Hivi maisha yanawafanyaga nini wadada mpaka mvuto unapotea?

kijana mkimya

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
277
121
Hii imenitokea sana unakutana mdada mliokuwa unasoma nae, kipindi yuko shule alikuwa anaonekana mrembo kweli alikuwa tishio kwa kila mtu ila ukikuta nae tena mtaani baada ya kupotezana miaka kadhaa dah utashangaa muonekano wake amenyorodoka anaonekana kama mchafu fulani hivi hana mvuto tena yupo yupo.

Kama kipindi upo nae shule ulikuwa unaplan uje kumfanya mke unainua mikono juu na kushukuru Mungu uamuzi wako ulifeli mana muonekano ziro kwasasa. Hivi haya maisha yanawafanyaga nini miaka mi 2 tu mtu anakua hatazamiki mara mbili aiseee, tatizo nini?
 
Teh,hlo la kawaida mkuu.wengi wakiwa mashuleni ama vyuoni huishi maisha ya kuigiza.lakini wakiingia mtaani inawapasa waishi maisha halisi
 
Yawezekana alikuwa mrembo na sio mzuri.

Maisha yana changamoto sana, yawezekana pia kapata emotional breakdown au kachomoa ujauzito.

Mambo hayo huwafanya wanawake watoke from hero to zero.
 
Maisha yanawapiga mara nyingi ukiwa shule unahudumiwa kila kitu ila ukiwa nyumbani huduma zinapungua au kunakuwa hakuna huduma kabisa na kuanza kujitegemea
Mkuu sio maisha kuwapiga .. ona hii
Nikiwa primary nilikuwa na gf wangu mrembo kweli kweli .. sio siri kata nzima hakuwepo wa kumfikia ...
Baada ya muda mi nilitoka kwenda Sekondary na kumuacha kijijini akisoma sekondari ya kata iliyokuwa hapo kwetu. Tulikuwa na mipango mingi sana ya kimaisha. Wazazi wake walikuwa wananifahamu na mimi wazazi wangu walimfahamu huyo mdada.
Nikiwa form IV mwezi Juni dada huyo alikuja shuleni kunitembelea na kuniaga, wazazi wake walimlazimisha kuolewa na tajiri mmoja aliyetokea jijini Dar na kumwaga mapesa mengi kwa wazazi.
Kweli tuliagana, alilia sana, niliumia sana kwani nilijua ndo mwisho wa safari yetu ya mapenzi.

Baada ya miaka miwili nilionana naye akiwa tayari ameishazalishwa mtoto mmoja, alikuwa amenenepa japo sio sana. Tulipanga wapi pa kukutana na kukumbushiana na hilo lilitendeka kama tulivyopanga.

Baada ya miaka kama 10 hivi, mdada huyo alinipigia simu akiwa hotelini akitaka niende nionane naye kwani ni siku nyingi tumeonana ... jamani ...
Nilikutana na kiumbe wa ajabu ... mkono mkubwa kama paja, kiuno hakipo tena, shingo haionekani, mguu mkubwa sana, mashavu .. dah! Aliponitambulisha kwa marafiki zake .. kwanza walikataa kwamba anawatania .. mi nilionekana bado kijana wakati yeye alionekana jimama .... Sikuwa na hamu hata ya kumwambia kuonana naye faragha ... ilibidi ninunue bia nyingi ili nivunge kulewa na kutoroka. Sitaki tena hata kuonana na kiumbe huyo.
KUMBE YA MUNGU MENGI YA SHETANI MACHACHE

Wadada kubadirika sio kupigwa kimaisha ni kujiachia
 
misuli ya wanawake natural ni milegevu wakati ya wanaume ni mikakamavu, ndomana madem wanatebweleka mapema
 
ko alinenepa au sio, shida iko wap hapo!
Kuna kunenepa na kunenepeana akakosa hata mipaka ya viungo vyake vya mwili, shingo kuungana na kichwa na kiwiliwili, kiuno na mgongo kuwa kitu kimoja ,,, haani anakuwa kama mdudu hivi ...
 
Back
Top Bottom