hata ushauri aliokuwa anaufanya kwa Mbowe na Lissu atautolea majibu.
Historia ya Mkumbo itaendelea...
Maono yangu yananiambia kuwa mtu wa Kwanza kuguswa na safari hii ya maisha ya Kitila atakuwa ni Mchumi Daraja la Kwanza Mwigulu Madelu Mchemba!
Kama sio ule WARAKA WA MABADILIKO NDANI YA CHADEMA ,uchaguzi wa Ubunge Iramba Magharibi mwaka 2015 ungekuwa tofauti sana!
Kazi kwako Mheshimiwa Nchemba Mapambano yameanza na natumaini unajua silaha unayotumiaga kushinda uchaguzi! Kwa kuwa hukutaka kuiondoa hali ile ya wananchi wa Iramba ili wewe na wenzio mtawale Daima sasa Fimbo ile ndio inaenda kukuchapa.
USISHANGAE KUSIKIA LOMBO KUMWELI IFIKAPO 2019!
Ahsante Mh. Magufuli kwa kunogesha Mpambano huu!
Songela zigizigi! Mwaka 2020 tuwe na helkopta mbili!