Mkombozi,
Kwa mujibu wa taarifa zisizo rasmi kutoka jikoni, ni kwamba mawaziri waliopo madarakani sasa ndio waliotoa fungu kubwa katika kumuweka mkuu pale alipo, sasa kuwaondoa kabla hisa zao hazijaisha ni sawa na kukata tawi ambalo bila shaka unakuwa umelikalia. Unafikiri matokeo yake ni nini?
Jamaa hawezi kuwafukuza mawaziri wanaochemsha kwa sababu walichangia kwa kiasi kikubwa sana kumuwezesha muungwana kushinda. Wengine waliwahonga wahariri ili habari njema zisambazwe na mtandao ufahamike, wengine walianzisha tovuti na kuzilipia katika kutangaza jina la mkuu, kuna wengine ndio waliochapa zile khanga, T shirts, kapelo, beji, vipeperushi na mabango. Sasa ukiwaondoa watu muhimu kama hawa unatarajia nini? Hawa ndio siri ya ushindi wa kishindo wa 80%, kwa hiyo ndio uhai wenyewe wa muungwana, ndio maana anagwaya kuwang'oa. Hio ngumu!
Mfano mzuri, mkuu wa mkoa wa Manyara Bw Henry Daffa Shekifu ni mwanamtandao na alishiriki kwa kila hali kumpigia debe muungwana tangu uchaguzi wa 1995. Habari hizi alizisema mkuu, mie nilikuwa sifahamu kabisa kuwa jamaa alikuwa ni mpiga debe wa mkuu. Huyu bwana alipogombea ubunge kule kwao Lushoto alimwagwa katika kura za maoni na kwa kuwa ni mwanamtandao, akaongea na mkuu, mheshimiwa mkuu akaahidi kuwa sisiemu haitamtupa (kumbuka nilikuwepo wakati wa kampeni za 2005 wakati ahadi hii inatolewa pale uwanja wa Omar Ali Juma Lushoto). Mwenye shaka na ushahidi huu awaulize watu wa Lushoto, bifu kati ya Shekifu na mbunge wa sasa Bw Mshangama. Mara baada tu ya mkuu kukwaa ulaji tukashtukia Shekifu ni mkuu wa mkoa wa Mtwara. Akarudi na kuwatambia waliomyima kura, kuwa kama walidhani wanamkomoa basi wameula wa chuya, sasa anapeperusha bendera ya taifa, sio ya chama tena. Sasa Bw Mkombozi, ama Mushobozi, unadhani mtu kama huyu akibofoa katika uongozi ataadabishwa kweli?
Mfano wa pili ni Bw Nazir Karamagi. Huyu Bw pamoja na kigogo mmoja wa mkoa wa Morogoro ambaye ni mbunge, inasemekana kuwa ndio waliochapisha zile takataka zote za kampeni nilizotaja hapo juu. Sasa mazagazaga yote yale ya kampeni kwa nchi nzima kugharamiwa na watu wachache namna hiyo unadhani jamaa wana pesa ndogo? Sasa kama hisa zao ni hizo, je mkuu ana ubavu wa kuwang'oa? Thubutu! Hiyo ni mifani michache tu, nadhani kuna wengine hapa wataleta mifano mingi zaidi.
Kikubwa atakachofanya kwa sasa ni kuwahamisha wizara tu, leo jamaa akichafua hapa, anapelekwa pale, na kesho mahali pengine, hadi 2010 inafika ikiwa anafanya usanii huu huu.
Ajidhaniye amesimama, aangalie asije kuanguka!