Hivi ndivyo hali itakavyokuwa Yesu atakapokuja! Ni mshikemshike!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,527
Reaction score
7,121
Kama kuna habari tunayopaswa kuisikia tena na tena ni habari ya Ujio wa Bwana Yesu Kristo. Hilo ni tukio la hakika na la kutisha kwa wasiomwamini, lakini lenye furaha kuu kwa waaminio. Maandiko yanathibitisha wazi kuwa Yesu atakuja mara ya pili kama alivyokwenda mbinguni. Malaika waliwaambia wanafunzi: "Huyu Yesu, aliyetwaliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni, atakuja vivyo hivyo kama mlivyomwona akienda mbinguni" (Matendo 1:11).

Yesu mwenyewe alisema: "Basi mimi nikienda kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo." (Yohana 14:3). Yesu alizitaja dalili za kuja kwake. Dalili hizo karibu zote zimetimia:
  • Upungufu wa upendo na mmomonyoko wa maadili (Mathayo 24:12)
  • Vita, njaa, matetemeko ya ardhi, magonjwa ya ajabu (Mathayo 24:6-7)
  • Watu wengi kudanganywa na manabii wa uongo (Mathayo 24:11)
  • Habari njema kuhubiriwa duniani kote ili iwe ushuhuda kwa mataifa yote (Mathayo 24:14), nk, nk
Yesu atakapokuja, kutakuwa na ufufuo na unyakuo. Hayo yatafanyikaje?
“Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.” (1 Wathesalonike 4:16-17)

Siku hiyo kuu, tarumbeta maalum ya Mungu italia. Ndipo makaburi ya wale waliofariki katika Kristo yatafunguka, na miili yao itafufuka kwa utukufu. Watakatifu watakaokuwa hai wakati huo, nao watabadilika upesi—kufumba na kufumbua—na kuvaa miili ya utukufu, isiyoharibika. Kisha watakatifu wote, yaani waliokuwa wamefariki na walio hai, watanyakuliwa fasta kwenda kumlaki Yesu mawinguni. (1 Wakorintho 15:51-52). Yesu hatakanyaga ardhi siku hiyo. Ataishia mawinguni na kuwanyakua wateule.

Itakuwaje kwa wasioamini?
Siku hiyo, wasiomwamini Yesu hawatanyakuliwa. Nchi ambazo siku ya tukio hilo itakuwa usiku, kama watu wawili watakuwa wamelala kitandani—mmoja anayeamini atanyakuliwa, mwingine asiyeamini ataachwa (Luka 17:34). Katika maeneo ambayo itakuwa mchana, watu wawili watakaokuwa shambani—mmoja anayeamini atanyakuliwa, mwingine asiyeamini ataachwa (Luka 17:36).

Ghafla dunia itabaki na watu waovu tu. Majengo ya makanisa ya watu wanaoishi maisha matakatifu, yatabaki matupu—hakuna tena kuhubiri, hakuna ibada, hakuna wokovu. Wale waliokuwa wanasitasita kutubu, watatambua wameachwa. Walimu wa Neno, wachungaji, walokole—wote watakuwa hawapo.

Kifuatacho?
Baada ya tukio hilo la unyakuo, ndipo dhiki kuu itaanza, ambayo haijawahi kuwapo tangu mwanzo wa ulimwengu (Mathayo 24:21). Mpinga Kristo atatokea na kujidhihirisha, na kuanza kuwatesa waliobaki. Hakutakuwa na amani. Dunia itatawaliwa na hofu, mateso na mapigo ya kutisha. Waliomkataa Yesu na kupinga kwamba sio Mungu, watatamani kufa, lakini kifo kitawakimbia (Ufunuo 9:6).

