Hivi kwanini Star Times mnakua wahuni kiasi hiki?

hawajajipanga kabisa inabid tcra wajaribu kulifuatilaa tena kwa umakini zaid bila hvyo tv ni mateso tupu mara no service mara no signal wakati tumelipia 18000

yaani hadi wanaudhi. wanafanya biashara kihuni. mia
 
Startimes ni hovyo sana kwa upande Wa customer care! Nimekinunua kingamuzi siku tano zilizopita nikapiga simu customer care ili kisajiliwe wakanijibu nimeshakisajili! Nikaja home nikaunganisha, kila nikizungusha mnara sipati kitu! Nimecheza na signal mpaka nikachoka' maana nikipiga simu wanajibu natakiwa nipate signal 65%. namimi nilikua napata 50%. Ikabidi nikirudishe niliponunua wakaniambia labda hakijasajiliwa! Waliposajili tu kikaonyesha! Sasa kwanini hawa customer care walikukua wananidanganya kingamuzi kimesajiliwa? Maana niliwauliza zaidi ya Mara 5 kumbe wananimalizia vocha tu!
 
Mi niliwafata wakaniambia ninunue antena yao nikafanya hivyo ikawa chenga bado nikawapigia wakaniambia nigeuze antena kisarawe aijasaidia nikajaribu kugeuza na kin'gamuzi chenyewe kisarawe chenga mtindo mmoja leo naenda kujaribu kugeuza na TV yenyewe huko kisarawe nione,
 
Kwahiyo ili usisumbuke kabisa na chaneli ukitumia Startmz mliofanikiwa mmewezaje wenzetu ama ambao mnaenjoy kupitia huko
 
Mi niliwafata wakaniambia ninunue antena yao nikafanya hivyo ikawa chenga bado nikawapigia wakaniambia nigeuze antena kisarawe aijasaidia nikajaribu kugeuza na kin'gamuzi chenyewe kisarawe chenga mtindo mmoja leo naenda kujaribu kugeuza na TV yenyewe huko kisarawe nione,

Mkuu mandemba umetisha,kikigoma tena nadhani utabeba vitu vyako na kuamia Kisarawe kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Nenda dstv, kiboko yao!

mkuu kule hadi uwe na hela ndefu. sasa watu wengine hela ya kula tabu itakuaje hela ya king'amuzi?. Tanzania ilikua haijajipanga. paul hagame alikataa akasema hajajipanga hadi 2015 lakini tanzania tunataka kuvunja record ya kuwafurahisha na kuwanemesha wakoloni. mia
 
Mi niliwafata wakaniambia ninunue antena yao nikafanya hivyo ikawa chenga bado nikawapigia wakaniambia nigeuze antena kisarawe aijasaidia nikajaribu kugeuza na kin'gamuzi chenyewe kisarawe chenga mtindo mmoja leo naenda kujaribu kugeuza na TV yenyewe huko kisarawe nione,

dalili ninazoziona kuna uwezekano tukaambiwa tuhamie kisarawe ili kusogelea mitambo yao,heri yao waishio huko hawana dhahama hili.
 
Easy tv ndo mpango mzima sasa hivi
1/Hawa jamaa wa Easy Tv wanafika mikoa ipi mbali na Dar?

2/Nini ubora wao katika matangazo(Mawimbi, sauti, picha, channel)?

3/Gharama zao za ving'amuzi, Installation, monthly payment nk zikoje?

3/Wana nini cha tofauti kulinganisha na provider wengine?

4/Wana free channels?

5/Wana local channels zipi? Are those free?
 
Wiki iloisha nlienda kununua king'amuzi 50,000. Nikaambiwa ntakuta channel 30, cha ajabu nafika home home nakuta channel 15. kuwapigia wakanambia nunua antena. nikanunua antena 20,000 lakini ikawa vilevile. kuwauliza wakasema nimelipia 9000 so nilipie 18000 ili nione zote 30. kuwabana maswali wakanambia "nimechukua king'amuzi cha kukodi yaani wamenikodisha kwa dhamana ya 39000 kwa mwaka so hadi local channels inabidi niwe nalipia" nikashangaa!. so jana sikuona mpira. ntanunua kingine. mia
uwo sasa ni wizi wa mchana kabisa
 
dalili ninazoziona kuna uwezekano tukaambiwa tuhamie kisarawe ili kusogelea mitambo yao,heri yao waishio huko hawana dhahama hili.
kwani nyumba za kuishi kisarawe sh.ngapi? dalili zinaanza kuonekana mapema.ipo siku tutaambiwa ukitana kuona bila chenga nenda kisarawe
 
mkuu kule hadi uwe na hela ndefu. sasa watu wengine hela ya kula tabu itakuaje hela ya king'amuzi?. Tanzania ilikua haijajipanga. paul hagame alikataa akasema hajajipanga hadi 2015 lakini tanzania tunataka kuvunja record ya kuwafurahisha na kuwanemesha wakoloni. mia
ili tupate msaada wa chandarua kutoka marekani
 
Mi niliwafata wakaniambia ninunue antena yao nikafanya hivyo ikawa chenga bado nikawapigia wakaniambia nigeuze antena kisarawe aijasaidia nikajaribu kugeuza na kin'gamuzi chenyewe kisarawe chenga mtindo mmoja leo naenda kujaribu kugeuza na TV yenyewe huko kisarawe nione,
bora kuamia mikoani,uku songea bado hayo mambo hayajaingia,uondo tu mtindo mmoja
 
kwani nyumba za kuishi kisarawe sh.ngapi? dalili zinaanza kuonekana mapema.ipo siku tutaambiwa ukitana kuona bila chenga nenda kisarawe

ngoja nilifanyie kazi hili la bei za kupanga lazima zitakuwa zimepanda sana sababu kisarawe hata gesi ya mtwara ndiyo inakopelekwa ndugu sijui nayenyewe inasogezwa kwenye mitambo ya digital!
 
DIGITEK nimesikia bei yake ni laki na sitini na hakuna malipo mengine tena ila sijajua kwa mwaka au ndio forever bwana Nyingi anahasira sana....
 
Back
Top Bottom