Haki ya MUNGU Watanganyika lazima tubadilike na kuitukuza Tanganyika yetu. Wazanibar wametupiga bao wanajitambulisha kwa uzanibari na upemba. Mi mzanzibar mi mpemba .Sisi watanzania mpaka ukakasi mi MTANGANYIKA. TAFAKARI BADILIKA CHUKUA HATUA .Jivunie Utanganyika wako
......ole wao wanaojiita watanzania, maana mimi nikiangalia mbele siioni Tanzania zaidi ya Tanganyika na Zanzibar, akah! mi mtanganyika yakhe!Jana tulikuwa kwenye udahili katika chuo fulani cha umma, sasa kwenye fomu yao, sehemu ya uraia wa mdahiliwa mimi nikaandika kuwa ni Mtanganyika. cha ajabu ni kuwa mhusika alishangaa ile fomu, kisha kuniuliza mara kadhaa kwamba kimejiri nini hata nijitambulishe hivyo, tena akauliza kwani tunachotaka ni nini hasa, kwani ameona fomu kadhaa zikiwa zimejazwa hivyo. Sasa nauliza wana jamvi, izi zea e problemu na Utanganyika wangu?
......ole wao wanaojiita watanzania, maana mimi nikiangalia mbele siioni Tanzania zaidi ya Tanganyika na Zanzibar, akah! mi mtanganyika yakhe!
......ole wao wanaojiita watanzania, maana mimi nikiangalia mbele siioni Tanzania zaidi ya Tanganyika na Zanzibar, akah! mi mtanganyika yakhe!
Samahani na pole kwa kum- overestimate maalim. Ulivyomdhania sivyo alivyo kabisaaaa... Kifupi yule ni mchumia tumbo!Kuna yale maonyesho ambayo hufanyika Zanzibar kila mwaka, waandaaji kwa kukosa fedha za kuendeshea wakaamua wayahamishie huku "Tanzania bara". Nikamsikia Maalim Seif Sharrif Hamad (Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar) akikataa na hapa namnukuu "Mimi siafiki maonyesho haya kupelekwa Tanganyika". Kwa kiongozi mkubwa hivyo kusema hayo, basi hata wao wanaijua. Ndo maana mimi sipendi siasa ni KIGEUGEU.
Jana tulikuwa kwenye udahili katika chuo fulani cha umma, sasa kwenye fomu yao, sehemu ya uraia wa mdahiliwa mimi nikaandika kuwa ni Mtanganyika. cha ajabu ni kuwa mhusika alishangaa ile fomu, kisha kuniuliza mara kadhaa kwamba kimejiri nini hata nijitambulishe hivyo, tena akauliza kwani tunachotaka ni nini hasa, kwani ameona fomu kadhaa zikiwa zimejazwa hivyo. Sasa nauliza wana jamvi, izi zea e problemu na Utanganyika wangu?
LOL. Wewe dogo haujatulia
Ningekuwa nakulipia mimi school fees ningeku-ground, hahaha!
Anyway, alimradi ulitaka kuburudisha kidogo, mbona haukutumia jina la kwanza kabisa la hii nchi, yaani German East Africa! Au Deutsch-Ostafrika.
I hope unajua kuwa hii nchi iliundwa na waJerumani na baadaye kupewa jina la Tanganyika na waIngereza walipowashinda waJerumani katika vita ya kwanza ya dunia. Infwakti baba wa taifa wa kikwelii ni Karl Peters na siyo Kambarage!
duh! Umenifumbua macho, ila katika Deustche Ostafrika watu hawakuwa huru kama ilivyo sasa. Ni vigumu kutaja kama nchi yetu. Karl Peters hawezi kuwa baba wa taifa kwa kuwa alikuwa akisimamia matakwa ya Udachi na Wadachi, Nyerere anastahili kwa kuwa alikuwa pale kwa maslahi ya nchi na wananchi.