Hivi mtu anakunyimaje Amani

Hivi mtu anakunyimaje Amani

Labda nibadilishe mtazamo juu yake maana

Hahaha! Hongera sana kwa kupenda aisee! Ngoja Nikushauri kidogo ingawa itabidi uufuate ushauri huu kwa kuuadapt na mazingira yaliyopo baina yako na huyo Mwanamke.
Kitu cha kwanza, acha kujilegezalegeza, wewe ni mwanaume kwa hiyo futa kabisa swala la kulialia, wanawake hawapendi mwanaume anaejilizaliza. Wao huamini kuwa ni dalili ya udhaifu/mapungufu na kuwa mtu asieweza kutegemewa au kuaminika kimaamuzi .
Cha pili, usikimbilie kumtongoza na badala yake, jenga nae urafiki wa mbali. Hapa ina maana kuwa, jaribu kumzoea ila usipende kukaakaa nae kama vile huna kazi au kumfuatafuata kila mahali kama nzi.
Kama una namba yake, mpigie umuulize hali n.k kisha jali mambo yako. Pangilia ratiba yako ya kazi na umtengee dakika 10 tu za kumpigia kila siku.
Mtafutie zawadi nzuri kwa kumshtukiza. Hapa ina maana gani? Mtafutie kitu kama kadi nzuri ukiwa umeiambatanisha na perfume nzuri ya kike ambayo si ya bei rahisi, miwani mizuri ya jua, mkufu n.k bila kumtaarifu kuwa utafanya hivyo. Yaani usimwambie kwamba kesho utaenda kumnunulia kitu fulani na utamletea ukiwa umeambatanisha na kadi na ua jekundu bali umpe pale ambapo hakutarajia. Kadi isiwe ya mapenzi bali iwe tu ya kumsifia kuwa yeye ni mrembo, ana akili, blah blah blah, mnaujua uzushi wenu vijana.
Subiria reaction yake. Kama ataipokea zawadi na kuipenda, utakuwa umefungua milango yake ya akili na ataanza kukufikiria, sio lazima iwe kimapenzi bali walau utakuwa mawazoni mwake tu hata kama rafiki. Epuka zawadi ambazo ziko common au zile ambazo zinaashiria mapenzi moja kwa moja kama vile kufuli, sidiria, perfume za bukubuku n.k kwani hizo huashiria wewe kuwa mjinga, una mawazo ya kitoto, una papara na hujakomaa kifikra. Halafu cha mwisho, Usije ukawa unatusumbua hapa halafu ukawa unatongoza watoto wa sekondari. Anza na hayo kwanza kisha tutakuelekeza mengine baadae.
 
hahaha! Hongera sana kwa kupenda aisee! Ngoja nikushauri kidogo ingawa itabidi uufuate ushauri huu kwa kuuadapt na mazingira yaliyopo baina yako na huyo mwanamke.
Kitu cha kwanza, acha kujilegezalegeza, wewe ni mwanaume kwa hiyo futa kabisa swala la kulialia, wanawake hawapendi mwanaume anaejilizaliza. Wao huamini kuwa ni dalili ya udhaifu/mapungufu na kuwa mtu asieweza kutegemewa au kuaminika kimaamuzi .
Cha pili, usikimbilie kumtongoza na badala yake, jenga nae urafiki wa mbali. Hapa ina maana kuwa, jaribu kumzoea ila usipende kukaakaa nae kama vile huna kazi au kumfuatafuata kila mahali kama nzi.
Kama una namba yake, mpigie umuulize hali n.k kisha jali mambo yako. Pangilia ratiba yako ya kazi na umtengee dakika 10 tu za kumpigia kila siku.
Mtafutie zawadi nzuri kwa kumshtukiza. Hapa ina maana gani? Mtafutie kitu kama kadi nzuri ukiwa umeiambatanisha na perfume nzuri ya kike ambayo si ya bei rahisi, miwani mizuri ya jua, mkufu n.k bila kumtaarifu kuwa utafanya hivyo. Yaani usimwambie kwamba kesho utaenda kumnunulia kitu fulani na utamletea ukiwa umeambatanisha na kadi na ua jekundu bali umpe pale ambapo hakutarajia. Kadi isiwe ya mapenzi bali iwe tu ya kumsifia kuwa yeye ni mrembo, ana akili, blah blah blah, mnaujua uzushi wenu vijana.
Subiria reaction yake. Kama ataipokea zawadi na kuipenda, utakuwa umefungua milango yake ya akili na ataanza kukufikiria, sio lazima iwe kimapenzi bali walau utakuwa mawazoni mwake tu hata kama rafiki. Epuka zawadi ambazo ziko common au zile ambazo zinaashiria mapenzi moja kwa moja kama vile kufuli, sidiria, perfume za bukubuku n.k kwani hizo huashiria wewe kuwa mjinga, una mawazo ya kitoto, una papara na hujakomaa kifikra. Halafu cha mwisho, usije ukawa unatusumbua hapa halafu ukawa unatongoza watoto wa sekondari. Anza na hayo kwanza kisha tutakuelekeza mengine baadae.

nimekupata ila hayo itakua maigizo maana hayo ndio siwezi kufanya hata siku moja.
 
Back
Top Bottom