Hivi kumbe baadhi ya watanzania waliosoma na kufaulu vizuri wanaongoza kwa majungu??

Ilankunda1234

JF-Expert Member
Dec 28, 2015
4,842
4,777
Habari wakuu,

Mi nimeuleta uzi huu baada ya kutembelea nyuzi nyingi na habari mbalimbali kutoka mutandaoni na sehemu nyingi ambazo mtu anaweza toa yale yaujazao moyo.

Sababu zilizonifanya nifungue kinywa ni hizi:-

1. Kwanza wanaamini kua ajira zote zilipaswa ziwe zao na maisha mazuri yapo kwa ajiri yao. Hapa ukiwakuta wakijadili mpaka namna ya mjasilia mali fulani anavyokosea kuendesha shughuri zake wakiamini bora wangekua wao.

2. Napojikuta labda sehemu alipoenda kuomba kazi akamkuta mtu ambaye anamzidi hata kwa GPA tu za ufaulu utakuta analalamika eti haiwezekani na maneno mengi ya kijungu.

3. Huwa huwacheka na kuwadharau wale wenye kada za moja kwa moja ajira zake na zenye mshahara ama wanaosema ni mdogo kama Ualimu, polisi, jeshi n.k. hapa hua sipendi kanlbisaaa kulitolea maelezo na wakati waliowengi hujikuta wakikosa kazi hufikiria hata kuanza kuomba tempo za ualimu.

Sitaki kupatolea maelezo hapa,, yani mtu huyu akiingia ofisuni huhitaji apewe heshima ya GPA zake na division 1 na 2 zake. Kitu ambacho kiukweli hakiendi hivyo akiambiwa kufuata taratibu na kanuni za ofisi na hitaji kuaply matumizi ya ufaulu wake,, akikataliwa utamsikia mtaani yeyet ni wa majungu

4. Hujiona bora na wao ndio watu wengine ni binadam tuu.
Hapa wengi ni mashahidi kwa hili angalia mtu aliyesoma na kufaulu vizuri wengi na mwelekeo wa maisha hupotea pale anapokosa kazi huishia sana kulaumu na kuona wote ni watu wasiojua na pia utawajua wakikutana wale ambao wanaufalu sawa na wamekosa kazi hujadili maisha ya watu waliofaulu kawaida na maisha wametusua.
 
Kuna wasomi wa aina mbili; walio elimika na wasio elimika. Wasomi unao waongelea wewe ni wale ambao hawaja elimika. Hawa huwa wamejaa dharau, kiburi, kujisikia, kujiona, kujidai, nk.

Aina hii ya wasomi unaweza ukawakuta wanaishi maisha ya kifahari halafu wazazi na ndugu zao huko vijijini walikotokea wakiishi kwenye dimbwi la umaskini. Kiufupi ni watu wabinafsi na walafi waliopitiliza.

Binafsi sina ujasiri wa kumdharau mtu kwa sababu tu ya umasikini wake, elimu yaje, kazi yake halali inayomuingizia kipato, umri wake, jinsia yake, nk. kwa kuwa tu eti mimi ni zaidi yake na ni msomi! Huo ndio tunaouita ULIMBUKENI! Mbaya zaidi wanaoitwa wasomi wengi wa Tanzania wanaangukia kundi hili.Wamejawa na superiority complex isiyo na tija dhidi ya makundi mengine.
 
Hii ni kawaida kwa wasomi wa kibongo wasio elimika, anataka waitwe ma eng, dr ili hali hakuna hata project moja walizosimia kudhihirisha usomi wao, zaidi ya usomi wa makaratasi, dharau, kiburi na ujivuni ndiyo sifa yao.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom