Hivi kwanini Watanzania wengi wanapenda kupiga simu kuliko kutuma meseji?

Buzi Nene

Senior Member
Feb 10, 2020
142
310
Wadau naomba kuuliza,

Mimi kwa kweli sipendi kabisa kupigiwa simu, hasa simu ambazo hazina ishu serious. Yaani unakuta mtu anakupigia simu hata mara tano, ukipokea anakwambia nilitaka kukusalimia tu, huwa najiuliza kwanini usitumie tu text mpaka upige simu?

Sababu ni nini haswa au kiwango cha elimu pia kisaendana na hii tabia?
 
Message huacha ushaidi mkuu, bora tuongee kama nikikujibu vibaya au nikimsema mtu fulani au nikakutusi hakuna ushaidi instantly.

Ila kupiga simu mpaka ufuate protocol ya police, mahakamani (affidavit) na TCRA ndio usikilize nikichokwambia endapo huna ujanja wa kurekodi mazungumzo wakati mnaanza kuongea.
 
Hiyo nakubaliana na wewe,mimi shida yangu kubwa ni zile simu za salamu tu
 

Saa nyingine mtu anakua hayuko kwenye position ya kujibu kwa text mathalani mtu anaendesha gari ni rahisi kuitafuta namba yako mara moja na kuipiga kuliko kuanza kudonyoa herufi moja moja kwenye keyboard kukuandikia text
 
Swali kwa kichwa cha habari;
Umelinganisha na nchi zipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…