GE2025 Hivi kampeni za CHADEMA za no reform no election zitaruhusiwa kwenda sambamba na zile kampeni za kuelekea uchaguzi zitakapofunguliwa?

GE2025 Hivi kampeni za CHADEMA za no reform no election zitaruhusiwa kwenda sambamba na zile kampeni za kuelekea uchaguzi zitakapofunguliwa?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Dr Akili

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Posts
5,313
Reaction score
4,750
Hivi karibuni kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025 zitaanza. Tarehe ya kuanza itatangazwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi hivi karibuni. Vyama vyote vya siasa isipokuwa chadema viko kwenye harakati ya kupata orodha ya wagombea wao na kuiwakilisha INEC. Daftari la wapiga kura limeshafungwa.

Chadema haikushiriki kwenye uandikishaji wa wanachama wake kwenye hilo daftari la wapiga kura na hivyo hawataweza kupiga kura. Chadema hadi sasa hawako kwenye harakati ya kupata orodha ya wagombea wao kwenye huu uchaguzi na siku za kuwakilisha orodha hiyo kwa INEC zinakaribia ukingoni.

Muda wote huu tangia Tundu achukue madaraka, chadema imekuwa ikitumia nguvu zake zote kufanya ziara nchi nzima ya kampeni ya no reforms no election hadi kujikuta kwenye matatizo kutokana na sintofahamu ya hiyo kampeni iliyojitokeza:
1. G55 ikameguka na kuungana na CHAUMA kwani hawakukubaliana na hiyo dhana ya no reforms no election inavyotekelezwa. Muasisi wa no reforms no election ni Raila Odinga mwaka 2014 ambaye hauitekeleza kwa aina wanachofanya akina Tundu.

2. Ruzuku ya chadema ikazuiliwa na Msajili wa vyama ili kupunguza spidi ya kampeni yao. Wabakia kuwa omba omba na wanatonetone! Marafiki wao wa EU hawakuwapa hata tone moja.

3. Tundu akawekwa kizuizini akikabiriwa na mashitaka mbali mbali likiwemo la uhaini

4. Mahakama kuu ikaipiga marufuku chadema kufanya shughuli zo zote za kisiasa ikiwemo hiyo kampenj ya no reforms no election hadi pale kesi ya msngi walioshitakiwa itakaposikilizwa na kufanyiwa uamuzi.

My take: Ni dhahiri kuwa hadi kumalizika kwa hiyo sintofahamu niliyoitaja hapo juu, kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu zitakuwa zimeshaanza na hakutakuwa na reform yo yote ya sheria ya uchaguzi wala katiba itakayokuwa imefanyika.

Tulimsikia Tundu mahakamani akiomba aachiwe huru haraka kama ushahidi bado hautoshelezi kumpeleka mahakama kuu, ili akashiriki kwenye kampeni za uchaguzi mkuu. Sasa tunajiuliza huko kwenye kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu chadema watashiriki kufanya nini kwani hawatakuwa na wagombea wa kunadi wala wapiga kura wa kuwapigia kura kwani hawakujiandikisha kwa amri ya no reform no election?

Au bado wanataka wakaendelee na kampeni yao ya no reform no election sambamba na zile kampeni za vyama vingine vitakavyokuwa vinanadi wagombea wao na ilani za vyama vyao. Chadema hadi sasa haina ilani yo yote ya uchaguzi wa mwaka huu. Hivyo haina cho chote cha kunadi isipokuwa no reforms no election. Sasa wataruhusiwa kufanya hivyo? Nini madhara yake kama wataruhusiwa?
 
Kujenga msingi imara hasa wa demokrasia kunahitaji sacrifice
Chadema wanajua ugumu na hatari ya kutaka mabadiliko ili kuleta usawa.wako tayari kukosa yote lakini in a long run tutapata mabadiliko ambayo hata wewe na kizazi chako kitajivunia
 
Kujenga msingi imara hasa wa demokrasia kunahitaji sacrifice
Chadema wanajua ugumu na hatari ya kutaka mabadiliko ili kuleta usawa.wako tayari kukosa yote lakini in a long run tutapata mabadiliko ambayo hata wewe na kizazi chako kitajivunia
Hiyo long run ni mpaka lini? How long is long run? Ikumbukwe baada ya uchaguzi mkuu huu chadema haitakuwa na ruzuku kwani haitakuwa na mbunge hata mmoja bugeni. Haitakuwa na uwezo wa kujiendesha. Hata kwenye hizo reforms zitakazofanyika haitakuwa na mwakilishi, hivyo matakwa yake hayatakuwemo. Chama kitakosa mvuto na wanacham watakihama kama ilivyotokea kwelnye chama cha NCCR -Mageuzi kilipokuwa chama kikuu cha upinzani enzi za Lyatonga Mrema. Chama kinakwenda kufa. Tundu Lissu na God bless Lema watarejea kwao ughaibuni wakimwacha Mura Chacha Heche akigaragara peke yake. Mangi John Mnyika atakuwa ameshatimukia CHAUMA au CCM.
 
Walionywa mapema lakini walikaidi. Sasa wanalia kwa vibano wanavyopitia. Walidhani marafiki wao wa nje kama wa EU wale rafiki zao wa ndani kama akina Warioba wangaliwasaidia laki ni kitu ambacho hakiwezekani. Waliendelea na wanataka waendelee na huo ukhulukutabu wao. Haiwezekani.


View: https://youtu.be/kREY2F4BXGE?si=C1bstEHIn5YTGhDc
 
Back
Top Bottom