Hivi Kikwete anasubiri nini huku tayari dalili zimeshaanza kuonekana?

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,483
159
Heshima mbele wanabodi,

nimekuwa nikiwaza tunapoelekea na nimekosa jibu,Mambo mengi yanafanyika nchini yamejaa usanii mtupu na watendaji wameshinda kuwajibika ipasavyo katika kutupatia maisha bora sisi watanznia.

Suala la Mkataba wa Buzwagi, suala la richmond, suala la Ukraine, suala la mikopo ya wanafunzi, suala la Ditto, suala la kufukuzwa mhasibu wa wizara ya elimu, suala la helikopta za jeshi, suala la kasungura ambako sisi hatujakaona.

Suala la MOI: Hivi Muungwana anasubiri nini kuwaondoa Mawaziri hawa, Watendaji hawa, wakati dalali mbaya zilishajionesha ya kuwa utendaji wao ni wa mashaka na unadhidi kutududumiza sisi wana wa watanzania?

Sina ubaya na hawa watu ila inauma sana. Naomba kuiwasilisha Hoja Nzito, tukiungana kwa pamoja kama JF na kuwa Busara zetu tushnikize mawaziri na watendaji wote ambao wameonesha kushindwa kutulea maendeleo tunayotaka wang'olewe,. Naamini muungwana unasoma mada hii nayo, tupe raha watanzania.

Mafisadi wote: Kama uko ofisi yoyote naomba utupe Watu wanokwamisha maendeleo, na Naapa Nitakusanya majina yote na nitafunga safari mimi mwenyewe mpaka ikulu kumplelekea Muungwana..uwe na ushahidi wa kutosha..

Nimechoka na Usanii,na niko tayari kwenda kumuona Amri Jeshi Mkuu,

Mhe. Mwanakiji alishaanza na kampeni ya Msolla Ang'oke
Mie naendeleza jina la pili Karamagi ang'oke..
 
inaonekana hawa mawaziri wana hisa kubwa sana kuliko aliyo nayo muungwana katika serikali yake. au inawezekana serikali yake iliundwa na hao hao ambapo yeye muungwana hana majukumu ya kuweza kuwajibisha hata mmoja.
 
Mkombozi,
Kwa mujibu wa taarifa zisizo rasmi kutoka jikoni, ni kwamba mawaziri waliopo madarakani sasa ndio waliotoa fungu kubwa katika kumuweka mkuu pale alipo, sasa kuwaondoa kabla hisa zao hazijaisha ni sawa na kukata tawi ambalo bila shaka unakuwa umelikalia. Unafikiri matokeo yake ni nini?
Jamaa hawezi kuwafukuza mawaziri wanaochemsha kwa sababu walichangia kwa kiasi kikubwa sana kumuwezesha muungwana kushinda. Wengine waliwahonga wahariri ili habari njema zisambazwe na mtandao ufahamike, wengine walianzisha tovuti na kuzilipia katika kutangaza jina la mkuu, kuna wengine ndio waliochapa zile khanga, T shirts, kapelo, beji, vipeperushi na mabango. Sasa ukiwaondoa watu muhimu kama hawa unatarajia nini? Hawa ndio siri ya ushindi wa kishindo wa 80%, kwa hiyo ndio uhai wenyewe wa muungwana, ndio maana anagwaya kuwang'oa. Hio ngumu!
Mfano mzuri, mkuu wa mkoa wa Manyara Bw Henry Daffa Shekifu ni mwanamtandao na alishiriki kwa kila hali kumpigia debe muungwana tangu uchaguzi wa 1995. Habari hizi alizisema mkuu, mie nilikuwa sifahamu kabisa kuwa jamaa alikuwa ni mpiga debe wa mkuu. Huyu bwana alipogombea ubunge kule kwao Lushoto alimwagwa katika kura za maoni na kwa kuwa ni mwanamtandao, akaongea na mkuu, mheshimiwa mkuu akaahidi kuwa sisiemu haitamtupa (kumbuka nilikuwepo wakati wa kampeni za 2005 wakati ahadi hii inatolewa pale uwanja wa Omar Ali Juma Lushoto). Mwenye shaka na ushahidi huu awaulize watu wa Lushoto, bifu kati ya Shekifu na mbunge wa sasa Bw Mshangama. Mara baada tu ya mkuu kukwaa ulaji tukashtukia Shekifu ni mkuu wa mkoa wa Mtwara. Akarudi na kuwatambia waliomyima kura, kuwa kama walidhani wanamkomoa basi wameula wa chuya, sasa anapeperusha bendera ya taifa, sio ya chama tena. Sasa Bw Mkombozi, ama Mushobozi, unadhani mtu kama huyu akibofoa katika uongozi ataadabishwa kweli?
Mfano wa pili ni Bw Nazir Karamagi. Huyu Bw pamoja na kigogo mmoja wa mkoa wa Morogoro ambaye ni mbunge, inasemekana kuwa ndio waliochapisha zile takataka zote za kampeni nilizotaja hapo juu. Sasa mazagazaga yote yale ya kampeni kwa nchi nzima kugharamiwa na watu wachache namna hiyo unadhani jamaa wana pesa ndogo? Sasa kama hisa zao ni hizo, je mkuu ana ubavu wa kuwang'oa? Thubutu! Hiyo ni mifani michache tu, nadhani kuna wengine hapa wataleta mifano mingi zaidi.
Kikubwa atakachofanya kwa sasa ni kuwahamisha wizara tu, leo jamaa akichafua hapa, anapelekwa pale, na kesho mahali pengine, hadi 2010 inafika ikiwa anafanya usanii huu huu.
Ajidhaniye amesimama, aangalie asije kuanguka!
 