Nini sasa kifanyike?
Ndugu yangu, habari hiyo sio hadithi za kutungwa, ni ukweli wa maandiko. Pinga usipinge, Yesu atarudi. Hatujui siku wala saa, lakini atakuja kwa siku watu wasiyoitarajia. Je, utakuwa tayari? Utakuwa miongoni mwao watakaonyakuliwa? Kama huna uhakika, ina maana bado hujaokoka. Amua leo kuokoka, usingoje kesho. Tubu dhambi zako, amini kuwa Yesu alikufa kwa ajili yetu na umpokee sasa kwa imani, awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako. “Tazama, sasa ndiyo wakati uliokubalika; tazama, sasa ndiyo siku ya wokovu.” (2 Wakorintho 6:2)

Ukifanya hivyo, Yesu atakapokuja, utakuwa miongoni mwao watakaonyakuliwa kwenda mbinguni.
 
Itakuwaje kuhusu magari na ndege za abiria zitakazokuwa zinaendeshwa na walokole, wakinyakuliwa? Ingawa Biblia haisemi moja kwa moja kuhusu ndege za abiria, magari, au mashine nyingine wakati wa unyakuo, maandiko yanatufundisha kuwa tukio hilo litatokea ghafla. Wanaomwamini Yesu, watanyakuliwa popote pale walipo — iwe ni angani, ardhini, kazini au kitandani.

Yesu alisema:
"Wawili watakuwa kondeni, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa; wawili watakuwa kitandani, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa." (Luka 17:34-36)

Hivyo basi, Yesu atakaporudi, kama marubani wa ndege wameokoka, na kunyakuliwa wakiwa angani, hali hiyo inaweza kusababisha ndege za abiria kupoteza mwelekeo au kuanguka chini.

Magari barabarani yataachwa yakienda kwa kasi bila udhibiti ikiwa dereva ni mkristo aliyenyakuliwa.

Treni, meli, mitambo ya viwandani, vituo vya nishati, hospitali — vyote vitaathirika kama wafanyakazi watakaokuwa kazini siku hiyo ni waumini watakaonyakuliwa.

Hii ina maana hata jukwaa letu hili pendwa, halitafanya kazi iwapo wanaotunza servers za JF na moderators watanyakuliwa siku hiyo.

Ni mshikemshike! Kutatokea vurugu, ajali, mtafaruku mkubwa, na watu wataanza kuulizana: “Wako wapi walokole? Wameenda wapi?”

Ni wazi ulimwengu utaingiwa na hofu kubwa kwa sababu tukio hilo litaathiri kila sekta ya maisha.

Watakaobaki, waliopata neema ya kusoma uzi huu au kusikia habari hizi makanisani, watajua kwa hakika: Yesu amerudi na wao wameachwa! Hali ya kilio na kusaga meno itaanzia hapo.

Ndugu yangu, Usiwe miongoni mwao watakaobaki. Muda wa maandalizi ni sasa. Mpokee Yesu, uishi kwa utakatifu, ili siku ile unyakuliwe pamoja na watakatifu wengine kwenda mbinguni katika makao anayotuandalia Yesu.
 
Kama kuna habari tunayopaswa kuisikia tena na tena ni habari ya Ujio wa Bwana Yesu Kristo. Hilo ni tukio la hakika na la kutisha kwa wasiomwamini, lakini lenye furaha kuu kwa waaminio. Maandiko yanathibitisha wazi kuwa Yesu atakuja mara ya pili kama alivyokwenda mbinguni. Malaika waliwaambia wanafunzi: "Huyu Yesu, aliyetwaliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni, atakuja vivyo hivyo kama mlivyomwona akienda mbinguni" (Matendo 1:11).

Yesu mwenyewe alisema: "Basi mimi nikienda kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo." (Yohana 14:3). Yesu alizitaja dalili za kuja kwake. Dalili hizo karibu zote zimetimia:
  • Upungufu wa upendo na mmomonyoko wa maadili (Mathayo 24:12)
  • Vita, njaa, matetemeko ya ardhi, magonjwa ya ajabu (Mathayo 24:6-7)
  • Watu wengi kudanganywa na manabii wa uongo (Mathayo 24:11)
  • Habari njema kuhubiriwa duniani kote kuwa ushuhuda (Mathayo 24:14), nk, nk
Yesu atakapokuja, kutakuwa na ufufuo na unyakuo. Hayo yatafanyikaje?
“Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.” (1 Wathesalonike 4:16-17)

