Hivi Mjadala wa Katiba mpya tunamwambia nani hasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Mjadala wa Katiba mpya tunamwambia nani hasa?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Mathias Byabato, Dec 16, 2010.

 1. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #1
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Nafuatilia mjadala wa ama kuwepo au kuwepo kwa mchakato wa katiba mpya unavyoendelea hapa nchini.

  Lakini ukifuatilia kwa makini utagundua kuwa wadau wakuu serikalini,wasomi,.wananzuoni,Marais wastaafu wanakubali kuwepo kwa katiba nchini Tanzania wakiwemo pia watendaji wa serikali nk.

  Sasa kama hawa wanakubali kwa nini tusianze mchakato au Mpaka nani aamue kuanza kwa mchakato.

  Kwa sababu mimi naona kama tunapiga kelele kwani watu wote wanasema bila kuwa wazi hasa NANI ANATAKIWA KUSEMA TAUNZE.

  Wengi watasema serikali,lakini nani mwenye maamuzi Rais,wananchi,bunge nani hasa tuwe wazi(au nisaidie nijue)

  Byabato
   
 2. N

  Nonda JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Mimi nilitegemea kwa vile huu mjadala umepamba moto, vyama vya upinzani hasa vingeandaa hoja ya kuibadili katiba au kuifanyia mabadiliko significantly hii iliyopo.Kwa umoja wao wakaiwasilisha hiyo hoja bungeni kama hoja ya number 1 ya upinzani katika Bunge. CCM kwa jinsi wanavyokaririwa katika vyombo vya habari ni kuwa wanasubiri wasukumwe ingawaje wanakubaliana na hoja ya mabadiliko ya katiba au katiba mpya.

  Ukizungumzia serikali ,hapa unazungumzia CCM na CCM hawaoni haja ya kuibadili katiba inayowanufaisha kama Chama cha siasa, inayowahakikishia kubaki katika madaraka.

  Ninasema hivi kutokana na kumbukumbu ya kuwa vyama vya upinzani vilikwishatengeneza rasimu ya Katiba huko nyuma. Baada ya hatua ya kuipeleka hoja bungeni, sambamba na kuandaa something like one million people Katiba mpya match katika jiji kama dar na 200000- 500000 people match katika miji mikubwa yote Tanzania ili kuwashirikisha wananchi kutoa ujumbe kwa serikali kuwa watanzania wako tayari kwa Katiba mpya.

  Pia kuunganisha nguvu za vyama vya siasa,asasi za kiraia na vyama vya kitaalamu kama vya wanasheria,wasomi, vyama vya wafanyakazi na kila anayependelea katiba mpya katika kuipa msukumo hoja hii ya katiba mpya.

  Mambo haya yaende sambamba. Na isiwe na utashi wa kukipa ujiko chama fulani cha siasa au kikundi chengine chochote. Maslahi ya umma/taifa ndio kiwe kipaumbele katika hili..

  Kuna wengi wanaodai, wanaotaka katiba mpya lakini hakuna coordination na sauti ya pamoja. Suali ni nani ata-assume hiyo responsibility ya coordination?
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  labda tunamwambia dr (mwenye zile 5!)
   
Loading...