Hivi kesi ya Mpendazoe imefikia wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kesi ya Mpendazoe imefikia wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Analytical, Sep 9, 2011.

 1. A

  Analytical Senior Member

  #1
  Sep 9, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi, siko informed kuhusu hili. Hivi ile kesi ya Mpendazoe kupinga ushindi wa Mahanga imefikia wapi?
   
 2. s

  seifkud Member

  #2
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaposubiri Update ya Kesi ya Mpendazoe
  SI VIBAYA UKASOMA HABARI KUHUSU KESI INAYOENDELEA MAHAMA KANDA YA SUMBAWANGA
  Hukumu ya kesi kupinga ubunge Sumbawanga mjini
  Kesi ya uchaguzi ya kupinga kutangazwa kwa ndg Aeshi Hiraly CCM kuwa mbunge wa Sumbawanga mjini leo mashahidi wa pande zote mbili wamehitimisha kutoa ushahidi wao mbele ya jaji wa mahakama kuu mh Jaji`Bethuel Mpakani Kasefu Mmilla “J.4”(Judge incharge mahakama kuu Mbeya). Kesi hiyo inasikilizwa katika mahakama kuu mjini Sumbawanga, ambapo hoja za msingi zilizokuwa zikisikilizwa ni, moja, mchakato mzima wa uchaguzi kugubikwa na rushwa iliokuwa ukitolewa na mgombea wa CCM na pili ni uchakachuzi wa matokeo uliopelekea kutangazwa kwa bw Aeshi. Katika kesi hiyo iliyofunguliwa na bw Noberth Yamsebo aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA (mlalamikaji) anayetetewa na wakili mmoja toka mbeya na upande wa washitakiwa unatetewa na mawakili wanne. Kesi hiyo ilianza kusikilizwa rasmi tangu tarehe 27/03/2012 na leo tarehe 14/03/2012 ndio mashahidi wote wamemaliza kutoa ushahidi wao, upande wa mlalamikaji ulikuwa na mashahidi 25 na upande washitakiwa ulikuwa na mashahidi wanne tu ambao wawili kati yao “ bw Vitusi Silago mchambuzi wa mifumo manispaa ya Sumbawanga na bi Silvia Siriwa aliyekuwa mkurugenzi wa manispaa na msimamizi mkuu wa uchaguzi wa jimbo la sumbawanga mjini” (kwa sasa yuko halmashauri ya wilaya ya Ileje kama mkurugenzi) ndo wamefunga pazia la mashahidi. Vielelezo mbalimbali vilitolewa upande wa mlalamikaji na mashahidi kama ushahidi kuihakikishia mahakama kutilia manani hoja za msingi za kesi hii, moja kati ya vielelezo hivyo ni fomu mbalimbali zilizotumika kujaza, kujumlishia na kutangazia matokeo ya ubunge ambazo zilitumiwa kuchakachulia matokeo, mashahidi upande wa mlalamikaji walitoa ushahidi wao dhidi ya mgombea wa CCM ukiwepo wa kununuliwa pombe, kununuliwa baiskeli, kupewa fedha cash, ununuzi wa shahada za kupigia kura, ununuzi wa vinanda “keyboard” kwa ajili ya kwaya za makanisa mbalimbali na kuwa vyote hivyo vilitolewa kwa mashariti ya kumpigia kura mgombea wa CCM bw Aeshi. Leo mara baada ya wakili mojawapo toka wa upande washitakiwa kuiambia mahakama kuwa mashahidi toka upande wake wameisha, alisimama wakili upande wa mlalamikaji na kuomba kuwa kwakuwa kesi inaelekea mwisho basi itolewe fursa kuandaliwa majumuisho ya kesi, hoja iliyoungwa mkono na upande wa mshitakiwa, hatimaye katika kuitekeleza hoja hii, upande wa walalamikaji waliihakikishia mahakama kuu kuwasilisha majumuisho yao tarehe 26/03/2012 na washitakiwa wakaahidi kupeleka tarehe 10/04/2012, na mwisho kabisa mh jaji Bethuel Mpakani Kasefu Mmilla akahitimisha mjadala kwa kusema kuwa hukumu ya kesi hii itakuwa tarehe 30/04/2012, na ndo ukawa mwisho wa shughuli za leo kuhusiana na kesi hiyo ya uchaguzi wa Sumbawanga mjini. Katika hatua nyingine, waandishi wa habari walioko Sumbawanga na mkoa wa Rukwa kwa ujumla wamekuwa wakilalamikiwa kwa kutekwa na bw Aesh kwa kutoripoti matukio mbalimbali yanayotokea katika mwendelezo wa kesi hii tangu ianze kwani kwa kiasi kikubwa kumekuwa kukitolewa ushahidi ambao kwa kiasi kikubwa ni udhalilishaji wa bw Aeshi, moja kati ya viongozi waandamizi wa klub ya waandishi wa habari mkoa wa Rukwa alipoulizwa kuhusu hili alijibu kwa madaha kuwa “waandishi tunaangalia matukio yenye maslahi” na kusema kuwa hawajaahidiwa chochote na yeyote na kuwa wao wansubiria hukumu. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI SUMBAWANGA ILI HAKI ITENDEKE. AMINA. Nikiripoti moja kwa moja toka mahakama kuu kanda ya Sumbawanga ni mimi PTZ wa JF.

   
 3. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Nilisoma kuwa hukumu ya Mpendazoe ni siku moja baada ya May Mosi
   
 4. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Hukumu ni tarehe 2 mwezi wa 5.. Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa mahakamani Mahanga ana hali ngumu.. Bt cintoshangaa kama Hukumu ikiwa tofauti.. Mahakama haziko huru..
   
 5. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Yeah mahakama za bongo siziamini toka hukumu ya lema iwe released,mahanga kama fair atachinjwa tar 2
   
 6. n

  ndoleha Member

  #6
  Apr 11, 2012
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kwa ushahidi ule Magamba hawachomoi asilani na wakilazimisha basi hukumu hiyo itaingia kwenye Guinness World Book of Records kwani ni ajabu haswa. Tujiandae. tu kwa kurudia uchaguzi.
   
 7. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #7
  Apr 11, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  sio toka kesi ya lema tu mahakama imekuwa ikitoa ruling ambazo zipo politically influenced mfano kesi ya mgombea binafsi na nyingine nyingi kesi ya chenge kugonga na kuuwa na gari ambayo haina bima akatozwa laki saba tu etc mambo haya ndio yanasababisha wananchi kuchukua sheria mkononi na kutokuiamini mahakama chanzo cha machafuko
   
Loading...