Hivi Kunguru weusi wamepotelea wapi hapa Dar?

Crimea

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
26,815
Reaction score
38,887
Kuna kipindi walikuwa wengi sana..kiasi kwamba huku uswahilini ilikuwa unaweza kupika nyama yako jikon akaja kufunua ili achukue!

Akina mama ilikuwa unakuta anaosha vyombo nje huku anafukuzana na kunguru..

Nguo za watoto zikianikwa unakuta zimebebwa na kunguru..

Pale Ikulu kunguru walikuwa wanahanikiza kwa kelele mpaka mtu una jiuliza wamefugwa ama?

Kiufupi kunguru weusi walikuwa wengi na walikuwa kero sana kwa wakazi wa dar. Siku hizi wapo ila mmoja-mmoja sana. Hivi kulikuwa na mpango wa kuwaangamiza ama?
 
Kweli wamepungua kiasi, nakumbuka kunamwaka nilienda kwa jamaa yangu Magomeni Usalama basi wakati namsubiri atoke ndani kunguru akawa anaimendea simu yangu niliyokuwa anandiki text sio siri nilibanwa na kicheko
 
Unajua hawa kunguru si wenyeji wa dar,ni wahamiaji tu na inawezekana kabisa tabia zetu huku bara zimewachosha wakaamua kurudi nchini kwao zenj.
 
Unajua hawa kunguru si wenyeji wa dar,ni wahamiaji tu na inawezekana kabisa tabia zetu huku bara zimewachosha wakaamua kurudi nchini kwao zenj.

teh teh....wameenda kupiga kampeni ya kukataa katiba pendekezwa!
 
wamerudi kwao india baada ya kampeni ya tokomeza kunguru weusi kurushwa dar.....kila ukiuwa mmoja ulukuwa unapewa kati ya mia moja na mia mbili............!!
 
Ni Kampeni na sikumbuki ulifadhiliwa na Norway au nchi gani si kumbuki.Lakini ipo mitego mingi tu na kila baada ya muda jamaa huja na gari kuwakusanya na kwenda kuwateketeza. Pia niliwahi kusikia kuwa ilikuaepo campaign ya kukamata kunguru unalipwa pesa na Hao jamaa
 
Mbona wapo wengi tu hapa dar,mimi naona umechanganya waliopotea ni wale walio na baka jeupe kifuani lakini hao wala mizoga wapo tele ,kwani wewe mkuu unawala hao
 
Bado wapo ingawa si kwa wingi

Hawa wanaiba hadi chujio la chai

Vifaranga wanabeba

Ole wako uweke nyama ovyo wanaichukua kama wamenunua wao
 
Kutokana na ugumu wa maisha wananchi wameamua kuwafanya kitoweo.....
 
Naona wengi wenu mnachanganya mambo humu. Kunguru anaowauliza mleta uzi ni wale weusi wenye doa jeupe kifuani na ni wakubwa kuliko hawa kunguru wezi wanaonyea watu hovyo. Ila baadhi ya mikoa wapo wale hapa Dar ni nadra sana kuwaona.
 
Ile mishikaki ya chelewa mnayobugia huko ndio imesaidia kuwapunguza punguza..
 
Hahahaha majibu yaliyotolewa humu! Hata kama jamaa alikua serious nafikiri imebidi acheke tu!
 
kampeni ya kuwapunza kunguru 2010 au mmesahau.
 
Unajua hawa kunguru si wenyeji wa dar,ni wahamiaji tu na inawezekana kabisa tabia zetu huku bara zimewachosha wakaamua kurudi nchini kwao zenj.

alafu pale zenji kuna kunguru wenye mabaka meupe shingoni hawapatani kabisa na hawa kunguru wa bara
 

Huu hapa ndio mtego wao, upo hapa NIT (Chuo Cha Usafirishaji)
 

Attachments

  • 1413202906639.jpg
    113.6 KB · Views: 87
  • 1413202933719.jpg
    100.2 KB · Views: 77

Hii mitego iko mahali pengi sana. Unaweza usijue kama ni mitego
 

Attachments

  • 1413203475143.jpg
    78.4 KB · Views: 75
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…