Siku hiyo kuu, tarumbeta maalum ya Mungu italia. Ndipo makaburi ya wale waliofariki katika Kristo yatafunguka, na miili yao itafufuka kwa utukufu. Watakatifu watakaokuwa hai wakati huo, nao watabadilika upesi—kufumba na kufumbua—na kuvaa miili ya utukufu, isiyoharibika. Kisha watakatifu wote, yaani waliokuwa wamefariki na walio hai, watanyakuliwa fasta kwenda kumlaki Yesu mawinguni. (1 Wakorintho 15:51-52)

Itakuwaje kwa watakaoachwa?
Siku hiyo, wasiomwamini Yesu hawatanyakuliwa. Nchi ambazo tukio hilo litakuwa usiku, kama watu wawili watakuwa wamelala kitandani—mmoja anayeamini atachukuliwa, mwingine asiyeamini ataachwa (Luka 17:34). Katika maeneo ambayo itakuwa mchana, watu wawili watakaokuwa shambani—mmoja anayeamini atachukuliwa, mwingine asiyeamini ataachwa (Luka 17:36).

Ghafla dunia itabaki na watu waovu tu. Majengo ya makanisa ya watu wanaoishi maisha matakatifu, yatabaki matupu—hakuna tena kuhubiri, hakuna ibada, hakuna wokovu. Wale waliokuwa wanasitasita kutubu, watatambua wameachwa. Walimu wa Neno, wachungaji, walokole—wote watakuwa hawapo.

Kifuatacho?
Baada ya tukio hilo la unyakuo, ndipo dhiki kuu itaanza, ambayo haijawahi kuwapo tangu mwanzo wa ulimwengu (Mathayo 24:21). Mpinga Kristo atatokea na kujidhihirisha, na kuanza kuwatesa waliobaki. Hakutakuwa na amani. Dunia itatawaliwa na hofu, mateso na mapigo ya kutisha. Waliomkataa Yesu na kupinga kwamba sio Mungu, watatamani kufa, lakini kifo kitawakimbia (Ufunuo 9:6).

Nini sasa kifanyike?
Msomaji, habari hiyo sio hadithi za kutungwa, ni ukweli wa maandiko. Pinga usipinge, Yesu atarudi. Hatujui siku wala saa, lakini atakuja kwa siku watu wasiyoitarajia. Je, utakuwa tayari? Utakuwa miongoni mwao watakaonyakuliwa? Kama huna uhakika, ina maana bado hujaokoka. Amua leo kuokoka, usingoje kesho. Tubu dhambi zako, amini kuwa Yesu alikufa kwa ajili yetu na umpokee sasa kwa imani, awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako. “Tazama, sasa ndiyo wakati uliokubalika; tazama, sasa ndiyo siku ya wokovu.” (2 Wakorintho 6:2)

Ukifanya hivyo, Yesu atakapokuja, utakuwa miongoni mwao watakaonyakuliwa kwenda mbinguni.
Mathayo 16:28
"Amin, nawaambia, wapo baadhi ya wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti, hata watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake."

Fundi selemala aliyasema haya karine za kutosha huko nyuma lakini hadi leo hii imebakia ngonjera na walioambiwa saa hii walisha geuka mchanga
 
Mtumishi, ni sahihi mwanamke kuwa Askofu/Mchungaji?
 
Jibu utalipata kwenye uzi huu
 
Mathayo 16:28
"Amin, nawaambia, wapo baadhi ya wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti, hata watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake."

Fundi selemala aliyasema haya karine za kutosha huko nyuma lakini hadi leo hii imebakia ngonjera na walioambiwa saa hii walisha geuka mchanga
Rafiki yangu Mayu ngoja nikueleweshe vizuri maana ya andiko hilo la Mathayo 16:28 ulilonukuu:

Katika andiko hilo, Yesu alikuwa akiongelea tukio la karibu kabisa la kuonyesha utukufu wa Ufalme wake, ambalo lilitokea siku sita baadaye alipobadilika sura (Mathayo 17:1-9).

