Tusikatae ukweli kwamba darasani alikuwa vizuri hususani kwenye economics. Na hata kwenye research za world bank kuhusu Development economics na agriculture amezifanya sana na ni mtaalam sana kwenye development economics na agriculture. Nilibahatika kuona dissertation title yake ya master enzi zile akiwa UDSM.
Ila kwenye kufundisha kwa sasa hatakuwa active sana maana tangu aingie kwenye siasa nadhani hajawahi kuwa full time teacher wa chuo particularly hapa ndani ila naskia kuna washkaji walikuwa mbale yangu pale UDSM wanasema alifundisha kama topic moja kwenye Development economics.
Mara ya mwisho kumuona Lipumba akichambua uchumi publicly ilikuwa pale Nkrumah hall i think ilikuwa kati ya 2011 au 2012 ila sikumbuki vizuri ilikuwa kwenye Kigoda cha mwalimu na prof. Tibaijuka alikuwepo. Alitoa lecture nzuri kwa mtazamo wangu na kiasi nilimuelewa Lipumba ni mtu wa aina gani kwenye uchumi. A lot of facts na how mechanism zinatokea na kuhathiri economic variables, kitu ambacho wanauchumi wengi wanashindwa kukielezea.
Siku hiyo nakumbuka aligusia kuhusu commodity price change katika soko la dunia, kuna mahali alihusianisha na kuelezea bei ya mchele inavopanda na kushuka mpaka nikampigia saluti.
Kwa ufupi jamaa yupo vizuri sana, na najisikia sana vibaya mtu wa kariba yake anajiaibisha na kufanya folks wamshushe heshima. He is a very very great man and smart na anastahili heshima kubwa sana, sio mtu wa kustahili kutukanwa tukanwa hovyo. Sad