Hivi Kwanini Watu Hukamatwa Wakati Upelelezi Haujakamilika?

Suala la kukamatwa na kupelekwa rumande haliwiani na suala la upelelezi,bali hutokeA pale wanapohisi umetenda jambo ambalo ni kinyume cha sheria....Ila suala la kupelekwa mahakamani ndo linategemea kukamilika kwa upelelezi wa kosa husika
 
Wengine wakibaki uraiani wakati wa Upelelezi wanaweza kuharibu upelelezi au wengine wanaweza kudhuriwa na Wabaya wao kuficha au kuharibu Upelelezi !

Wengine wanaendelea na Makosa Mengine ya namna ile ile
Kwa nini wanapewa dhamana na upelelezi ukiwa unaendelea? hapo kuna tatizo aise
 
Huwa ninajiuliza ni kwanini watu huswekwa rumande kwa muda mrefu sana, lakini wakipelekwa mahakamani Jamhuri huomba kesi kuahirishwa ili kukamilisha upelelezi. Kwanini wasikamate watuhumiwa baada ya kukamilisha upelelezi?
Ni matatizo ya utawala usio wa kisheria ingawa watawala wanasema vingine. Na pia uwapo Wa sheria za udhalilishaji za tangu enzi ya mkoroni na hazijaondolewa kwenye vitabu. Hapa Canada Na Marekani Na Nyingine zilizoendelea polisi hawezi kukumata na kukufungulia kesi kabla hajakamilisha uchunguzi. Police wa Canada akiongea upuuzi huu mbele Ya jaji eti uchunguzi haujakamilika anatolewa nduki na jaji, na uliyewekwa ndani bila wao polisi kukamilisha unaweza kuishitaki polisi na kudai fidia. Bongo bado tuko nyuma ndugu zangu
 
Kwa nini wanapewa dhamana na upelelezi ukiwa unaendelea? hapo kuna tatizo aise

Hiyo ipo Dunia Nzima, kabla ya kupewa dhamana Mwendesha Mashtaka huwa anaulizwa Kama kuwepo kwa Mtuhumiwa Nje Kama kunaweza kuathiri upepelelezi!
 
Ni matatizo ya utawala usio wa kisheria ingawa watawala wanasema vingine. Na pia uwapo Wa sheria za udhalilishaji za tangu enzi ya mkoroni na hazijaondolewa kwenye vitabu. Hapa Canada Na Marekani Na Nyingine zilizoendelea polisi hawezi kukumata na kukufungulia kesi kabla hajakamilisha uchunguzi. Police wa Canada akiongea upuuzi huu mbele Ya jaji eti uchunguzi haujakamilika anatolewa nduki na jaji, na uliyewekwa ndani bila wao polisi kukamilisha unaweza kuishitaki polisi na kudai fidia. Bongo bado tuko nyuma ndugu zangu
Acha uongo wewe watuhumiwa wa ugaidi wako waliokaa miaka bila kufunguliwa mashtaka marekani kisa uchunguzi unaendelea baadaye wakaachiwa bila kufunguliwa mashtaka kuwa hawajapata ushahidi wa kutosha . Acha uongo
 
Fafanua basi ndugu ili ueleweke vizuri. Mimi Nilikuwa naongelea kesi kawaida za kijinai na kwa jinsi nilivomuelewa mtoa. Tusaidie basi kutoa mfano japo mmoja wa hizo kesi za kigaidi. Kama unaongelea Guantanamo ile ni ishu tofauti kabisa. Ndani ya Marekani huwezi wekwa ndani bila uchunguzi haujakamilika, uwe gaidi au mhalifu yoyote. Unaweza kuwa ndani kwa kushindwa masharti ya dhamana au jaji kakunyima dhamana kwa sababu kadha wa kadha.
 
Acha uongo reference 9/11 jengo la world trade center lilipobomolewa na kamata kamata bila kufunguliwa mashtaka ilivyofuata watu walishikwa kama kuku na hawakufunguliwa mashtaka chap chap. Mwongo wewe.
 
Ndugu kwa heshima na taadhima Nadhani nitaishia hapa ktk huu mjadala. Inawezekana Kweli hayo unayosema yalitokea ukizangatia ugumu Na unyeti Wa hayo matukio , lakini kwa ujumla Marekani hakuna kamatakamata hiyo unayoisema ya kuweka watu ndani eti kwa kisingizio uchunguzi haujakamilika. Ni hilo tu Mkuu. Have a nice day
 
Sijawahi kufika huko dunia ya kwanza, lakini siamini kama bado wanafanya kama huku kwetu.
Sssa we angali kesi ya lema Arusha. Kesi inadhaminika lakini wanamnyima dhamana, halafu wanadai inchi inaendeshwa kwa utawala wa kisheria.
 
Back
Top Bottom