Hivi kuna wake kama huyu mama kwa tabia?

Namshukuru mwenyezi mungu, nami nna aina ya mwanamke kama huyo, though hatuna kazi za kuajiliwa, but tuko pamoja na tunashare each and everything together.
wife yuko simple sana, na anajua nini anataka kwenye haya mishaps again thanks God.
"nitakupenda kwa moyo wangu wote mama kijacho wangu"..
 
wasali sana pia maana shetani hakawii !
i bet mume hajawah kuonja kitu pombe kabisa
 
Wamebaki wachache sana wenye tabia hii, japo mara nyingi wake zetu wanakuwa na tabia nzuri au mbaya kutokana na sisi wanaume tunavyoishi nao. ukiwaonyesha upendo nao watakuwa na upendo kwako, mume ukiwa bandidu nae atakuwa bandidu zaidi yako.
 
Ebu weka picha yake kwanza tumuone
6146a8d35f347645c382c2d83ed08c71.jpg
 
Mume aliachishwa kazi miaka 4 imeisha, mke hajawahi lalamika hata siku moja kwanini mwanaume hatoi hela na hajawahi mlalamikia mwanaume kuhusu mahitaji ya pesa ndani,

Mke huwasilisha pesa zote za marupurupu mezani kila anapotoka kazini ili mwanaume atunze na apange matumizi yake,

Mke amekataa kujihusisha na bajeti ya pesa ndani pamoja na kuwa yeye ndiye ana kipato kwa miaka yote hii 4, ila mwanaume akimwambia wapange bajeti ndio anakubali si vinginevyo,

Mke kamuachia mwanaume kuwa mshauri mkuu wa pesa anazo tafuta yeye mke, kitakacho amuliwa na mwanaume na kuona kinafaa basi mke huridhia mke hana neno,

Mwanaume ndiye kaachiwa kadi ya benki kutoa na kupanga matumizi,

Mke hana tama ya kupenda vitu vya hali ya juu huwa mwanaume ndiye anaamua kumchukulia mke vitu vyenye thamani ila mke hataki, mke husema kama mume ataleta au kumnunulia sawa ila sio yeye.

Maswala mengi yanayohusu aina ya vitu, chakula na maisha yao mwanaume ana nafasi kubwa sana pamoja na kutokuwa na kipato,

Mwanamke kila atokapo kazini hufikia kumpa ripoti ya kazi alizozifanya na kipato alichokipata kwa siku hiyo, mke hana password kwenye simu mara nyingi humpa mumewe atumie simu yake na mumewake humpa mkewe simu yake atumie,

mke na mume hawana hata chembe ya siri ndani kwao, mume alipokuwa akifanya kazi alikuwa anamwachia mke walet kujua kuna hela ngapi, mfukoni mwa suruali mke hujua mume wake ana sh ngapi, mke alikuwa anajua benki mumewake ana sh ngapi na password zote anazijua mke


Wana JF nimeliona na nimeshuhudia nimeshangaa sana kwa mke kuwa na tabia hizo zaidi sana anajua mume hana kazi halafu amekataa kuwa msiri mwanaume anajua kila kitu hadi password zote za benki…

Hivi kweli wanawake kama hawa tunao wangapi. Ila huyu mwanaume sio kwamba kalelewa hapana au ameolewa hapana najiuliza je hili lawezekana kumpata mwanamke kama huyu.
Wakati mwingibe unapoandika ujue wasomaji wako ni watu wazima. Dunia hii hakuna mwanamke mwenye sifa zote hizo ulizotaja hapo. Ukimtaka bensa sayari nyingine au umba wa kwako
 
Wakati mwingibe unapoandika ujue wasomaji wako ni watu wazima. Dunia hii hakuna mwanamke mwenye sifa zote hizo ulizotaja hapo. Ukimtaka bensa sayari nyingine au umba wa kwako
Huyu Mama ni Manager wa Benki moja wapo hapa nchini sitaki kumtaja hapa na uzi huu si ajabu ameusoma. yuko Mkuu amini hili ni swala la kujipima kila mtu na mkewe au mumewe na kuangalia yana madhara gani na kujiuliza je kuna ubaya gani kuishi maisha kama haya, tatizo tumezoea kuwa na mengi ya sirini ndio maana tunaona ni ajabu ila ndivyo ilivyo. wapo, wakubwa na watu wazima tusome na tujifunze.
 
Umenikumbusha last year nilipokuwa jobless na yf akawa analeta pesa zote za mshahara wake kwangu na tunakaa pamoja kupanga matumizi ya pesa hizo. God blessed me with a wonderful wife.
 
Kuna mwanamke ukimpata maishani unaona ni kama zawadi toka kwa muumba.
 
Back
Top Bottom