Hivi kwa nini CUF haina gazeti lake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kwa nini CUF haina gazeti lake?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Aug 24, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wiki iliyopita nilimwona katika TV Profesa Lipumba akiwa katika mkutano wa waandishi wa habari na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa ulioitishwa na Idara ya Maelezo kutoa maelekezo namna ya kurpoti habari katika kipindi cha kampeni.

  Akizungumza katika kongamano hilo la siku moja Lipumba, pamoja na mambo mengine, alisisitiza umuhimu kwa vyombo vya habari kufuata maadili na kuandika yaliyo ya kweli, bila upendeleo na ushabiki wa kisiasa.

  Tatizo langu na hawa CUF ni kwamba ni zaidi ya miaka 18 sasa tangu chama kingie mambo ya siasa, inakuwaje hakina hata gazeti lake, achilia mbali radio au TV? Mpaka lini chama hichi kitategemea huruma ya vyombo vya habari binafsi (na vya serikali) kuandika habari ya chama hicho bila upendeleo?

  Si dhani kama ni tatizo la pesa kwani CUF imekuwa inapata mamilioni ya fedha kila mwezi kama ruzuku lakini hawakuwa na mpango wowote wa kuanzisha angalau hata gazeti – au hata mmoja wa viongozi wake wenye fedha kufanya hivyo.

  Kuanzisha gazeti hakuhitaji fedha nyingi sana – Kubenea, mwaka 2006 aliweza kuanzisha gazeti lake na sasa linauza nakala nyingi kila toleo kupita magazeti yote hapa nchini kuachilia yale ya udaku.

  Chadema wana gazeti lao – Tanzania Daima – ingawa inaejulikana kama ni la Freeman Mbowe, mwenyekiti wa chama hicho.

  Lakini kama tunavyoona sasa hivi, gazeti hilo linakisaidia chama hicho kutokana na propaganda za vyombo vya habari vya serikali na chama tawala pamoja na vile vinavoonekana kununuliwa na chama tawala. Na hivi sasa nasikia linauzwa kama njugu – bila shaka kutokana na kuandika ukweli kuhusu matukio mbali.

  CUF ina viongozi wasomi, na waliobobea katika masuala ya siasa na kufanya publicity. Vipi kasoro yao hii hawaioni? Profesa, Maalim, hamad Rashid na Jussa – hela mnapeleka wapi? Msikae kulalamika tu – kuweni na chombo chenu.
   
 2. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  Al-Nuur linatoka kila Ijumaa
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ni kweli, An Nur huandika habari nyingi kukitetea chama hicho na ndo maana kinaitwa chama cha Kiisilamu. Lakini wangekuwa na gazeti lao, nembo ya Uisilamu wangeweza kuikwepa.

  Lakini mimi naona viongozi wakuu wa CUF wanatafuna tu fedha za ruzuku na ndo maana hao hao wameng'ang'ania madarakani miaka nenda miaka rudi.
   
 4. D

  Dick JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hawana gazeti rasmi la chama, hilo linawapigia debe tu. Ni uvivu wa kufikiri.
   
 5. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Al-Nuur ndo gazeti lao
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Halafu utasikia baadhi ya wafuasi wao wakilalalmika eti vbyombo vbya habari vinaichukia CUF bila sababu na ndo maana havikipi kipaumbele katika habari zao. Kuepukana na hili, si waanzishe tu gazeti lao wenyewe? Nakumbuka kulikuwapo gazeti la Fahamu ambalo lilikuwa linawapigia debe mwaka 2005 -- ikawaje tena?
   
 7. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Al Nuur...ishu ya nembo ya udini si tatizo, mbona wakati wanamkaribisha Mwera wa Tarime alisalimia 'ASALAAM ALEKUUM'....
   
 8. C

  Calipso JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Alichozungumza Pr Lipumba ni uhuru na maadili ya waandishi, usibadilishe mada,kuwa na gazeti lake ama hawana ni miongoni mwa mipango yao, kwani Nipashe ni gazeti la chadema? mbona wameipa kipaumbele sana,majira je? mwananchi je? yote hayo wameipa chadema kipaumbele,kama watatoa habari za cuf basi ni kwa uchahe sana na tena page za ndani huko. na mdau mmoja umezungumza kuhusu gazeti la kubeinea,nani asiejua gazeti la kubeinea ni la nani,kumbuka mpaka kesi alikua nayo mhakamani.. fuatili uzuri chanzo cha gazeti hilo...
   
 9. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,730
  Trophy Points: 280
  Al huda
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Yote unayosema huenda ni kweli. sasa kama magazeti hayo yamekipa kisogo CUF, sasa kifanyike nini? Hakuna sheria ya kulazimisha gazeti kuandika habari zako hata kama huko ni kwenda kinyume cah maadili, au hata kwa pesa, kwani anayo hiari ya kukubali au kukataa, na si lazima atoe sababu. Kwa gazeti kuandika habari ya chama fulani ni hisani tu na siyo lazima.

  Inawezekana, kwa mfano, wamegundua kwamba wakiandika habari za CUF mauzo yanapungua. Nasema kwa mfano tu.

  Swali linabakia pale pale -- kwamba kuepukana na yote haya si bora CUF ingekuwa na gazeti lake? Ingekata kabisa mzizi wa fitina. Au unayo sababu ya msingi ya chama hicho kutokuwa na gazeti?
   
 11. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #11
  Aug 24, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  Al Sahaf wa Iraq
   
 12. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Acha uzushi nyie ndio wenye fikra mgando Annur ni gaazeti la Kiislam na lina chapishwa na taasisi ya kiislam au ndio nyie mnaosema CUF chama cha waislamu?
   
 13. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  msiseme kwa kuwa manataka kusema tu tupeni proof, kama ya kusema Tanzania daima ni ya chadema si sawa sote tunajua ni ya freemedia uhusiano wake pengine mwenyekiti wake ndio mmliki sasa tunaomba mtutajie wamilikiwa hiyo al huda na al nurr acheni unafiki Mungu anapenda wanaosema ukweli na hakuna dhabi kubwa kama unafiki.
   
 14. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,730
  Trophy Points: 280
  Wewe ndiyo mnafiki mkubwa hivi hujui magazeti hayo yanashabikia chama gani hapa nchini? suala la kutaja wamiliki si hoja ya msingi , hoja hapa je hao wamiliki wana sera gani? Siku zote tunaona hoja za magazeti hayo ni kuipigia debe CUF, kama unabisha ubishe tu.
   
 15. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,134
  Trophy Points: 280
  halafu walijibu...alikuwa msalani...
   
 16. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #16
  Aug 24, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,134
  Trophy Points: 280
  al nuur na al huda ndiyo vijarida vya cuf ndiyo maana haiwezi kuhangaika kuwa na kijarida kingine maana vilivyopo ni vya kidini na cuf ni taasisi ya kidini zaidi
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  Aug 24, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Al huda na Al-Nuur kila Ijumaa haya ni CUF! Huwa yanagawiwa misikitini baada ya swala Ijumaa.
   
 18. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #18
  Aug 24, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Eh!
   
 19. Wun

  Wun JF-Expert Member

  #19
  Aug 24, 2010
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 353
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ninawaonea huruma sana na fikra zetu watanzani kweli akili mgando.poleni sana
   
Loading...