Hivi LUKU tatizo ni nini?

Hivi LUKU tatizo ni nini?

Juma123

Senior Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
193
Reaction score
47
Jamani wana jamvi, hivi tatizo la LUKU ni nini?

Nilidhani saa kumi hii nitafanikiwa wapi?

Jamani tuepusheni kabla sijaingia kwenye giza.
 
tafuta uzi unaomuhusu simbachawene jukwaa la siasa utaelewa nini tatizo
 
Jamani wana jamvi, hivi tatizola LUKU ni NINI? Nilidhani saa Kumi hii nitafanikiwa wapi? Jamani tuepusheni kabla sijaingia kwenye giza
Tatizo watawala wetu wameigeuza nchi yetu kuwa shamba la bibi.

Kwa hiyo hata hizo tenda za serikalini na kwenye mashirika ya Umma, ambazo wanapewa 'washirika' wa watawala wetu, zote zimejaa harufu ya ufisadi.

Mbaya zaidi Waziri Simbachawene ameishia tu kusema kuwa wanavunja mkataba na hiyo kampuni ya Selcom, badala ya kutwambia kuwa anawaburuza mahakamani 'wahalifu' hao kutokana na 'wizi' mkubwa waliotufanyia watanzania.
 
NMB mobile/ATM peke yake ndio haina longolongo. nenda ukanunue umeme kama una akaunt huko. kwingine ni majanga tu
 
Ni mojawapo ya mashirika kongwe linaloendelea kupumua, ni shirika linalojulikana hata kwa watoto wadogo.

Lakini limekuwa kichefuchefu na headache kubwa kwa taifa na wananchi kwa ujumla, kila mahali kila kona ni malalamiko juu ya Tanesco, kama sio kwenye kununua umeme, basi ni kupoteza pesa kwenye luku, kama sio huko basi ni matatizo ya low voltage, kukatikatika kwa umeme, umeme kuongezeka na kupungua ghafla, kufungiwa umeme, kuripoti dharura, hakuna penye afadhali.

Huwezi kwenda tanesco ukatoka kwa furaha ni shirika lililojajaa madudu kwa kiwango chake, lakini hii yote inasabibishwa kwakuwa hatuna mbadala wa nishati na mbadala uliopo ni ghali umeme wa sola na jenereta.

Miaka ya nyuma tuliteseka sana na mashirika ya simu, TTCL, bima NIC, na DAWASA/DAWASCO, Hizi huduma zilikuwa kizungumkuti hasa lakini baadae kukawa na mibadala siku hizi tuna makampuni mengi tu ya bima na simu hakuna kuringa tena, upande wa maji tuna mbadala wa visima japo hili bado halijakaa sawa sana lakini kuna nafuu

Sasa ni zamu ya Tanesco, hili shirika limezidiwa linahitaji mshindani/ washindani nchi inakuwa kwa kasi kuna ongezeko kubwa sana la mahitaji ya nishati hii muhimu, na kwa hali ilivyo Tanesco hawana uwezo wa kulipa nishati ya kutosha hili taifa.

Tunahitaji mbadala/mshirika wa Tanesco sasa.
 
Mie nimebakiza 0.63 Unit nimeanza kununua tangia jana mpaka sasa sijapata,naambiwa huduma ya LUKU haipo kwa sasa,Ndio nataka niende Kituo cha Maxmalipo au Kituo cha Tanesco ninunue.
 
Nimenunua muda huu kwa Mpesa na kupata token baada ya dakika kama tano.Jaribu kwa mpesa.
 
Mbadala ni serikali kulegeza masharti ya uingizaji wa vifaa vya sola kutoka nje. Vipatikane genuine kwa affordable price kila mtanzania.
 
Nimeamka saa tisa usiku, nikaanza kununua umeme hola! Nikaamua kulala, saa mbili nimejaribu kununua kwa M-PESA nimefanikiwa kupata token, so endelea kujaribu
 
hii sasa mang'ana gasalikile kweli,unaamka usiku kwenda kununusa umeme?
 
Mbadala ni serikali kulegeza masharti ya uingizaji wa vifaa vya sola kutoka nje. Vipatikane genuine kwa affordable price kila mtanzania.

Kwa serikali hii ya sasa sijui kama hilo litawezekana
 
Nimenunua muda huu kwa Mpesa na kupata token baada ya dakika kama tano.Jaribu kwa mpesa.

Mbona kama nimesikia kuwa Tanesco imevunja mikataba na makampuni ya tigo, Voda na Airtel?
 
Mie nimebakiza 0.63 Unit nimeanza kununua tangia jana mpaka sasa sijapata,naambiwa huduma ya LUKU haipo kwa sasa,Ndio nataka niende Kituo cha Maxmalipo au Kituo cha Tanesco ninunue.

Tigo jana walituma msg kuwa kuna tatizo la kiufundi na hivyo umeme hauwezi kununulika
 
Mbona kama nimesikia kuwa Tanesco imevunja mikataba na makampuni ya tigo, Voda na Airtel?

Kiongozi, hili tatizo ni kubwa kuliko unavyofikiria. Ni hivi, Tigo, Vodacom, Airtel na mabenki hawana connection direct na system ya Luku. Selcom ndio mwenye connection direct na server za Luku Tanesco. Hivyo hizo kampuni za simu na mabenki wanawauzia wateja wao wa Luku kupitia connection ya Selcom. Selcom anatumika kama gateway. Hivyo kitendo cha Waziri Simbachewene kuagiza Tanesco kuvunja mkataba na Selcom si kwamba kinamuathiri Selcom peke yake bali na mabenki na makampuni ya simu kwa ujumla. Na mbaya zaidi asilimia 80 ya watoa huduma wa Luku walikuwa wanapitia Selcom ndio maana hadi sasa ununuzi wa Luku umeathirika kwa kiasi kikubwa.
 
Mkuu nashukuru kwa hii clarification! Ila Tanesco jana walisambaza message wakishauri wateja wanunue umeme katika vituo vya Tanesco, CRDB, NMB, AKIBA na MAXMALIPO. Hawa watakuwa wameunganishwa na Tanesco moja kwa moja?!
 
Mkuu, vituo vya Tanesco havipitii popote kwa sababu wao Tanesco ndio wanamanage system ya Luku hivyo vipo connected moja kwa moja kwe server za luku. MaxMalipo ni gateway kama ilivyo Selcom. Sina uhakika kwa CRDB na NMB ila Akiba wanapitia MaxMalipo. Kujua zaidi idadi ya wanaopitia Selcom soma hii post yenye nyaraka za Tanesco, Selcom na TRA kuhusu hii scandel ya Luku.

[h=2]Kufungiwa SELCOM: Simbachawene amekurupuka? JamiiForums ilikuwa na taarifa kabla ya mwekezaji![/h]
 
Mkuu, vituo vya Tanesco havipitii popote kwa sababu wao Tanesco ndio wanamanage system ya Luku hivyo vipo connected moja kwa moja kwe server za luku. MaxMalipo ni gateway kama ilivyo Selcom. Sina uhakika kwa CRDB na NMB ila Akiba wanapitia MaxMalipo. Kujua zaidi idadi ya wanaopitia Selcom soma hii post yenye nyaraka za Tanesco, Selcom na TRA kuhusu hii scandel ya Luku.

Kufungiwa SELCOM: Simbachawene amekurupuka? JamiiForums ilikuwa na taarifa kabla ya mwekezaji!

Mkuu nashukuru.....naisoma sasa hivi!
 
Back
Top Bottom