Hivi Kikwete hachukiwi na wasomi tu?

mbombongafu

Member
Nov 1, 2010
61
3
Jamani nilikuwa najua watu wanaompinga kikwete na utawala wake ni wasomi wengi wao kumbe hata watu wa kawaida wanaona hali ya hewa ilivyo na wamesoma alama za nyakati. Nilikwenda kumchukua wife wangu salon moja huko sinza na leo mkulu karudi television karibu zote zimejaribu kumuonyesha airport, wife ananiambia hiyo habari ilivyoanza tu kila mwanamke pale salon alitoa msonyo wa nguvu, wengine wanasema "huyu nae"yaani baada ya hapo kila mtu anamuongelea vibaya mkulu wetu nikasema duh, kumbe hata wa kawaida wanayaona ya mkwere kwamba kachemsha.
Kazini kwetu o.c tumeomba bilioni nane na ndio kawaida kupewa safari hii tumepewa milioni 800, unategemea kutakuwa na ufanisi ofisini?mkwere unatupeleka pabaya kuanzia wafanyakazi na wafanyabiashara ni vurugu tu
 
Unafahamu kama huna uwezo na kuvamia mambo ambayo ni mbingu na dunia matokeo yake ndio haya. atamaliza vibaya kwa sababu ya kuwakumbatia mafisadi. Ooops na yeye ni Fisadi pia.
 
Wenzake walimuweka ili wajiandae kuchukua Kaya.Bahati mbaya alipoingia kunyumba akakuta kuna taratibu zisizoruhusu kuingia kwa kupokezana vijiti. akaamua kuwatosa walomtanguliza ili awasafishie road! badala yake ameamua kumwaga mboga kwa kuvurunda!! wao wameamua pia kumwaga ugali!!!
 
Sio salon hata kwa mama ntilie yaani sasa hivi kila mtu kazinduka hatutaki tumechoka sana kwa kweli. Hali ya nchi inakatisha tamaa
 
Nahisi sasa tanzania kilichobaki tunahitaji mtu wa kututekenya na kutuorganize tuanzishe liberation square yetu mkwere aende kwao
 
Kwenye daladala!! ndio balaaa, yaani watu hawa pamoja na miimi! hatumtaki huyu jamaa
 
Na wengi wa hao wasio na elimu na uelewa ni wanaofuata mkumbo mathalani utakuta mtu anadai katiba mpya wakati ya zamani haijui!
 
PHP:
Kazini kwetu o.c tumeomba bilioni nane na ndio kawaida kupewa safari hii tumepewa milioni 800, unategemea kutakuwa na ufanisi ofisini?mkwere unatupeleka pabaya kuanzia wafanyakazi na wafanyabiashara ni vurugu tu

Huku kwetu TT ya mshahara wa mwezi wa kwanza iletwa ikiwa inaupungufu wa Shs. 28 mil. Ilibidi Halmashauri ijazie ili mshahara ulipwe!!! Wacha OC.... Kunasiku hata mishahara hatutapata mkubwa!!!...
 
Wakuu, nadhani sasa wakati umefika tutambue ya kuwa nchi yetu ni failed state na mkuu wa nchi amekosa mwongozo. Tokea 2006 alipochukua nchi alikuwa hatuongozi. Kila kitu ilikuwa remote control na system ilikuwa inaenda na steam ya awamu ya 3 lkn sasa baada ya 2010 mipango imekamilika au ku expire ...sasa JK na kabinet lazima watupe mipango yao na hawana vision au overall strategy. Now everything is falling apart ...
 
dah.huyu jamaa anaacha wananchi wake kwenye janga kubwa la mabomu yeye anapaa kwenda ivory coast sijajua uwezo wake.
 
huko kote tisa kumi ni kwamba, polisi na wanajeshi wamechoshwa na siasa, mabomu ya gongolamboto ni pigo kubwa sana na Mwamunyange ameonekana vibaya na jamii za kimataifa na kupoteza sifa yake lakini amegundua kuwa JK ndiye amepelekea hayo yote na polisi nao mauaji ya arusha wameona siasa chafu za ccm ndizo zimepelekea kukosa kwao msimamo. Mwema ana akili na mchapa kazi, ila jamaa alim-mislead hivyo jeshi limejipanga na polisi wamejipanga na for sure wapo upande wetu.

hivyo jamaa ana hali mbaya.
 
PHP:
Kazini kwetu o.c tumeomba bilioni nane na ndio kawaida kupewa safari hii tumepewa milioni 800, unategemea kutakuwa na ufanisi ofisini?mkwere unatupeleka pabaya kuanzia wafanyakazi na wafanyabiashara ni vurugu tu

Huku kwetu TT ya mshahara wa mwezi wa kwanza iletwa ikiwa inaupungufu wa Shs. 28 mil. Ilibidi Halmashauri ijazie ili mshahara ulipwe!!! Wacha OC.... Kunasiku hata mishahara hatutapata mkubwa!!!...
Kaka vitu vingine sio serikali ila watendaji wamechoishwa na wanaboronga makusudi ili serikali itoke.
 
Na wengi wa hao wasio na elimu na uelewa ni wanaofuata mkumbo mathalani utakuta mtu anadai katiba mpya wakati ya zamani haijui!

hakuna kipengele chochote cha katiba ya Tanzania kinachomtaka au kumshurutisha mtu au mwananchi kuijua katiba ..... dhumuni la katiba ni kuendesha nchi kwa misingi ya kisheria katika nyanja zote .... kutokuijua katiba siyo excuse ya kudai katiba .... representation ya wanaoijua katiba kuwa mbovu inatosha .... sielewi fikra zetu zikoje lakini sipati picha kwa mama ntilie au fundi gereji umpatie katiba aisome yote kifungu hadi na aielewe yote ... hata sisi wenyewe hakuna mtu mwenye uelewa wa katiba yote ..... ni baadhi tu za sehemu zinazogusa utendaji husika ... mbona DCI Manumba aliulizwa kuhusu sheria katika katiba zinazounda jeshi la polisi akasema hajui kwani yeye siyo mtaalamu wa katiba ... na hawa ndio viongozi wa nchi yetu ... hivyo unataka mama ntilie aijue katiba wakati DCI Robert Manumba haijui katiba..! lol

lets be realistic
 
Jamani hata wazee huku Mwanza wana hasira na mkwere zamani vijana tulionekana wahuni
 
huko kote tisa kumi ni kwamba, polisi na wanajeshi wamechoshwa na siasa, mabomu ya gongolamboto ni pigo kubwa sana na Mwamunyange ameonekana vibaya na jamii za kimataifa na kupoteza sifa yake lakini amegundua kuwa JK ndiye amepelekea hayo yote na polisi nao mauaji ya arusha wameona siasa chafu za ccm ndizo zimepelekea kukosa kwao msimamo. Mwema ana akili na mchapa kazi, ila jamaa alim-mislead hivyo jeshi limejipanga na polisi wamejipanga na for sure wapo upande wetu.

hivyo jamaa ana hali mbaya.

Aithee fafanua aithee, Je, hii ni siriasi?
 
Back
Top Bottom