Uchaguzi 2020 Hivi maaskofu wangu mpo au?

kimbendengu

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
6,081
10,390
Tumsifu Yesu Kristu!

Bado siku nne tu taifa hili linaingia kwenye uchaguzi ambao utaamua hatma ya wananchi wake ambao miaka mitano iliyopita walichagua viongozi wao, lakini kutokana na katiba ya nchi mwaka huu na mwezi huu tena wananchi wanakwenda kuchagua tena viongozi kwa awamu nyingine, nakumbuka mwaka huu kanisa la Tanzania katika jumuiya, vigango, na parokia tumefanya chaguzi mbalimbali ili kusukuma gurudumu la kiroho.

Sasa miaka mitano hii yote Maaskofu wangu mumekaa kimya kwa mambo mbalimbali ambayo waumini wenu wanakumbananayo katika maisha yao ya kila siku awamu hii imeshuhudia pale Mkuranga, Kibiti, Rufiji na Mtwara, atu mbalimbali wakiuawa kwa sababu mbalimbali kwa utashi wenu tu kuanzia Jimbo la Mtwara, Jimbo la Tunduru Masasi, Jimbo la Songea, Jimbo la Mbinga, Jimbo la Iringa, Jimbo la Mbeya, Jimbo la Mpanda Jimbo la Mahenge, Jimbo la Moshi, Jimbo la Dar es salaam, Bukoba, Mwanza na Tabora mumeamua kuwasaliti waumini wenu kwa kukaa kimya.

Hivi ni utume upi ambao Yesu aliwafundisha wanafunzi wake? Leo nyinyi Maaskofu kila Dominica mnawataka waumini wachangie fedha za Tegemeza Parokia, Tegemeza Jimbo huku mkielewa kabisa kuwa waumini wenu wamefunga maduka kuanzia pale Kariakoo hadi Majengo pale Mbeya na hali hii imesababishwa na uongozi wa ovyo wa serikali iliyopo madarakani!

Yaani tunawashangaa sana nchi inavyoendeshwa na nyinyi mpo kama akina Yuda ,unajiuliza hivi huyu Ruwaich yupo au amekimbia altare? Hivi Mzee pengo upo au umekimbia mjini?

Mimi kama muumini wenu sina imani na kanisa hili Catholic maaskofu mnachuma dhambi kwa makusudi,na awamu hii mmepunguza sana waumini kwenye makanisa.

Amina
 
Hawa masadukayo na wanafiki hakika wamemdhalilisha Kristo kwa kula karamu na tawala dhalimu inayomkufuru Mungu nao sehemu yao ni lile ziwa la Moto.
 
Maaskofu ni watumishi wa kweli

Kiongozi wa Nchi Rais Magufuli ametenda mambo makubwa na mazuri ndio maana Maaskofu na Mashekh wanamuombea ushindi wa kishindo Rais Magufuli
 
Back
Top Bottom