Papa Mobimba
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 1,153
- 1,359
Huko zamani watu walikuwa wanaamini kwamba dunia iko tambalale kama meza. Baadae wakaja watu kama Galileo wakasema dunia ni duara. Pia watu walikuwa wanaamini jua na mwezi ndivyo vinaizunguka dunia.
Wanasayansi hao kina Galileo, Kepler na wengine wakaanza kutuaminisha kuwa dunia ni duara. Dunia inazunguka jua. Vitabu vikatungwa. Tukafundishwa mashuleni. Dunia inazunguka jua. Dunia inajizungusha kwenye mhimili wake.
Spidi ambayo dunia inatumia kuzunguka kwenye mhimili (kama ni kweli) itakuacha mdomo wazi. Dunia inatumia kilomita 108000 kwa saa ( 108000km/hr) sawa na kilomita 30 kwa sekunde kujizungusha kwenye mhimili wake. Mzunguko huo wa kwenye mhimili ndio unaleta usiku na mchana. Kwa spidi hiyo kama dunia ingekuwa ndege ingechukua masaa manne tu kufika kwenye mwezi.
Ajabu ni kwamba licha ya spidi hiyo yote kuwa kubwa kiasi hicho lakini watu wala miti huwa haiteteleki wala kuyumba. Kuna watu ambao wakisafiri kwenye vyombo mfano gari huwa wanasumbuka na matatizo ya kutapika na kichefuchefu. Lakini spidi hii ya dunia haiwafanyi chochote.
Kwa kweli nimekuwa nikiwaza sana juu ya dhana hii. Mpaka sasa nimeanza kuacha kuamini kuwa dunia haizunguki jua. Sijui wenzangu mtazamo wenu ni upi