Mzee_londo
Member
- Dec 5, 2018
- 46
- 99
Nimepokea ujumbe ufuatao kutoka whatsapp na umenifungua akili sasa ni kwanini serikali kupitia BOT Au Waziri husika wapo kimya
Ujumbe wenyewe
“Habari Mtanzania mwenzangu,
Leo nataka nikutahadharishe na utapeli kuhusu biashara haramu ya Sarafu za kidigitali (cryptocurrencies) ambazo zipo aina nyingi na zifuatazo ni chache tu;
1. Bitcoin
2. Lite coin
3. Ethereum
Nadhani katika majukumu yako ya kila siku ushawahi kukutana na wakaka watanashati au wadada warembo wakakuomba muda wako ili waweze kukushirikisha kukuelezea fursa ya biashara na ukatenga muda wako, kilichofuata ni kushawishiwa kufungua akaunti aidha ya dola za kimarekani 10000$, 5000$, 2000$ au 500$ baada ya maelezo mareefu ya kukushawishi huku ukiahidiwa faida kubwa zenye marejesho kilasiku. Kama bado basi utakutana nao hivi karibuni.
Ndugu zangu huu ni utapeli tena unaenea kwa kasi kama ilivyokuwa DESI au D9, epuka kutapeliwa waingereza wanasema “there is no easy money”. Huu ni utapeli kwasababu zifuatazo:
1. Umiliki wa hizi sarafu za kidigitali, ili kitu chochote kiitwe pesa lazima kiwe na mmliki lakini pesa hizi mmiliki wake hawafahamiki mpaka sasa. Hapa kuna wasiwasi kupotea katika soko bila kujua nini kimetokea ni kama kuteleza tu!
2. Ustahamilivu katika soko, pesa hizi zimekuwa zikipanda thamani kila kukicha na kushuka. Kupanda kwake thamani huwa maradufu hii inaleta wasiwasi kwamba siku zitakuja kushuka vibaya sana.
3. Serikali kupitia benki kuu haitambui hizi sarafu na nimatumaini yangu muda si mrefu watatoa tamko rasmi.
4. Hakuna sheria inayosimamia hii biashara ukitapeliwa huna pa kuanzia
5. Upatu, hii ikimaanisha hakuna kinachofanyika zaidi ya wale waliojiunga kukopeshana wenyewe. Ukijiunga leo unasaini mkataba wa mwaka mmoja ndo uchukue pesa yako.
6. Utakatishaji pesa na ukwepaji kodi, watu wanatumia hii biashara kutakatisha pesa na pia faida inayopatikana kutokana Na hii biashara haikatwi kodi. Epuka kuanguka kwenye mikono ya TAKUKURU
7. Kampuni zinazojihusisha Na hii biashara hapa Tanzania zimekuwa zikibadilisha majina kila mwaka hii sio dalili nzuri
Mwisho nasikitika kwamba watanzania wenzangu takribani 6800 wameweza kuingizwa katika utapeli huu.
Nakutakia kazi njema”
Toa maoni yako