Katika tukio hilo: Yesu aliwapeleka Petro, Yakobo, na Yohana mlimani, kisha alibadilika sura mbele yao, uso wake ukang’aa kama jua na mavazi yake kuwa meupe kama nuru. Musa na Eliya walionekana wakizungumza naye. Na sauti ya Baba ikasikika kutoka mawinguni. Hali hiyo ndiyo aliyoimaanisha Yesu kwamba atakuja katika Ufalme wake, na wale mitume watatu waliuona huo utukufu na ufalme wake kabla ya kufa. Hivyo basi, Mathayo 16:28 ni unabii uliokwishatimia, hauhusiani na unyakuo au ujio wa pili wa Yesu.

Pamoja na jibu hilo ni muhimu utambue kwamba "kwa Bwana, siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja." (2 Petro 3:8). Hivyo Yesu hajakawia kuja. Kwa miaka ya mbinguni, tangu Yesu aondoke ni kama siku moja na nusu tu iliyopita.

Yesu hajachelewa kuja. Petro anasema:
"Bwana hakawii kutimiza ahadi yake kama wengine wanavyodhani kwamba anakawia. Bali huvumilia kwa ajili yenu, kwa kuwa hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikie toba."
(2 Petro 3:9)

Yesu anaendelea kuvumilia akisubiri watu wengi zaidi waokoke kabla ya hukumu.

Usisahau pia kwamba hata Manabii waliotabiri kuja kwa Yesu mara ya kwanza kama Masihi walikufa miaka mingi kabla Yesu hajazaliwa, lakini kila neno walilotabiri lilitimia (Mika 5:2, Isaya 7:14, Zekaria 9:9 nk). Vivyo hivyo, kurudi kwa Yesu mara ya pili kutatimia, hata kama kwa mtazamo wa kibinadamu inaonekana karne nyingi zimepita.

Mtu anayeona ujio wa Yesu kuwa ni ngonjera au hadithi za kale anakuwa amepofushwa akili zake na shetani kama Maandiko yanenavyo:
“...mungu wa dunia hii[shetani] amezipofusha akili za wasioamini, hata wasiione nuru ya Injili ya utukufu wake Kristo, aliye sura ya Mungu.”

Kwetu sisi tunaoamini, tunajua kuwa: “...bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia.” (Waebrania 10:37)

Mpokee Yesu sasa, wakati wa kuja kwake umekaribia kuliko unavyodhani. Na ukiona wengine wanadhihaki, wewe simama imara, maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe (Wagalatia 6:5)
 
Kama kuna habari tunayopaswa kuisikia tena na tena ni habari ya Ujio wa Bwana Yesu Kristo. Hilo ni tukio la hakika na la kutisha kwa wasiomwamini, lakini lenye furaha kuu kwa waaminio. Maandiko yanathibitisha wazi kuwa Yesu atakuja mara ya pili kama alivyokwenda mbinguni. Malaika waliwaambia wanafunzi: "Huyu Yesu, aliyetwaliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni, atakuja vivyo hivyo kama mlivyomwona akienda mbinguni" (Matendo 1:11).

Yesu mwenyewe alisema: "Basi mimi nikienda kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo." (Yohana 14:3). Yesu alizitaja dalili za kuja kwake. Dalili hizo karibu zote zimetimia:
  • Upungufu wa upendo na mmomonyoko wa maadili (Mathayo 24:12)
  • Vita, njaa, matetemeko ya ardhi, magonjwa ya ajabu (Mathayo 24:6-7)
  • Watu wengi kudanganywa na manabii wa uongo (Mathayo 24:11)
  • Habari njema kuhubiriwa duniani kote ili iwe ushuhuda kwa mataifa yote (Mathayo 24:14), nk, nk
Yesu atakapokuja, kutakuwa na ufufuo na unyakuo. Hayo yatafanyikaje?
“Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.” (1 Wathesalonike 4:16-17)

Siku hiyo kuu, tarumbeta maalum ya Mungu italia. Ndipo makaburi ya wale waliofariki katika Kristo yatafunguka, na miili yao itafufuka kwa utukufu. Watakatifu watakaokuwa hai wakati huo, nao watabadilika upesi—kufumba na kufumbua—na kuvaa miili ya utukufu, isiyoharibika. Kisha watakatifu wote, yaani waliokuwa wamefariki na walio hai, watanyakuliwa fasta kwenda kumlaki Yesu mawinguni. (1 Wakorintho 15:51-52). Yesu hatakanyaga ardhi siku hiyo. Ataishia mawinguni na kuwanyakua wateule.

