Hivi ndivyo nilivyo deal na Jirani Bahiri

Hivi ndivyo nilivyo deal na Jirani Bahiri

Even MOre

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
261
Reaction score
382
NRNE 🔨

Leo nimekumbuka wayback mkasa wa kama miaka 6 hivi nyuma.

Kuna kipindi nilipanga chumba maeneo flan nikiwa ni senior bachelor mmbobevu 😂 sasa kwenye nyumba ya mtaa niliopanga kulikuwa kuna chumba cha nje barabarani ambacho kilikuwa kinatumika kukodishwa kama kibanda cha biashara.

Baada ya kuhamia pale alikuja bwana mmoja akapanga chumba kile na kuweka duka la mahitaji ya kawaida ya nyumbani (Kioski) yale maduka ya mtaani. Lakini yeye hakuwa akiishi na sisi pale alikuwa akija asubuhi kufanya biashara yake na jioni kuondoka.

Sasa kulingana na kuwa wapangaji wenzangu wawili pale walikuwa na familia zao mean wameoa so hakuwa zoea haraka tofauti na mimi hivyo, so toka siku ya kwanza anakuja kufanya usafi vifaa vya usafi na maji aliomba kwangu.

Baada ya muda kama mwezi mmoja akitumia vitu vyangu kama fagizo, zoleo sometime maji mimi nili fikiri labda atanunua. Sasa jambo ambalo lilikuwa linakikera ni siku za weekend ambazo mimi sikuwa naenda kibaruani so natumia muda huo kupumzika , kwa kuwa yeye anawahi kufungua hivyo lazima aje mapema kukufunguza umpe vifaa vya usafi.

Nikawaza je huyu mtu ni kweli hana hela ya kununua fagio na zoleo almost kama elf 4 hivi? Oky nikasema ngoja nimfanyie surprise ya maana. Basi siku moja nikamuomba ANIKOPESHE TSH. ELF 5.

Baada ya kunipa nikaenda, jioni kabisa nikamwagiza dogo wa jirani akanunulie fagio na zoleo. Alipoteta nikamwambia peleka kule dukani mwambie nimekupa mimi umpelekee.

Baadae jamaa alinitumia text kuwa "Nashukuru nineona hivi vitu, nani kanunua? Nikamjibu haina shida kaka tumia tu, kuna mtu kaniletea sasa mimi ninavyo".

Baada ya siku kadhaa akanikumbusha deni la hela aliyonikopesha. Nikampa 500 hela iliuobaki kwenye kununua vifaa vyake, theni nikamwambia "Hiyo hela nilikuomba kwa ajili ya kukununulia vifaa vya usafi, hiyo ndiyo hela iliyobaki" 😂😂

Jamaa alinichukia mpaka nahama maeneo hayo.

Je, umeshawahi kukutana na kisa gani cha majirani wa aina hii? 👇🏻👇🏻
 
1749658907229.png
 
Kila siku jamaa ilikua lazima aje geto kwangu kuangalia Tv , akanizoea sana hadi akawa anaweka miguu juu ya kochi, kilichoniuma zaidi ni siku 1 alinikuta nipo na demu hajiongezi na yeye akaingia akaja kukaa kwenye kochi kuangalia Tv.

Masaa yanazidi kwenda demu anachelewa kwenda kwao ila mwamba hajiongezi ndo kwanza anatafuta vipindi vya kuangalia nikamwambia nataka kutoka akaniambia we toka ukirudi utanikuta, nikamwambia sirudi nataka kufunga mlango ndo akasepa.

Tangu siku hiyo ikawa kila nikimsikia anakuja nazima Tv namwambia sijalipia kifurushi, au namwambia mi ndo naenda kazini na nikaacha kuchekacheka nae hadi siku hizi haji tena
 
Ubaya ubwela every where 😆😆😆
 
Back
Top Bottom