Hivi kati ya RAS na UKAWA nani ni mgomvi? Mwenye vurugu ni nani?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Hivi mtu anaitisha uchaguzi halafu siku ya uchaguzi anaenda kuwaambia watu naahirisha uchaguzi kutokana na zuio la mahakama, Zuio lenyewe ni fake!

Jamani hapa hata kama ingekua ni wewe mtu anataka kukuchoma machoni na kidole wewe ubaki unamkodolea macho tu? lazima uwe na reaction kujihami ili usiumie.

Kwakweli kamata kamata inayofanywa na jeshila polisi ni uonevu mkubwa ambao unaweza kuibua hisia kubwa sana ndani ya jamii, polisi walitakiwa kutumia busara kidogo kwa kulitazama jambo lenyewe na mazingira yake na sio kutumia nguvu kubwa kiasi hiki kuhangaika na watu ambao hawajahatarisha amani ya nchi wala watu na mali zao ispokua wangebaki kuhangaikia majambazi ambayo matukio ya uporaji yamekua yakitokea mfululizo katika jiji la Dar.

Nauliza tena mwanzilishi wa vurugu alikua RAS au UKAWA? Kwa hali hiyo ni binadamu gani angeza kuvumilia? Huu msalaba wa Zuio fake la mahakama anaubeba nani!
 
CCm ni jipu, Magufuli ni jipu, Polisi ni jipu, Mahakama ni jipu,utatumbuaje majipu wakati mfumo mzima majipu matupu?
 
CCm ni jipu, Magufuli ni jipu, Polisi ni jipu, Mahakama ni jipu,utatumbuaje majipu wakati mfumo mzima majipu matupu?
Ifike mahali hili jeshi waajiriwe vijana venye ufaulu mzuri na sio kama tulivyozoea mtu na div 4 anakimbilia kule. Ukiona msomi na Elimu yake kakimbilia polisi ni kwa sababu ya tatizo la ajira tu na sio wito. Tuige mataifa ya wenzetu ambayo huajiri vijana creative.
 
Maneno mazima unayosema lakini vyeti feki vipo vingi sana tu mkuu. Haya yote yamesababishwa na ccm
 
Maneno mazima unayosema lakini vyeti feki vipo vingi sana tu mkuu. Haya yote yamesababishwa na ccm
Hili taifa bado lina mwendo sana kufikia tunakotaka, Yaani kama wewe ni muungwana na unawapenda watanzania unazungusha uchaguzi wa nini? Hapa hakuna kuwajali watanzania ni maslahi binafsi tu.
 
Back
Top Bottom