Bwana Mugabe hakubali degree za kuchonga ili uone wanakuthamini uwauzie nchi yako kwa bei ya kutupwa,yuko kwenye uongozi sababu anawatetea Wazimbabwe dhidi ya ukandamizaji wa wazungu,ndio maana Wazimbabwe wanamkubali wanataka afie kwenye kiti akiwa bado ni rais wa Zimbabwe,hakubali kununuliwa kirahisi kama hawa viongozi wetu,
Angalia hao hao waCanada ndio wamechukua dhahabu ya Tanzania kwa bei ya kutupwa na kutuachia mashimo makubwa ambayo hatujui yatazibwa na nini,siku hizi hadi mchanga wanachukua kwamba wanaenda kuupima kama una madini Ajabu,tuma madini ya kila aina lakini Watanzania ndio masikini wa kutupwa wakati viongozi wanapewa degree za ajabu ajabu kwa mchango upi alioutoa kwa wananchi wake kama hajui ni kwa nini anaowaongoza ni masikini kiasi hicho,ila anawatajirisha Wazungu
Subirini na China nao watataka kumpa degree ya PHD kabla hajastaafu kwa kuwapa miradi mingi Tanzania
Tumeshauzwa woote,tuna raslimali nyingi hapa nchini,madini ya kila aina,mbao,wanyama,vivutio vingi vya utalii,ardhi nzuri lakini Watanzania ni maskini wa kitupwa eti kuna slogan inasema
TUMEWEZA,TUMETHUBUTU NA SASA TUNASONGA MBELE,tunasonga mbele kwenda wapi? Kufanya nini mara NGUVU MPYA ARI MPYA NA KASI MPYA siku hizi wala haisikiki tena watu wameshajitajirisha kwa nguvu,kasi na ari mpya halafu mnawadanganya Watanzania?
MTANZANIA INATOSHA HAPA TULIPOFIKISHWA TUCHUKUE HATUA,