Vyamavingi
JF-Expert Member
- Oct 3, 2014
- 5,794
- 5,507
Leo imebidi ni jiulize swali naomba majibu kutoka kwa Balozi Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi maana alikuwemo na yuko madarakani.
Leo Waziri Kairuki amemsimamisha kazi Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma baada ya kuitia hasara Serikali kwa kupandisha gharama za ujenzi wa jengo la Chuo hicho mwaka 2011 huko Mtwara. Waziri Kairuki ananukuu ripoti ya CAG kama uthibitisho wa tuhuma hizo. Kumbe taarifa ilikuwepo!
Mwezi January mwaka huu, Waziri Mkuu, Majaliwa alivamia TPA akiwa na ushahidi wa hujuma ilivyofanywa na Makampuni yanayoendesha Bandari kavuruga (ICDs) kwa kushirikiana na baadhi ya watendaji wa Mamlaka ya Bandari na TRA tangu mwaka 2013!
Bado kuna ubovu mwingi na hasara nyingi, na hujuma nyingi zimefanywa na wafanyabiashara wakisaidiwa na Watumishi wa ngazi za juu serikalini , tena Ikulu (rejea ruhusa ya kusafirisha wanyama hai). Taarifa zote hizo zilikuwepo na zilijulikana pale Ikulu yetu ya Magogoni, lkn hatua hazikuchukukiwa! Je, Kikwete alikuwa wapi?
Leo, watendaji wanachukuliwa hatua na Serikali ya JPM kana kwamba nchi haikuwa na Rais awamu iliyopita, maana yake nini? Kama Serikali hii ya JPM imewachukulia hatua watendaji wake kwa makosa yaliyofanyika awamu iliyopita (naunga mkono sana kwa hili), Je, ni haki kuwafumbia macho waliokuwa wanawafumbia macho wezi bila kuwachukulia hatua stahiki?
Je, tutaendelea na tabia hizi za viongozi kutowajibishwa kwa makosa ya dhahiri na makusudi kama haya ambayo waliyajua lkn hawakuchukua hatua hadi lini?
Kuna hatari kubwa huko mbele kama hatutabadilisha sheria na Katiba, kuwa na aina ya Watawala wa aina hii - awamu hii tunapiga hatua tano mbele, lkn Mtawala wa awamu ijayo anaturudisha nyuma hatua 10, tusipochukua hatua sasa hivi na JPM kusimamia kuandikwa Katiba mpya, huko tuendako tutakuwa tunacheza ngoma ya watoto.
Wakati umefika sasa wa kuweka misingi na sheria madhubuti zitakazowezesha Rais au Viongozi waliofumbia macho wizi wa mali za umma na uhujumu wa uchumi wa nchi wa wawajibishwe, vinginevyo hizo ndoto za Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2020 itakuwa ndoto za Alinacha.
Nawasilisha.
Vv