Hivi kwanini Mwl. Nyerere hakupewa PhD?

KOMBAJR

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2011
Posts
5,827
Reaction score
1,276
Wanabaodi Heshima kwenu, Kuna jambo limekuwa likinitatizo, katika kipindi cha karibuni tumeona tumesikia karibu zaidi ya vyuo vyetu ambapa nchini kutoa Phd za Heshima kwa viongozi ambali mbali ambayo imepeleka mpaka Kiongozi wa Nchi yaani Rahisi kutunukiwa Phd za Heshima zaidi ya Nne kama sikosei mwenye data sahahii atarekebisha! Maswali ambayo nimekuwa nikijiuliza kitu ambacho nahisi kunawengi pia ambao wanamaswali kama yangu ni haya yafuatayo:
  1. Hivi Sifa na Sababu hasa kupewa Phd ni nini au ni zipi?
  2. Hivi Kwa kazi aliyolifanyia Mwl.Nyerere kwa hili Taifa hakustahili Kupewa Phd au alipewa akakaata?
  3. Je Hizo PHD zina tija kwa taifa?
Ni hayo tu

Nawatakia Bajeti Njema.

====

Vatican - Mwenye heri na mtakatifu
 
Mwalimu J.K. Nyerere alipewa PhD za heshima (Honoris Causa) na vyuo vikuu vingi tu kutoka Africa, Marekani na hapa Tanzania. Inawezekana wewe tu ndo huna hizo kumbukumbu. Lakini kwa taarifa yako, Chuo Kikuu cha Dar es salaam, kilimtunuku uprofesa wa historia, kwa hiyo alikuwa ni title ya Professor katika chuo kikuu cha DSM.
 
Kwa kumbukumbu zangu ni kwamba mpaka anafariki alikuwa na PhD za heshima 14 kutoka katika vyuo mbali mbali barani Afrika, Ulaya na U.S vikiwemo chuo kikuu cha Oxford na Cambridge vya Uingereza, ila yeye kwa kutokujikweza kwake aliamua kuitwa Mwalimu, na hiyo ndo inamtofautisha na hao wengine
 
Inamaana hakupena sifa kama huju JK WA ukware.
 
ALIKUWA NAZO 26... hakuona sababu ya kujiita Dr. Kwa sababu kama alikuwa na nia ya kuipata kwa kukaa Darasani angeipata. Tatizo linakuja kwa hawa hata first degree aliipata kwa mazabwe. anatamani kuwa Dr ila kwa kukaa darasani haiwezakani. Akipatiwa hiyo ya heshima Lazima anganganie kuitwa Dr
 
Inamaana hakupena sifa kama huju JK WA ukware.

watu wengi hawajui matumizi ya degree za heshima. huruhusiwi kuandika jina lako likianzia mfano: DR.J.Nyerere, inapaswa itamkwe tu na si vinginevyo.
 
KOMBAJR.

Inawezekana umri wako mdogo wakati wa Nyerere ulikuwa mdogo, University of Kankan Guinea walipa PhD.

Tafuta makala ya muandishi wa zamani wa BBC James Robbis, alikuwa akimuandika Dr Julius Nyerere.
 
Last edited by a moderator:
KOMBAJR.

Inawezekana umri wako mdogo wakati wa Nyerere ulikuwa mdogo, University of Kankan Guinea walipa PhD.

Tafuta makala ya muandishi wa zamani wa BBC James Robbis, alikuwa akimuandika Dr Julius Nyerere.

Are you trying to justify calling JK DR or what ?
Kila mtanzania leo ukisema Dr.Nyerere watadhani ni mtu mpya maana hawakuwahi kuzoea ujinga huu .Yeye ukisema Mwalimu basi hata nani anamjua .
 
Are you trying to justify calling JK DR or what ?
Kila mtanzania leo ukisema Dr.Nyerere watadhani ni mtu mpya maana hawakuwahi kuzoea ujinga huu .Yeye ukisema Mwalimu basi hata nani anamjua .

Hapo vipi Rtd Lt. Jakaya M. Kikwete
 
KOMBAJR.

Inawezekana umri wako mdogo wakati wa Nyerere ulikuwa mdogo, University of Kankan Guinea walipa PhD.

Tafuta makala ya muandishi wa zamani wa BBC James Robbis, alikuwa akimuandika Dr Julius Nyerere.

Zingatia msingi wa Swali Kikongwe!
 
