Hivi kuna siri gani ya mtu kuwa mweupe na kuwa na mvuto kwenye hizi maeneo?

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,604
Hii ni observation ndogo tu nimekuwa nikifanya. Si maanishi nipo sahihi wala sitaki kuamini kama nipo sahihi ila nilitaka kujua hii kasumba ni kwanini ipo hivo. Imejitokeza sana kwamba mtu mweupe kwenye jamii zetu za kiafrika aonekana kama vile ni mtu ambaye status yake ipo kubwa kidogo

Muonekano kwa watu
Yaani mtu mweupe akienda mahali fulani huwa anakuwa noticed mapema sana, utaanza kusikia 'White' 'White'. Ila mtu mweusi akipita huwez ona watu wakishtuka kama inavokuwa kwa mtu mweupe.

Kwenye hili utaona kabisa watu weusi mpaka wanajichubua ili waonekane weupe. Hii wanaume kwa wanawake. Na ukiwauliza haswa wanakuambia eti wanataka kuwa na mvuto.

Kuwa na pesa
Hii imenifanye niache kwenda kwenye soko la Karume, yaani wale jamaa ukipita kule sokoni 'White' 'White' njoo nikuoneshe shati, ukijeuka huyu naye anakuita njo ona kadet, huyu njoo ona moka kali. Yaani inakuwa kama kero fulani hivi. Sasa kuna siku nikamuuliza jamaa mmoja muuzaji, mbona mi nikipita humu sokoni kila mtu anadhani mi ni mteja? Yule jamaa akadai eti 'Wewe kwa sababu ni mweupe kila mtu anajua una hela, kuwa eti wao wanaamini mtu mweupe ndo mwenye hela'

Mapenzi
Hii sijui ipo kwa kiasi gani ila, kuna wanawake huko kipindi cha ujana damu kali nilikuwa katika mahusiano sasa wakawa wananiambia eti. 'Nimekupenda sababu wewe ni mweupe' Ooh mara mi sipendi wanaume weusi... Lakini bado mi nikiangalia sioni bado ni kwanini mweupe.. Yaani ina add value kwa kiasi gani kwa mtu kuwa na mpenzi mweupe?

La mwisho kabisa, ni mara chache sana kupishana na machokoraa ama vichaa weupe. Kwa uzoefu wangu, wengi nnaowaona wanakuwaga ni rangi nyeusi. Sasa je ina maana hapo bado sielewi kuna siri gani.

Nisameheni kwa hii mada mbovu, mimi mwenyewe najua ni mbovu, sio kawaida yangu kuja na nyuzi mbovu hivi.. ila sio mbaya tukijadili pia hili suala la kuwa mweupe na uhusiano wake katika mapenzi, uongozi, kazi, na mafanikio
 
Ilo lakuonekana una pesa , hata sisi MABLACK sura ngumu tunaonekana tunazo kikubwa ni kua smart tu.


Ilo LA kupendwa na MADEMU,..kila MTU na Mtuwe , hata Mimi naambiwaga ,kua "Mwanaume mweusi kama wewe Unanimaliza nyang'anyang'a".


Tena nyie maWhite, maisha yakiwatandika, +harufu ya kuchomwa najua+ midevu mnaonekana kama Mizuka.





Pia nyie maWhite, hata MADEMU wenu weupe , Akili inaamiaga kwenye Rangi nyeupe ulionayo ...ndo maana Mnakuaga na maringo sana, mbwembwe kibao, ..alafu mwisho wasiku mnazalishwa Home !!!.
 
Ilo lakuonekana una pesa , hata sisi MABLACK sura ngumu tunaonekana tunazo kikubwa ni kua smart tu.


Ilo LA kupendwa na MADEMU,..kila MTU na Mtuwe , hata Mimi naambiwaga ,kua "Mwanaume mweusi kama wewe Unanimaliza nyang'anyang'a".


Tena nyie maWhite, maisha yakiwatandika, +harufu ya kuchomwa najua+ midevu mnaonekana kama Mizuka.





Pia nyie maWhite, hata MADEMU wenu weupe , Akili inaamiaga kwenye Rangi nyeupe ulionayo ...ndo maana Mnakuaga na maringo sana, mbwembwe kibao, ..alafu mwisho wasiku mnazalishwa Home !!!.
Wanawake weupe wamekukosea nini jombaa mbona povu ivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona mambo ni simple tu hata katika kufua huoni unatenga nguo nyeupe kivyake na zarangi nyingine tofauti na kufua huwa unaanza kufua nyeupe kisha ndio unafuata rangi zingine 😊

Lakini mm kwenye mapenzi hapo nitakuwa tofauti mm na penda sana wachumba weusi.
 
Back
Top Bottom