Itakuwaje kwa wasioamini?
Siku hiyo, wasiomwamini Yesu hawatanyakuliwa. Nchi ambazo siku ya tukio hilo itakuwa usiku, kama watu wawili watakuwa wamelala kitandani—mmoja anayeamini atanyakuliwa, mwingine asiyeamini ataachwa (Luka 17:34). Katika maeneo ambayo itakuwa mchana, watu wawili watakaokuwa shambani—mmoja anayeamini atanyakuliwa, mwingine asiyeamini ataachwa (Luka 17:36).

Ghafla dunia itabaki na watu waovu tu. Majengo ya makanisa ya watu wanaoishi maisha matakatifu, yatabaki matupu—hakuna tena kuhubiri, hakuna ibada, hakuna wokovu. Wale waliokuwa wanasitasita kutubu, watatambua wameachwa. Walimu wa Neno, wachungaji, walokole—wote watakuwa hawapo.

Kifuatacho?
Baada ya tukio hilo la unyakuo, ndipo dhiki kuu itaanza, ambayo haijawahi kuwapo tangu mwanzo wa ulimwengu (Mathayo 24:21). Mpinga Kristo atatokea na kujidhihirisha, na kuanza kuwatesa waliobaki. Hakutakuwa na amani. Dunia itatawaliwa na hofu, mateso na mapigo ya kutisha. Waliomkataa Yesu na kupinga kwamba sio Mungu, watatamani kufa, lakini kifo kitawakimbia (Ufunuo 9:6).

Nini sasa kifanyike?
Ndugu yangu, habari hiyo sio hadithi za kutungwa, ni ukweli wa maandiko. Pinga usipinge, Yesu atarudi. Hatujui siku wala saa, lakini atakuja kwa siku watu wasiyoitarajia. Je, utakuwa tayari? Utakuwa miongoni mwao watakaonyakuliwa? Kama huna uhakika, ina maana bado hujaokoka. Amua leo kuokoka, usingoje kesho. Tubu dhambi zako, amini kuwa Yesu alikufa kwa ajili yetu na umpokee sasa kwa imani, awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako. “Tazama, sasa ndiyo wakati uliokubalika; tazama, sasa ndiyo siku ya wokovu.” (2 Wakorintho 6:2)

Ukifanya hivyo, Yesu atakapokuja, utakuwa miongoni mwao watakaonyakuliwa kwenda mbinguni.
Sidhani kama tunaelewana kuhusu ujio wa pili wa Yesu. Kwani Yesu alienda huko alipokwenda akiwa na mwili wa nyama,mifupa na damu? Atarudi kwa namna ipi? Maana kuna watu wana hekaya za unyakuo (rapture) na cinema za watu wanapaishwa angani!!! Hadithi za kijinga hizi kwa kusoma biblia bila kuelewa lugha yake. Yesu anarudi vipi? Atakuja Yerusalemu au wapi? Nini hasa maana ya alichosema kujusu kurudi kwake na nini maana yake halisi?
 
Kaka, Biblia iko wazi kwamba Yesu atarudi kama alivyopaa. Malaika waliwaambia wanafunzi: ‘Yesu huyu aliyetwaliwa juu mbinguni toka kwenu, atakuja vivyo hivyo kama mlivyomwona akienda zake mbinguni’ (Matendo 1:11). Pia Paulo anasema: ‘Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na sauti ya malaika mkuu… nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai tutanyakuliwa pamoja nao… ili tukutane na Bwana hewani’ (1 Wathesalonike 4:16-17). Hizi sio hekaya, ni ahadi ya maandiko. Kurudi kwake sio sinema, ni ukweli wa Neno la Mungu.
 
Back
Top Bottom