Kawaida nafikiri madingi huwa hawana muda wa kupoteza na wakwe zao. Mradi unamheshimu yeye hana soo na wewe. Nafikiri akina dada na mama huwa wanatumia muda mwingi na wakwe kwa hiyo wanahitaji mtu atayeelewana nao. Sina experience na kuoa ila nafikiri labda hili linachangia
umenena vyema,nothing more to add!Songíto;2783822 said:Trust me unayekwenda kumuoa ni msichana, hivo wao kama wanawake wapo katika position nzuri zaidi ya kukushauri maana kuna mambo ya kina dada ambao wanaume sio rahisi kujua...thats why wanakushauri wao na sio baba maana wanajijua vizuri jinsi wanawake wanavyokuwa...
Mi nitofautiane na wewe kidogo kaka, ushauri wao ni muhimu sana, hasa mama mkuu!! siku hizi tunadharau sana busara za hawa watu tunapotafuta majiko lakini kiuhalisia wao wanajua mengi sana juu ya maisha...
enzi hizo kabla ya mzazi kukushauri umchumbie binti flani, anakuwa amemfahamu muda mrefu sana may be tangu anazaliwa, anakuwa,anakuwa anafahamu historia ya familia yake kwa mapana na marefu na hivyo anajua in and out juu ya huyo anayekuarifu juu yake... thats why unakuta ndoa za miaka hiyo zinadumu sana na pengine kifo ndo huwatenganisha wanandoa..
Hebu angalia haya mapenzi ya ki.com ya siku hizi... watu wanaoana asubuhi, jioni mwanandoa anafumaniwa au anaachika... tu ni kwa kuwa wakati wa kuoa/kuolewa walitazama sura, urembo, uhandsome bila kujua historia halisi ya mtu anayeolewa nae au anayemwoa.... na hii ndo siri kubwa ya ndoa nyingi za vijana wa siku hizi kuvunjika.... wanaoana wakiwa hawafahamiani hata, hawajuani hata...zamani hii kazi walikuwa wanafanya wazee.. wanachunguza weeeeeee, wewe unawowaaaaaa tuuuuuuuuuuu
Madingi wanatoa ushauri lakini indirectly. Kwa mabinti zao huwa wanawatumia mama zao kufikisha ujumbe. Kwa vijana wa kiume kuna wanaozungumza moja kwa moja, kuna wanaotumia akina mama kwa sababu hata vijana wa kiume huwa wanajisikia comfortable mbele ya mama zao kuliko baba na wengine wanashauri katika mazungumzo ya kawaida bila kuonekana wanalazimisha na mwisho kuna wanaowachagulia wachumba watoto wao moja kwa moja. Siku hizi vijana wakikutana na kukubaliana wanaenda kutambulishana kwa wazazi. Sasa unapomtambulisha mchumba wako unategemea wakae kimya bila kuhoji na kutaka kumfahamu zaidi?Kawaida nafikiri madingi huwa hawana muda wa kupoteza na wakwe zao. Mradi unamheshimu yeye hana soo na wewe. Nafikiri akina dada na mama huwa wanatumia muda mwingi na wakwe kwa hiyo wanahitaji mtu atayeelewana nao. Sina experience na kuoa ila nafikiri labda hili linachangia
Jihesabie una bahati ya kuwa na washauri katika hili; wengi wetu tulienda kichwa kichwa pengine kwa kukosa watu kama ulionao wewe na ndio maana unatuona hapa tukilalalma!