chameleon
JF-Expert Member
- Dec 4, 2013
- 555
- 170
Habari wakuu...nimekuwa nikijiuliza hivi hawa watu weupe hivi huwa wanaongozwa na nini mpaka kufikia hatua ya kutushusha thamani watu weusi..ukiangalia hata dini walizotuletea zinahubiri usawa na upendo..inakuwaje wao tena wavigeuke vitabu vyao walivyotuaminisha kuwa ni maneno ya MUNGU..tena mwenye upendo na huruma..au walituletea hizi dini hili kutupumbaza ?..kama vitabu vyao vya dini vinahubiri usawa na upendo kwa viumbe wote...iweje wao watubague sisi weusi?
Mimi naamini watu weupe hawatubagui sisi weusi bali ni hofu tulizonazo
*Wakati sisi tunajikoboa weusi wetu wao weupe ni rangi yao
*Sisi tunachangishana harusi za kifahari wao wanafikiri kupunguza gharama
*Sisi tunatumia mda mwingi kushangaa Video na Tv wao wanachukua muda mwingi kusoma na kufikiri
*Sisi tunabeba simu kubwa kuchati na Face Book wao wana download matereal
*Sisi tunasoma ili tufanane na wao, wao wanasoma ili wavumbue zaidi
*Sisi ni walalamishi ,wavivu na hatujui haki zetu wao wanapigania haki zao na ni wachapa kazi
NB Sisi pia tunabaguana kwa siasa kv UKAWA vs CCM, Ukabila,
-Kielimu wengine wanapewa mikopo wengine hawapati
-watawala wanalipana posho ya Sh 300,000 kwa siku na kujigamba kua wameongeza sana mshahara KCC Sh 180,000 kwa mwezi au Sh 3,000 kwa siku
Tuwe wakweli