Mkombozi,
Kwa mujibu wa taarifa zisizo rasmi kutoka jikoni, ni kwamba mawaziri waliopo madarakani sasa ndio waliotoa fungu kubwa katika kumuweka mkuu pale alipo, sasa kuwaondoa kabla hisa zao hazijaisha ni sawa na kukata tawi ambalo bila shaka unakuwa umelikalia. Unafikiri matokeo yake ni nini?
sasa Msola alitoa wapi pesa ya kuhonga huku alikuwa Mtumishi wa Umma??
Sasa mie naanza kupata wasiwasi kama BWana Hosea anafanya kazi kwa ufanisi,kwa Mshahara gani ulimuwezesha kupata pesa ya kufanyia Kampeni??
ALfu hawa watu wana dharau na Maneno ya ovyo,Kwa Maoni yangu Wizara ya Elimu ya Juu inhitaji Re-structuring ya khali ya juu,kuanzia waziri hadi watendaji wa juu wa wizara hiyo,
Mie nimeapa kabal ya Mwezi huu kuisha Lazima niende kumuona Muungwana..Hata Katibu kiongozi,Aniambie ni kwanini toka nimetuma maswali yangu katika tovuti yao hayajajibiwa,na Rais anasubiri nini kuwang'oa hawa mafisadi?
Serious,Niko Tayari kwa lolote hata kwa kuwekwa ndani ila laazima nimweleze ukweli Mkuu wakaya,Mie naumia sana na nchi hii..
Nilimpigia hadi kampeni nyumbani kwetu Bunda na nisingependa kura yangu ipotee bila mafanikio wala maemndeleo.

Mwanachama na Kada Wa Chama Cha Mapinduzi
 
niliweka post moja last week ila naona Admin aliing'oa,Kuna watu walibisha kwamba hauwezi kulipia gharama za dola 1500 kwa siku katika hotel za kitanzania.nimekusanya information za kutosha
Rack Rates 2008 (subject to change):

Full Board (includes game drives, wines, spirits and liqueurs from the Fine Wine Card & laundry)

$1500 ppn

Single Surcharges.
link yake ni hii hapa:http://www.go-safari.com/Serengeti/Sasakwa.htm

aliyesema udaku,naomba auulize tena.Mie huwa sitoi habari ya udaku hata moja,Na kwa taarifa yako,Mkuu wa nchi ameshamaliza kupitia ripoti ya mapendekezo ya kubadili Muundo wabaraza la mawaziri,kitafanyika kikao cha dharura na kamati kkuu ya chama cha mapinduzi hivi karibuni ili awashirikishe kabala ya kufanya maamuzi mazito.
 
Na kwa taarifa yako,Mkuu wa nchi ameshamaliza kupitia ripoti ya mapendekezo ya kubadili Muundo wabaraza la mawaziri,kitafanyika kikao cha dharura na kamati kkuu ya chama cha mapinduzi hivi karibuni ili awashirikishe kabala ya kufanya maamuzi mazito.[/QUOTE]

Kwa hiyo akitoka Serengeti anakwenda Butiama kwa ajili ya CC na NEC? Je, tutarajie "AZIMIO LA BUTIAMA"?
 
Hayo sasa matani mobu,Mbona alisema havunji kebineti yake ya mawaziri?Ebu dadafua vizuri.
Mkuu Mbuzi haki,Mkuu wa nchi alisema haya wakati akijibu swali la kuhusu uzvumi wakubaidili mawaziri

Swali:Watu wategemee nini ili ikifika mwaka 2010 kusiwe na kusutana? Na je, kuna ukweli gani kuhusu uvumi unaoenea mitaani na kuwaweka watu matumbo joto kwamba kuna mabadiliko ya Baraza la Mawaziri?


