Hivi kwanini wanawake ni waoga kuliko wanaume?

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
Habari za mapumziko wanajamvi?

Kuna hili suala nimekuwa najiuliza kwa muda mrefu, kwamba ni kwanini wanawake ni waoga sana kuliko wanaume.

Kwa mfano ukichukulia labda ametokea mnyama mkali kama simba, wanawake ni likely kuogopa kiasi hata cha kuzimia.

Wengine tuu hata akimuona mende anatetemeka balaa. Kukiwa na giza, anayeogopa zaidi ni mwanamke kuliko mwanaume.

Kwa mfano akitokea mwizi nyumbani mwanamke ni rahisi kutoa siri za pesa zilipo kuliko urahisi kwa mwanaume.

Tuchukulie pia mpo kwenye gari, ghafla gari ikaanza kuyumba, utasikia wanawake wengine wanasema ; 'Yesu wangu' , au 'Damu ya Yesu' au 'mtumee'

Wakuu kwanini iko hivi?

Naomba tuliangalie hili, kumbuka sijaandika kuwa-offend wanawake bali kutaka kupata just uzoefu kutoka kwenu na kujifunza.

Karibuni.
 
Mada yako iko vizuri ila mifano sio relevant kabisa... uoga wa SIMBA na MENDE? Seriously
 
Nakumbuka siku tuko class mara mende huyoooo kakatiza(nahisi kuna denti alikuja nae toka home)..Teacher alipiga kelele hatari...Lile pindi ilibidi lihairishwe..Tulimpongeza sana yule mende
 
Maumbile tu,japo kuna wanaume waoga wanawake hatufui dafu.
 
kwa sababu ndio wanabeba uhai wa mwanzo wa binadamu matumboni mwao.ndio maana unaona hata kwenye misiba huwa kina mama wanafungwa kanga kwa kukazwa tumboni au aone ajali mbaya utaona anashika tumbo.
 
Hizi mada za aina hii nazichukia saaana,. Hivi wewe unataka tuwe sawa kwa kila jambo? We ni mwanaume bhana mlinde mke, na mke hufarijika anapoona anapata ulinzi wa mwanaume, Mungu ndo katuumba hivyo. Utasikia mwanaume kabisa akipenda "hivi kwann wanawake wanapenda kudeka na kubembelezwa," sasa unataka nawe udeke na kubembelezwa kama mwanamke, kwann unahangaika kufanana na mwanamke? Ndg jiangalie saaana msije mkajiuliza hivi kwann wanawake wana matako Makubwa, je nawe ungependa Kuwa nayo? Akiogopa simba we shika mkuki kaue, Akiogopa mende, nenda kaue hapo mwanamke ndio faraja yake kuona mume yuko kwa ajili ya ulinzi wake. Kaka mbona hujauliza wanaume wa Dar walipokimbia panya Road hawakukimbia na wake zao? Au hao wa Dar sio wanaume?
 
Asante kwa maoni yako japo hujajibu swali. Kama ni pepa ungelamba mswaki!
 
Back
Top Bottom