Hivi Kikwete hachukiwi na wasomi tu?

Sisi huku kwetu hatujalipwa malimbiko ya mishahara mipya aliyotutangazia wakati anaomba kura. Chama chetu cha wafanyakazi na Hazina walikubaliana mwezi January kuwa tutalipwa malimbikizo ya mishahara mwezi huu February. Tetesi ni kwamba hadi hii leo hazina hakuna pesa ya kulipa malimbikizo hayo ya mishahara na kudhihirisha hayo hata OC nayo imechinjwa by 16%.

Sasa tunasubiri hii February imalizike chama chetu cha wafanyakazi kiitishe mngomo nchi nzima. (NOTE SIO TUCTA) ni TUGHE. And we are serious kama pesa ya kulipa DOWNS inapatikana chapuchapu kwanini sisi wafanyakazi tusilipwe sitahili zetu? Lazima kuchimbike tu.
 
Wakuu, nadhani sasa wakati umefika tutambue ya kuwa nchi yetu ni failed state na mkuu wa nchi amekosa mwongozo. Tokea 2006 alipochukua nchi alikuwa hatuongozi. Kila kitu ilikuwa remote control na system ilikuwa inaenda na steam ya awamu ya 3 lkn sasa baada ya 2010 mipango imekamilika au ku expire ...sasa JK na kabinet lazima watupe mipango yao na hawana vision au overall strategy. Now everything is falling apart ...

Unaongelea habari za strategy na mipango kwa mkwere, yeye anapambana na linalotokea. He has never been a leader mkwere. Na hakuna jipya la kutegemea kutoka kwa huyu jamaa.
 
Piga ua, huyu jamaa hakushinda huu uchaguzi na ndio maana hana uchungu wowote...anaebisha abishe tu
 
Chesty umesema kweli kabisa tunachoona ni kukosekana kwa uongozi. Hii iwe fundisho kwetu kuwa urais huhitaji kiongozi si kumpigia kura eti kwa kuwa ni handsome.
 
Na wengi wa hao wasio na elimu na uelewa ni wanaofuata mkumbo mathalani utakuta mtu anadai katiba mpya wakati ya zamani haijui!

hakuna mtazania asiye jua katiba ya sasa bali tunatofautiana katika uelewa!!! wananchi wa tz wanajua yafuatayo
Haki ya kupiga kura
Raisi kuteua wabunge 10
Raisi kuteua wakuu wa mikoa ,wilaya,makatibu wakuu wa wiza etc
Muungano wa tanganyika na zanzibar
na mengine mengi sana
Jamani m2 mwenye uelewa wa hayo hapo juu utasemaje hajui katiba ya tanzania??? plz tusisubiri wa2 waanze kunukuu kama wanasheria!!!
 
Back
Top Bottom