JibuWatu wategemee nini 2010? Mimi nasema kitu cha kutegemea ni kwamba kama nilivyosema nadhani narudia yale yale kwamba kuna kitu ambacho tumewaahidi Watanzania. Tumeahidi kwenye ilani yetu, tumeahidi huko. Kuna yale ya papo kwa hapo. Jitihada tunazohitaji sasa ni ikifika 2010 waseme tuliyoahidi yametimia, nisingependa tufike 2010 tusutwe; Tulisema hili, hakuna tulisema hili hakuna. Mimi nadhani kwamba tutatekeleza ahadi.
Uvumi wa Baraza la Mawaziri ni uvumi tu. Baraza la mawaziri nalibadilisha wakati wote ni uvumi tu. Ikiwapo haja tutabadili. Kama hakuna haja tutaendelea. Lakini kwa sasa tuchukulie kwamba ni uvumi au ni matakwa ya watu.
 
Wazo lako zuri. Ila Tuangalie na lingine :
Hivi huyu mkuu wa chuo cha Taifa cha Utalii- National College of Tourism, Tandika; mbona yeye Serikali hammuliki pamoja na madhambi yake yote ya kuvuruga chuo hiki kizuri cha Taifa? Ana majigambo mengi sana na anadai hawezi kuondolewa chuoni eti kwamba amewakumbatia wakuu wa nchi na anayetaka kumsababishia aondolewe wadhifa wake ndio huyo ataondolewa wa kwanza.Mara anadai amezaa mtoto na Katibu mkuu Luhanjo, mara anadai ni mke mdogo wa Rais Kikwete na majigambo mengine mengi. Hivi kwanini Serikali isimmulike na kugundua matatizo mengi aliyo nayo? Je Tanzania tunakwenda wapi?
 
Wazo lako zuri. Ila Tuangalie na lingine :
Hivi huyu mkuu wa chuo cha Taifa cha Utalii- National College of Tourism, Tandika; mbona yeye Serikali hammuliki pamoja na madhambi yake yote ya kuvuruga chuo hiki kizuri cha Taifa? Ana majigambo mengi sana na anadai hawezi kuondolewa chuoni eti kwamba amewakumbatia wakuu wa nchi na anayetaka kumsababishia aondolewe wadhifa wake ndio huyo ataondolewa wa kwanza.Mara anadai amezaa mtoto na Katibu mkuu Luhanjo, mara anadai ni mke mdogo wa Rais Kikwete na majigambo mengine mengi. Hivi kwanini Serikali isimmulike na kugundua matatizo mengi aliyo nayo? Je Tanzania tunakwenda wapi?

Tan karibu Jf,
Tunaomba Jina La huyo Mama hapa.Kama unaweza naomba unitumie PM maelezo Kamili ya Mambo anyofanya huyo mama.

Kuzaa na Luhanjo isiwe sababu ya kula pesa zetu,Sasa ya ukombozi ni sasa.unaweza kutuma e-mail mkomboziufisadi-at-yahoo-dot-co-dot-uk
 
hk kpindi cha epa na richmond.
baadae ikawa dowans.

mwaka 2014, ufisadi bado unaendelea kupitia
tanesco.
ss ni escrow
 
jk ni mpango wa mungu ili sisi wananchi tuokoke...kwa hakika baada ya miaka 10 tutakuja mshukuru mungu kutuletea hyu dhaifu..mm binafs nmejifunza mengi katika utawala wake ambao utanifanya nisirudie makosa uchaguz mwingin
 
Mtafanya dhihaka juu ya
Jakaya muwezavyo,mtamtukana muwezavyo ukweli yko palepale jamaa anafanya kazi yake vizuri sana,changamoto zipo na anakabiliana nazo kwa akuli busara na uangalufu mkubwa sana.Uraisi sio kukurupuka
 
Mtafanya dhihaka juu ya
Jakaya muwezavyo,mtamtukana muwezavyo ukweli yko palepale jamaa anafanya kazi yake vizuri sana,changamoto zipo na anakabiliana nazo kwa akuli busara na uangalufu mkubwa sana.Uraisi sio kukurupuka

nimeamini sasa kuwa kila mtu anatafsiri yake juu ya jambo fulani. Hivi, mtu anaiba na unamwona na kumtaja kwa jina lakini inapofika kutoa ushahidi wa kile ulichokiona unampamba mara ooh ni mtu makini kwani hata wizi wake ni wa kisayansi.
Haipendezi kwa rais kuongoza miaka 10 na kuiba kwa miaka yote 10. Hata kama haibi yeye lakini wateule wake wanahusika na yeye anawakodolea macho tu!. Huo si utawala bora kulinda wezi kwa miaka 10. Amechemka na siioni busara wala hekima zake kwa hili.
 
  • Thanks
Reactions: Ole
Back
Top Bottom