USHAURI
1. Chukua siku tatu bila kumtext wala kumfatilia au kumtafta mahara popote
2. Kama huna mtu yeyote wa kuwasiliana nae, weka simu mbali usijishughulishe na lolote kwenye simu hata games usicheze, hii itakusaidi kukwepa kumtumia text
3. Pendeza, acha kuvaa yale mavazi uliokuwa ukivaa pindi uko nae, jibadilishe kabisa,jipende aswa kama unauwezo wa kununua viwalo nunua, tupia upendeze
4. Badili muonekano wa chumba na achia kutembelea sehem mlizozoe kukutana
5. Sali sana, Mungu anakupenda muombe atakupa mpenzi mwingine
6. Amini kila kinachotokea kina 7bu zake asa kukukuza/kukufunza, yanakutokea sababu hayajawai kukutokea na mshukuru Mungu kwamba yametokea, je, vp angekuficha?!
7. Kubali ukweli hata kama ni utani/uwongo
8. Fikiria ni mwanamke wa aina gani ungependa awe mke wako asa kitabia
9. Spend time na washikaji na panga mipango yako kila hasubui na mambo yote yatimize kwa namna ulivo yapanga
10. Epuka kuwaza visasi, vitakupa majuto na kukuongezea majonzi kuliko uliyo nayo sasa hivi
11. Anza kuishi mwenyewe, acha kufikiria kumpata mwingine
12. Kama unamachungu na utokwa machozi , nenda sehemu ambayo unatakiwa uwe pekee yako nakushauri anza kumfikiria na lia kabisa lia ata ukimaliza masaa matatu unamwaga machozi, acha machozi yatiririke itakusaidia kupunguza machungu na usione haja tena ya kumlilia
13. Amini KARMA ipo itamlipa naye ipo siku itamtokea cha msingi ongeza juhudi na bidii katika shughuli zako, waza mapene waza vitu vikubwa, nyumba, magari nk kwa ujumla waza ndoto zako
MUACHE AENDE ZAKE!!
Huo ndio ushauri wangu utaniletea mrejesho
Keep to be UWABATA[emoji3] chama la wana hiyooooo!!
View attachment 1845643