Michael Chairman
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 922
- 583
Ibara ya 63 na 64 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inaanisha na kuyataja majukumu ya mbuge kama inavyosema kwa sehemu hiyo ya Ibara ya 63
(1) Rais kama sehemu moja ya Bunge atatekeleza madaraka yote aliyokabidhiwa na Katiba hii kwa ajili hiyo.
(2) Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.
(3) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge laweza-
(a) kumuuliza Waziri yeyoyote swali lo lote kuhusu mambo ya umma katika Jamhuri ya Muungano ambayo yako katika wajibu wake;
(b) Kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti;
(c) Kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano, na kutunga sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango huo;
(d) Kutunga sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji kuwapo sheria;
(e) Kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa kwa msingi huo mimi sioni kama Tanzania kama nchi inaweza kupiga hatua kupitia majukumu haya ya mbuge kwani kwa namna yoyote ile kazi hizi haziwezi kuleta tija kwa jamii inayohitaji maendeleo na wala si kuwakilishwa na mbuge Serikalini hali ya kuwa serikali kila kukicha ipo huko kwenye jamii hiyo inayodaiwa kuwakilishwa na mbuge. maoni yangu ni kuwa majukumu haya ya mbuge yanapaswa aidha kuongezwa au kubadilishwa.