Hivi kwani yakitengenezwa mabango machache tu ya kumkaribisha Rais kuna shida gani?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,579
44,826
Viongozi wa Serikali wa mikoa na wilaya ingefaa sana muwe mnapunguza gharama hata kwenye banner na flyer maana sasa inakuwa ni kama taasisi zinashindana yaani barabara zote za mjini au wilayani nguzo zote zimebandikwa picha ya Mh. Rais.

Tarura watoe za kwao mara nhcf tanesco wawekwe za kwao duh..kwanini bango lisiwe kubwa moja ambalo limechorwa fursa za mkoa husika na zinapopatikana kuliko hii ya karibu Mh. Rais kila sehemu kwa sababu lengo akaribishwe sasa sidhan kama akiwa ndani ya gari kwenye msafara anapata hata muda wa kuyasoma ma posters ya karibu Mh. Rais karibu Mh. Rais.
 
Back
Top Bottom