Hizi Degree za Heshima hutokana na mchango fulani ukatambuliwa na watu fulani then wakakutunuku hio heshima,
 
Nimeipenda.
Are you trying to justify calling JK DR or what ?
Kila mtanzania leo ukisema Dr.Nyerere watadhani ni mtu mpya maana hawakuwahi kuzoea ujinga huu .Yeye ukisema Mwalimu basi hata nani anamjua .
 
Mwalimu Nyerere alikuwa mtu wa kujishusha na alipenda kuitwa mwalimu na si vinginevyo,though alikuwa na Phd za heshima zaidi ya kumi.Hii na iwe fundisho kwa viongozi wetu,ambao wengine wanapewa phd za heshma zenye utata ili wajiite dr fulani.
 
Are you trying to justify calling JK DR or what ?
Kila mtanzania leo ukisema Dr.Nyerere watadhani ni mtu mpya maana hawakuwahi kuzoea ujinga huu .Yeye ukisema Mwalimu basi hata nani anamjua .

Wewe wakati wa Nyerere haukuwepo wewe kipindi chako cha siasa ni wakati wa JK, ndio maana wakongwe wamekaa kimya takuwekea makala ambazo Nyerere alikuwa anaitwa Dr wakati wewe bado ujazaliwa.
 
yeye si amepewa Dk yaani Dictator

Hili ndilo tatizo la kujichanganya na kila aina ya mtu. Unajua mtaani huwa tunajifanya mimi sijichanganyi na kundi fulani la watu kwa sababu tuna sababu za haki kufanya hivyo.

Ukikuta wanywa kahawa unaweza kusema hilo si genge lako unaenda kwa wanywa wine na whisky na huko mazungumzo yanaendana.

Hata majumbani tukitembeleana hali ni hivyohivyo. Eti mgeni akija tunafukuza watoto waende kucheza kwa kigezo kwamba mazungumzo hayawafai au hawataelewa au wataharibu mazungumzo.

Sasa mitandao imetuletea balaa tulilolikwepa kwa miaka mingi. Yule mtoto tunayemfukuza nyumbani kwamba hataelewa au kuvuruga mazungumzo sasa ndiye yuleyule anyekuja kwenye mitandao bila jina halisi.

Yule mnywa kahawa uliyekwepa genge lake ukakimbilia Yatch Club kwa wenzako sasa mnakutana kwenye mitandao bila yeye kujua na bila wewe kujua.

Kama ulikuwa unakwepa au unawanyanyapaa wasukuma mikokoteni kwamba huwezi kujadili nao eti si saizi yako, sasa wanajua ku-type keyboard na unakutana nao kwenye mitandao bila kujua unajadili na msukma mikokoteni.

Angalia nature ya swali hili. Ni wazi aliyeliuliza ingekuwa ni kwenye seating room au Yatch club sidhani kama kuna mtu angemjibu huyu na sanasana wangeishia kumkemea kwa maswali ambayo hayana kichwa wala miguu.

Mimi ni mzuri sana kukwepa makundi. Lakini kwenye mitandao sina jinsi maana ni ukweli ninayemkwepa mtaani ndiye siajabu ni yuleyule anayekuja kwenye mitandao bila ID.

Hivyo maswali mengine tunatakiwa tu kuyavumilia japo ukweli ni kwamba ni pumba.
 
Swali hili sio pumba kama unavyodhani. Ni swali la msingi sana. Linatoa uelewa wa mtu binafsi, hulka yake na jamii imwelewe. Mtu kiongozi wa watu lazima watu wake wamwelewe kwa undani, vitu anavyopenda, anavyochukia na umakini wake ili waweze kuishi naye vizuri. Mfano kwa maelezo ya hapo juu utajua nani kati ya viongozi hawa anapenda vya bure (simple popularity) nani anajikweza na kwa nini anajikweza. Hivyo huwezi kutegemea kupata makuu kwa mtu mvivu. Kwa mchapa kazi kupewa kitu asichokitolea jasho ni aibu kwa mvivu ni neema inayopaswa kukumbatiwa tena pasipo hata shukrani. Utasema ni pumba?
 
Fanya Research kabla ya kuweka Hoja Wajameni Dah; Nyerere alipewa Ph.D na alikuwa anaitwa Dr. Mara nyingi tu Most of the time alipokuwa South South Commission
 
Off point note: Nimesikia siku hizi wanatoa "O levels" za heshima, is it?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…